Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Sikupiga kura 2015 baada ya kujiridhisha kati ya Lowassa na Magufuli hakuna mwanaharakati mpenda mageuzi.
Wengi wakiwa ni watumwa wa masilahi ya vyama vyao walimkandia mmoja wao huku wakimpigia debe mtu wao.
Ifuatayo ni tathmini yangu ya vigogo hawa wawili:-
1) Kukwamisha vita ya ufisadi
Wote niliwapa A chanya kwa sababu zifuatazo:-
Wote wana tuhuma lukuki za ufisadi na lisemwalo lipo na kama halipo lipo nyuma laja.
Magufuli zake ni pamoja na wizi na ubadhirifu TANROADS na kwenye mizania, manunuzi mbali mbali yakiwemo MV. Dar, vivukio, daraja la Kigamboni, nyumba za watumishi wa umma, n.k
Lowassa kiroba chake ni vyakula vya wahanga wa mafuriko Lindi, mchepuko wa ziwa Victoria, Dar City Water, Richmond,l/ Dowans n.k
Wote kwa mtazamo wangu wanauchu wa kujilimbikizia mali.
2) Utawala bora.
Wote niliwapa F iliyo na mapembe kabisa.
Kifupi wote walipiga kura za aina moja bungeni kuanzia mwaka 1995-2015 ikiwemo kuirekebisha rasimu ya katiba ya Warioba.
Wote waliunga mkono wapinzani kubanwa mbavu sasa sijui mliowachagua mlitumia vigezo gani kuwatofautisha.
3) Kuimarisha ukoloni mamboleo
Hapa wote niliwapa A chanya iliyotulia kabisa
Sera ya CCM ya ubinafsishaji ilikuwa ni kuujenga upya na kuimarisha ukoloni mambo leo.
Ili kujikomba kwa Mkapa waliunga mkono kulipa madeni ya nje badala ya madeni ya ndani na kuzorotesha soko la ajira na ukuaji wa uchumi
Wote kwa kauli moja waliunga mkono misamaha ya kodi kwa wageni huku wazawa wakikamuliwa bila huruma.
Ikija bomoa bomoa bila fidia niliwaona kama Kurwa na Doto.
Kwa wale mnaowatofautisha sijui mliona nini ambacho mimi kilinipita?
Tofauti pekee niliyoiona ni uaminifu ndani ya CCM
Magufuli A plus na Lowassa F minus.
Magufuli jina lake lingekatwa angelibaki CCM hivyo ni mwanachama mwaminifu kwa chama chake. Hivyo, kinamna ninawaelewa wanaCCM walivyomkumbatia
Lowassa yeye hana itikadi wala mapenzi ila kiu yake ya kukwaa madaraka ilikwamishwa. Lowassa alikimbia CCM siyo kukemea ufisadi au ufinyu wa demokrasia bali masilahi yake yalikwazwa.
Lowassa alipoingia UKAWA aliyakata majina ya wagombea wenzie Dr. Slaa na Professa Lipumba bila kuhimiza misingi ya demokrasia ifuatwe na kufuta udi wowote ule aliokuwa nao wa demokrasia.
Kamwe UKAWA hawataweza kumtetea kwenye hili ukizingatia Lowassa alipotoka CCM hakuwa na mbadala zaidi ya kujiunga na upinzani. Ilikuwaje upinzani kumtosa Dr. Slaa na kumkumbatia mgeni ambaye hana itikadi wala mapenzi na chama chochote cha siasa zaidi ya kulinda masilahi yake.
Leo UKAWA wakimtema kugombea URAISI 2020 usishangae akarukia kwa rafiki yake Kabwe ili tu jina lake liwemo kwenye ballot box kugombea urais!