admissionletter
JF-Expert Member
- Sep 20, 2010
- 329
- 157
Ndugu Kipande acha kupotosha watu, hao watu wa hizo sehemu ulizozitaja (Kerege, Moga, Mbweni, Boko, Bunju, Tegeta, Ununio, Kunduchi, Mbezi ya Juu na Chini, Mwenge,Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala na Kinondoni) watatumia njia gani kufika kwenye hilo Daraja? Ujue hilo daraja linaanzia Coco beach, let say mimi natoka Kerege au Mbezi beach, kwanza nitakutana na foleni kubwa sana maeneo ya Tegeta na daraja la mlalakua. Watu wote wa sehemu hizo tukitaka kwenda coco beach ili kuja mjini itabidi tupitie njia ya msasani karibu na TANESCO Mikocheni, njia hii ni mpya lakini ni nyembamba sana, haiwezi kuhimili magari yote ya kutoka sehemu hizo ulizozitaja. Pili ukifika maeneo ya Kimweri road kuna foleni kubwa sana zinazosababishwa na Daladala na magari madogo yaendayo Masaki mwisho, Bararabara yote ya Msasani kuanzia mandazi road inafoleni sana nyakati zote. Sasa mtu atafikaje kwenye hilo daraja la Coco beach?
Simply hili Daraja litakua la wakaazi wa kile kinachoitwa MSASANI PENINSULA (MASAKI NA OYSTERBAY) ONLY. Na walengwa wakuu hapa ni Mabalozi, wazungu karibia wote wanaishi huko, Matajir na Viongozi wa serikali walio PORA NYUMBA ZA UMMA.
Suluhisho la foleni Dar liko kwenye sehemu kuu tatu.
1. Kuondoa junction na traffic lights kwenye maungio ya barabara kubwa kuu kama Morroco, Magomeni, Mwenge n.k. Nakujenga interchange kama ya Ubungo.
2. Upanuzi wa bararabara, na zijengwe kisasaa, mfano pale Sarender bridge, Daraja linaweza kutanuliwa pamoja na barabara yote ya Ali Hassan Mwinyi na kuwa na jia 12, njia 3 za kushoto kabisa ziwe za watu wa kinondoni, 6 za katikati za watu wanakwenda moja kwa moja Mwenge, na 3 za kulia za watu wa hiyo Msasani Peninsula.
3 Tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kiutaalamu, Kwa Raisi kuruhusu wafanya biashara ndogo ndogo (Machinga) kufanya biashara kwenye barabara kumeathiri sana barabara zetu. Mfano ukienda Kariakoo na Arusha mjini njia nyingi zinapitika kwa tabu sana kwa sababu hawa wamachinga wanapanga bithaa mpaka barabarani.
Mkuu hoja nzuri ila hili daraja ni moja tu kati ya mikakati ya kutatua shida za foleni unazosema. Si kwamba daraja tu ndio litatatua matatizo yote ya usafiri kwenye ukanda huo wa Dar. Haiwezekani kufanya kila kitu kwa wakati mmoja