Sioni vita dhidi ya ufisadi ikifanikiwa

Mmeanzisha mahakama ya mafisadi kwa sasa wanaishi ndege na popo. kila anayekamatwa anaishia kuachiwa kwamba mwendesha mashtaka hana nia ya kuendelea na kesi.

Serikali ya CCM ni kama filamu ya vichekesho maana wapinzani kwa sasa ni kama mmewafunga midomo na sasa Vita ya ufisadi imewashinda na kuanza kuulaumu Upinzani.
Endeleeni kununua viongozi wa upinzani labda mtafanikiwa
Hiyo biashara nayo feki. Wakanunuliwa mwili lkn imani na Roho kulekule. Ukiona naibu meya wa jiji alivyopatikana. Huenda huo ni mradi wa haraka haraka kupata mshiko wa kujenga ma gorofa kama dab. Wajanja hawa we Acha tu
 
Ningalikuwa mie ndo Jaji wa mahakama ya mafisadi ningejiuzuru maana nao ni ufisadi kula limshahara bils hata kufanya kazi. Kweli udisadi hauishi.
Atakayeshitakiwa kuwa fisadi siku hiyo aombe mwongozo majaji watoe ufafanuzi kujua maana yake akilenga uwepo wao.
Una uhakika hayo majengo yapo? Au nao ni ufisadi?
 
Ni yup huyo alikuwa kwenye list of shame na baada ya kushitakiwa waliomuweka kwenyee hio list wakaanza kumtetea ?
 
Story za mafisadi ilikusudiwa tu wa tz wajue wanavyo ibiwa na sio kuchukua hatua mimi nimesononeka zaidi na celnet ipo wazi jinsi tulivyo ibiwa waziri wa fedha kasema watakaa na wenye hisa hewa wapange ili wote tunufaike na gawio kitu ambacho hata mimi ambaye sikuenda shule nisingekubari
 
Wakati mwingine huwa nikifikiri sana juu ya hii iitwayo vita dhidi ya ufisadi, naishia kukata tamaa kabisa.

Nyakati zingine huwa najiuliza kama kweli huo ufisadi upo au ni jambo la kufikirika tu.

Wale waliokuwa mstari wa mbele kupigana hiyo vita sasa wamekuwa ndo watetezi wa watu wale waliokuwa wakiwatuhumu kuwa ndo mafisadi.

Na wale walokuwa na kigugumizi kukemea na kuupiga vita ufisadi sasa eti ndo wako mstari wa mbele kupigana hiyo vita.

Hapo ndo unaona ubovu na uozo wa siasa.

Leo hii wale wote waliotajwa kwenye ile iliyoitwa ‘list of shame’ wakikamatwa na kwenda kufunguliwa mashitaka, wale ambao ndo waliyoiandika na kuisoma hiyo ‘list’ watageuka kuwa watetezi wa watu hao hao waliowatuhumu kuwa ndo mafisadi!

Inafika kipindi mtu unashindwa kutambua ni yupi hasa aliye mzalendo wa kweli anayeuchukia ufisadi kwa dhati na nguvu zake zote!!!!

Tanzania hakuna ufisadi. Neno ‘fisadi’ ni chambo cha kujipatia kiki za kisiasa tu.

Bure kabisa!!!!
Mafisadi wapo tatizo vita ndiyo kiki, chama twawala ilitakiwa kuwafungulia mashitaka waliotajwa na cdm
 
Back
Top Bottom