Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Kwa macho ya kawaida unaweza kufikiri lengo la daraja hili ni kupunguza foleni ya Salender Bridge na kuwaondolea wananchi wa Dar kero ya foleni. La hasha daraja hili linalojengwa kwa gharama kubwa halitapunguza foleni kwa sababu watakaotumia daraja hili ni idadi ndogo sana ya wakazi wa jiji la dar es salaam.

bridge+pic.jpg

(under utilised bridge?).
Ukiangalia kwa jicho la tatu, lengo hasa ni kuwasaidia viongozi, mabalozi na wazungu wachache wanaoishi maeneo ya Osterbay na Masaki ambao hawazidi hata 200, labda wasikae kwenye foleni kwa muda mrefu wakichanganyika na walalahoi wa maeneo ya Mwenge, Kawe, Kunduchi, Tegeta, Boko na Bunju.

USHAURI: Kama lengo ni kupunguza foleni ya Salender Bridge ingefaa zaidi lijengwe daraja kubwa la nchi kavu kutokea maeneo ya Hananasifu au Magomeni hadi Muhimbili au Fire kuvuka bonde la Jangwani linalojaa maji kipindi cha mvua.

Daraja hili la Hananasifu - Muhimbili/Fire, lingehudumia watu wengi hasa wafanyabiashara wa Kariakoo na katikati ya jiji, ambulance, zimamoto na wafanyakazi wa kada za chini ambao ndio walio wengi, tofauti na daraja la Aga Khan - Coco beach ambalo litahudumia 'sana sana' wakazi wa Masaki na pengine kubaki 'idle' kwa kipindi kirefu.

Daraja kubwa la Jangwani si tu lingepunguza adha ya foleni ya Magomeni-Kariakoo/Posta lakini pia lingesaidia kupunguza magari yanayopita Salender Bridge.

Anyways kupanga ni kuchagua, tumechagua daraja la Coco beach kwa wadosi tukawaacha wa Mbagala wahangaike na foleni yao.

Ni ushauri na mawazo huru ya MwanaJF mzoefu Quinine.
 
Ndio matatizo ya kuongoza na kufanya mamiradi bila vision.... Tunapoteza pesa nyingi kwa miradi isiyo na faida wala tija.

Je kuna malori ya mizigo yanapita daraja hilo? Hakuna. Zaidi ya waenda majumbani na maofisini ambao wala hawana tatizo la foleni kiivyo
 
Inapendeza sana mtu anapopinga jambo, akatoa sababu kisha akaleta mapendekezo mbadala, Quinine hongera kwa hilo.

Tukirudi kwenye hoja. Kwa mtazamo wangu, hilo daraja litasaidia kupunguza foleni kwa wakazi wa Mwenge, Kawe, Mbezi, Kunduchi na maeneo yote ya huo ukanda.

Kumbuka kuna barabara imetengenezwa kwa kiwango kizuri sana kuanzia pale Mikocheni Tanesco, inakuja kutokezea Msasani, hapo watumiaji wengi watapita cocobeach kuja kutokezea mjini posta.

Lakini kinachonitatiza, bado nasikia wanataka kuipanua barabara ya AlHassan Mwinyi tena, ikiwa ni hivyo, wangeongeza tu upana wa daraja la zamani magari mengi yapite hapo kwa sababu msongamano unaanzia hapo kwenye daraja.
 
Inapendeza sana mtu anapopinga jambo, akatoa sababu kisha akaleta mapendekezo mbafala, Quinine hongera kwa hilo.

Tukirudi kwenye hoja. Kwa mtazamo wangu, hilo daraja litadaidia kupunguza foleni kwa wakazi wa Mwenge, Kawe, Mbezi, Kunduchi na maeneo yote ya huo ukanda.

Kumbuka kuna barabara imetengenezea kwa kiwango kizuri sana kuanzia pale Mikocheni Tanesco, inakuja kutokezea Msasani, hapo watumiaji wengi watapita cocobeach kuja kutokezea mjini posta.

Lakini kinachonitatiza, bado nasikia wanataka kuipanua barabara ya AlHassan Mwinyi tena, ikiwa ni hivyo, wangeobgeza tu upana wa daraja la zamani magari mengi yapite hapo kwa sababu msongamano unaanzia hapo kwenye daraja.
Mpwa nakafahamu kale ka njia, ule ni uchochoro, hautapunguza foleni popote pale
 
Halafu kwa nini liitwe jina la Hayati Selander
Kwani Selander bridge la sasa litavunjwa?

Au ni katika Straregy za kupunguza lawama kutoka kwa wananchi, ionekane kuwa ni upanuzi tu wa daraja la awali?
 
Back
Top Bottom