Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma, hivi Serikali itaagiza Waalimu kutoka nchi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma, hivi Serikali itaagiza Waalimu kutoka nchi gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wanitakiani, Jul 2, 2012.

 1. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali ina mpango wa kuagiza madaktari kutoka Iran kuja kuziba pengo lililotokana na Madaktari waliogoma. Nina maswali machache naomba Wanajamvi mnisaidie:

  1. Kuna mikakati gani ya kuhakiki ili kujua Madaktari wanaokuja ni qualified? maana si rahisi mtu/nchi ikatoa jembe la uhakika kwa mtu baki
  yeye akabaki na kanyanga.

  2. Ni gharama kiasi gani itatumika kuwalipa Madaktari hao? watalipwa mishahara kama waliyokuwa wakilipwa Madaktari waliogoma au
  watalipwa kama experts?

  3. Madaktari hao wageni wakija wataboresha huduma za afya nchini? wataondoa tatizo la wagonjwa kulala watatu watatu?
  watapunguzaje vifo hasa vya akina mama na watoto chini ya miaka 5? na watatumia miundombinu, vifaa vilevile au wataboreshewa?
  watakuja na dawa zao au serikali itanunua?

  4. Ikitokea Waalimu nao wakagoma (hatuombi iwe hivyo) waalimu watatoka nchi gani na wangapi watatosheleza shule zetu hasa za
  watoto wetu akina Kayumba?

  5. Iwapo Waalimu wa kutoka nje wakiagizwa watatosheleza katika masomo ya Kiswahili na Civic Education? au masomo hayo yatafutwa?

  Kwa kifupi sipati picha nini kitatokea mbele ya safari! kwa maoni yangu sioni kama maamuzi hayo yana afya njema kwa Serikali yetu.
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  toka malawi
   
 3. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Malawi wenyewe hoi kama sisi!
   
 4. mhagama1

  mhagama1 Senior Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Baba wa taifa alisema kijana bado sana kuongoza nchi kama Tanzania, ila sisi tukaona kuwa mwalimu ana hila. sasa ninajuta kwanini nilikaa foleni toka asubuhi hadi saa saba mchana ndiyo ninapiga kula then nina mchagua mtu ambaye hataki kusikia wala kutafakari mambo. Nchi imeyumba inahitaji msaada wa maombi haraka.
   
 5. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawatalipa, tutaingia mkataba na wao wapeperushe bendera ya tz kwenye meli zao za mafuta
   
Loading...