Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,881
Hakika dhana ya kuwa wabunge ni watetezi wa wananchi binafsi siioni kabisa.
Isitoshe pia kusema sioni bunge kuibana serikali zaidi ya kuipongeza.
Huu ni mwaka wa 6 toka toka serikali ya awamu ya 5 imeingia madarakani.Katika hiyo miaka 6 watumishi wa umma wamekuwa yatima hawajaongezewa mishahara zaidi ya kufuta hata posho zao. Serikali imekuwa ikitoa ahadi zisizotekelezeka kuwa kamati ya kuboresha mishahara ipo kwenye hatua nzuri za kukamilisha viwango vya mishahara.
Na haya maneno yamekuwa yakijirudia na kutamka na hayati rais magufuli,waziri mkuu majaliwa na aliyekuwa waziri wa utumishi mkuchika lakini mpaka leo hakuna cha maboresho ya mishahara.
Suala la machinga limekuwa lipo kisiasa zaidi na sio kiuchumi.
Machinga kila kukicha ni matamko wajiandae kuondoka lakini hakuna mipango ya kudumu ya kuwaandalia maeneo ya kudumu ili wafanye ujasilia mali wao.
Suala la wasaka ajira ndio halizungumzwi kabisa zaidi ya kuambiwa mjiajiri huwa najiuliza wajiajiri kwa mazingira gani mitaji wanapata wapi?
Wasaka ajira
Wengi wao walisomeshwa kwa mikopo ya bodi ya mikopo wanajiuliza tutalipaje hiyo mikopo na ajira hakuna?
Masuala yote haya wabunge walipaswa waibane serikali ili ieleze kwa kina mikakati ya kutatua.
Vikao vyote vya bunge katika miaka 6 hakuna hata kikao kimoja kilichozungumzia masuala kama vile hakuna.
Najiuliza hivi kweli wabunge hawayajua matatizo ya mishahara kwa watumishi?
Hivi kweli wabunge hawajui taabu wanayopata wamachinga ktk majimbo yao?
Hivi kweli wabunge hawajui tatizo la ajira kwa vijana?
Hakika inasikitisha kwa wabunge kutowapigani wananchi hawa badala yake wapo bungeni kuisifia serikali badala ya kuibana itatue matatizo haya.
Wahenga walisema "Aliye shiba hamjui mwenye njaa" tunajua wabunge mishahara,magari na posho za kutosha.
Sent from my sm-j600f using jamiiforums mobile App