Sioni umuhimu wa taasisi za umma kuwa na mawasiliano

Balvejmumt

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
2,149
2,784
Habari za asubuhi wakuu,

Nimekutana na hichi kituko mara nyingi na nimejaribu kukivumilia kimenishinda inabidi nitoe duku duku langu.

Taasisi za umma ni kwaajili ya wananchi, na taasisi hizi zimekuwa na namba ambazo zinawekwa kupitia wavuti zao, au katika majarida mbali mbali lengo likiwa endapo mtu anapohitaji huduma hasa katika taasisi hizi aweze kuwasiliana nao moja kwa moja.

Kama tunavyofahamu taasisi nyingi zipo mbali na hazipo katika kila eneo analoishi mwananchi na hata kama zitakuwepo ofisi basi ofisi hizi zitakuwa katika mgawanyo wa kanda au kiwilaya ambapo si kila mtu anaweza kupafikia kwaajili ya kujipatia huduma katika taasisi hizi za umma.

Kero ni hili la hizo namba kutokuwa hewani masaa ya kazi, au zinakuwepo hewani masaa ya kazi na hazipokelewi.

Wakurugenzi na makatibu wa taasisi za umma anzisheni kitengo cha mawasiliano na kama kipo na hakifanyi kazi kuna umuhimu gani wa nyie kuwa kwenye hivyo viti mnavyo vikalia au kuna umuhimu gani wa kuweka namba kupitia wavuti zenu?

Liwafikie hili

MEDICAL COUNCIL OF TANGANYIKA

Nawasilisha

Balvejmumt
 
Hata ww ukipewa hiyo kazi hutopokea simu nakwambia, mtu anapiga simu bila shida yeyote na kuanza kutukana tu. Mwingine anapiga simu za kipuuzi tu hana lolote eti anasalimia au amependa sauti yako mpokeaji hasa akiwa mdada.
 
Hivi ni nani alikuambia kila unayeongea naye anakuwa na akili timamu?

Hivi unafikiri wote tuna lingana?

ULIONA WAPI, NANI ALIKUAMBIA?
 
Hivi ni nani alikuambia kila unayeongea naye anakuwa na akili timamu?

Hivi unafikiri wote tuna lingana?

ULIONA WAPI, NANI ALIKUAMBIA?
Hiyo ndio sababu ya wao sio mm. Juzi juzi tu hapa nilienda ofisi moja nikawauliza mbona simu hazipokelewi ndio jibu nililopewa
 
Hata ww ukipewa hiyo kazi hutopokea simu nakwambia, mtu anapiga simu bila shida yeyote na kuanza kutukana tu. Mwingine anapiga simu za kipuuzi tu hana lolote eti anasalimia au amependa sauti yako mpokeaji hasa akiwa mdada.
KWAHIYO HUO NDIO UTETEZI WAKO WA KUHALALISHA KUTOPOKEA SIMU?

NDIO KAZI YA KITENGO CHA MAWASILIANO AU CALL CENTRE... UNAPOKEA SIMU YOYOTE ILE... IWE ITALETA FAIDA AU HAITALETA FAIDA... POKEA SIKILIZA TOA MAELEZO PANAPOBIDI...

ILA KWA OFISI ZA SERIKALI ZA UMMA... NI KWAMBA THEY DON'T NEED CUSTOMERS... BUT YOU CUSTOMERS NEED THEM. KWAHIYO HAWANA HAJA NA WEWE... WEWE KWAO NI USUMBUFU...
 
Back
Top Bottom