SIONI UMUHIMU TENA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Tamu chungu

Member
Dec 20, 2015
85
64
Kwa hali jinsi inavyokwenda mifuko ya jamii inaonekana imeshindwa kujiendesha sababu kumuambia mtu aliesitisha mkataba na kampuni aliyokua anafanya kazi kwamba asubiri miaka 55 ndo aende kuchukua mafao yake hii haiingii akirini.

Unakuta mtu ameajiriwa na kampuni flani kwa mkataba let say wa miaka mitatu,anafanya kazi mpaka mwisho wa mkataba wake akiamini anauwezo wa kwenda kuchukua chochote kitu chake ambacho alikua akikatwa kila mwezi lakini akienda kwenye mfuko ambao alijiandikisha anaambiwa asubiri baada ya miaka 55 kitu ambacho ni tofauti na matarajio yake.
Kutokana na hali hii ni bora watu wawe wanakatwa kodi tu na kinachobaki wapewe wenyewe sababu huwezi kumuambia mtu asubiri miaka 55 wakati ndo kwanza ana miaka 30.

Kama wameshindwa kuhifadhi senti za watu ni bora wakaacha ili wafanyakazi wajue wenyewe jinsi ya kujihifadhia pesa zao kwaajiri ya malengo ya baadae.
 
Back
Top Bottom