Sioni Umuhimu wa Maprofesa Kwenye nafasi ya baraza la mawaziri.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Aliyetudanganya kua kuwaweka wasomi hawa kwenye nafasi nyeti kama baraza la mawaziri kunaweza kubadili maendeleo ya taifa letu amepotoka.Sioni umuhimu wowote kua nao kabisa serikalini, sioni "positive impacts" zao kwenye nafasi hizo kabisa.


Wamekua watu wa matamko mengi na tata, kauli zisizoendana utendaji wao, wamekua watu wa michoro ya taswira zisizoenda na uhalisia mpaka hata kila mtu anawashangaa.Nimeshaacha kuwaamini kabisa ni bora wangebaki kuendelea kuwafundisha watoto wetu vyuoni huko.


Kwenye nchi za wenzetu watu hawa hupelekwa kwenye areas of production kama vinu vya kuzalisha nyukilia huko kama ni wataalamu wa masuala ya nishati hiyo, wengine mahospitalini na vyuoni kufundisha huko.


Kuwaweka watu hawa kwenye managements zilizojawa na matashi ya kisiasa ni kosa kubwa sana, kumweka mtu ambaye amekua akijiinamia kwenye vitabu muda wote kwenye management ni kupotoka sana maana hata muda wa interaction na jamii hana atakuwaje mwajibikaji mzuri kwenye masuala ya kijamii?


Ni bora tuendelee kuwaamini vijana wadogo kwa kuwajenga vizuri kisiasa na kiongozi vizuri ili kupata wanasiasa na viongozi wazuri wa baadaye, na wanataaluma wabaki vyuoni huko kama wanataaluma waendelee kutufundishia watoto wetu.
 
Back
Top Bottom