Sioni tofauti kati ya Lowassa na Magufuli!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
187,485
2,000
Sikupiga kura 2015 baada ya kujiridhisha kati ya Lowassa na Magufuli hakuna mwanaharakati mpenda mageuzi.

Wengi wakiwa ni watumwa wa masilahi ya vyama vyao walimkandia mmoja wao huku wakimpigia debe mtu wao.

Ifuatayo ni tathmini yangu ya vigogo hawa wawili:-

1) Kukwamisha vita ya ufisadi

Wote niliwapa A chanya kwa sababu zifuatazo:-

Wote wana tuhuma lukuki za ufisadi na lisemwalo lipo na kama halipo lipo nyuma laja.

Magufuli zake ni pamoja na wizi na ubadhirifu TANROADS na kwenye mizania, manunuzi mbali mbali yakiwemo MV. Dar, vivukio, daraja la Kigamboni, nyumba za watumishi wa umma, n.k

Lowassa kiroba chake ni vyakula vya wahanga wa mafuriko Lindi, mchepuko wa ziwa Victoria, Dar City Water, Richmond,l/ Dowans n.k

Wote kwa mtazamo wangu wanauchu wa kujilimbikizia mali.

2) Utawala bora.

Wote niliwapa F iliyo na mapembe kabisa.

Kifupi wote walipiga kura za aina moja bungeni kuanzia mwaka 1995-2015 ikiwemo kuirekebisha rasimu ya katiba ya Warioba.

Wote waliunga mkono wapinzani kubanwa mbavu sasa sijui mliowachagua mlitumia vigezo gani kuwatofautisha.

3) Kuimarisha ukoloni mamboleo

Hapa wote niliwapa A chanya iliyotulia kabisa

Sera ya CCM ya ubinafsishaji ilikuwa ni kuujenga upya na kuimarisha ukoloni mambo leo.

Ili kujikomba kwa Mkapa waliunga mkono kulipa madeni ya nje badala ya madeni ya ndani na kuzorotesha soko la ajira na ukuaji wa uchumi

Wote kwa kauli moja waliunga mkono misamaha ya kodi kwa wageni huku wazawa wakikamuliwa bila huruma.

Ikija bomoa bomoa bila fidia niliwaona kama Kurwa na Doto.

Kwa wale mnaowatofautisha sijui mliona nini ambacho mimi kilinipita?

Tofauti pekee niliyoiona ni uaminifu ndani ya CCM

Magufuli A plus na Lowassa F minus.

Magufuli jina lake lingekatwa angelibaki CCM hivyo ni mwanachama mwaminifu kwa chama chake. Hivyo, kinamna ninawaelewa wanaCCM walivyomkumbatia

Lowassa yeye hana itikadi wala mapenzi ila kiu yake ya kukwaa madaraka ilikwamishwa. Lowassa alikimbia CCM siyo kukemea ufisadi au ufinyu wa demokrasia bali masilahi yake yalikwazwa.

Lowassa alipoingia UKAWA aliyakata majina ya wagombea wenzie Dr. Slaa na Professa Lipumba bila kuhimiza misingi ya demokrasia ifuatwe na kufuta udi wowote ule aliokuwa nao wa demokrasia.

Kamwe UKAWA hawataweza kumtetea kwenye hili ukizingatia Lowassa alipotoka CCM hakuwa na mbadala zaidi ya kujiunga na upinzani. Ilikuwaje upinzani kumtosa Dr. Slaa na kumkumbatia mgeni ambaye hana itikadi wala mapenzi na chama chochote cha siasa zaidi ya kulinda masilahi yake.

Leo UKAWA wakimtema kugombea URAISI 2020 usishangae akarukia kwa rafiki yake Kabwe ili tu jina lake liwemo kwenye ballot box kugombea urais!
 
Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
22,443

Ili kujikomba kwa Mkapa waliunga mkono kulipa madeni ya nje badala ya madeni ya ndani na kuzoretesha soko la ajira na ukuaji wa uchumi

Ushindwe na ulegee kwa jina Yesu Kristo.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,641
2,000
Kama haya mngewaambia akina Mbowe kipindi kile kile cha kubadili gia angani pengine wangeona aibu kidogo ....ndio maana wengine tumejaa hasira na unafiki tunaofanya sasa kama vile kuna mtu katuflash 15yrs back kwenye bongo zetu ....ndio maana wachambuzi mahiri enzi hizo ambao imewabidi kutetea ujinga wa Mbowe wanaishia kutia aibu tu siku hizi .....CCM wanafanya watakavyo ....na hili tumeruhusu wenyewe ....bila kusahau ujumbe huu kwa mwanzisha mada ....mkuu wewe ni Chadema acha blah blah ...
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,392

Kama huoni kapime basi hata glaucoma
 
Wanafki waseme ndiyo!!
(makinda akiuliza bungeni)

Unatutupia lawama za nini sasa wakati jawabu lipo clear.

Na wanafiki wameshaanza sarakasi eti tumuunge mkono rais!!! Rais anayemkumbatia bashite!!!!
Pambaufu kabisa.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
187,485
2,000
Wanafki waseme ndiyo!!
(makinda akiuliza bungeni)

Unatutupia lawama za nini sasa wakati jawabu lipo clear.

Na wanafiki wameshaanza sarakasi eti tumuunge mkono rais!!! Rais anayemkumbatia bashite!!!!
Pambaufu kabisa.
Mimi sijasema hivyo, walakini na halahala
 
Nginana

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
835
1,000
Sikupiga kura 2015 baada ya kujiridhisha kati ya Lowassa na Magufuli hakuna mwanaharakati mpenda mageuzi.

Wengi wakiwa ni watumwa wa masilahi ya vyama vyao walimkandia mmoja wao huku wakimpigia debe mtu wao.

Ifuatayo ni tathmini yangu ya vigogo hawa wawili:-

1) Kukwamisha vita ya ufisadi

Wote niliwapa A chanya kwa sababu zifuatazo:-

Wote wana tuhuma lukuki za ufisadi na lisemwalo lipo na kama halipo lipo nyuma laja.

Magufuli zake ni pamoja na wizi na ubadhirifu TANROADS na kwenye mizania, manunuzi mbali mbali yakiwemo MV. Dar, vivukio, daraja la Kigamboni, nyumba za watumishi wa umma, n.k

Lowassa kiroba chake ni vyakula vya wahanga wa mafuriko Lindi, mchepuko wa ziwa Victoria, Dar City Water, Richmond,l/ Dowans n.k

Wote kwa mtazamo wangu wanauchu wa kujilimbikizia mali.

2) Utawala bora.

Wote niliwapa F iliyo na mapembe kabisa.

Kifupi wote walipiga kura za aina moja bungeni kuanzia mwaka 1995-2015 ikiwemo kuirekebisha rasimu ya katiba ya Warioba.

Wote waliunga mkono wapinzani kubanwa mbavu sasa sijui mliowachagua mlitumia vigezo gani kuwatofautisha.

3) Kuimarisha ukoloni mamboleo

Hapa wote niliwapa A chanya iliyotulia kabisa

Sera ya CCM ya ubinafsishaji ilikuwa ni kuujenga upya na kuimarisha ukoloni mambo leo.

Ili kujikomba kwa Mkapa waliunga mkono kulipa madeni ya nje badala ya madeni ya ndani na kuzorotesha soko la ajira na ukuaji wa uchumi

Wote kwa kauli moja waliunga mkono misamaha ya kodi kwa wageni huku wazawa wakikamuliwa bila huruma.

Ikija bomoa bomoa bila fidia niliwaona kama Kurwa na Doto.

Kwa wale mnaowatofautisha sijui mliona nini ambacho mimi kilinipita?

Tofauti pekee niliyoiona ni uaminifu ndani ya CCM

Magufuli A plus na Lowassa F minus.

Magufuli jina lake lingekatwa angelibaki CCM hivyo ni mwanachama mwaminifu kwa chama chake. Hivyo, kinamna ninawaelewa wanaCCM walivyomkumbatia

Lowassa yeye hana itikadi wala mapenzi ila kiu yake ya kukwaa madaraka ilikwamishwa. Lowassa alikimbia CCM siyo kukemea ufisadi au ufinyu wa demokrasia bali masilahi yake yalikwazwa.

Lowassa alipoingia UKAWA aliyakata majina ya wagombea wenzie Dr. Slaa na Professa Lipumba bila kuhimiza misingi ya demokrasia ifuatwe na kufuta udi wowote ule aliokuwa nao wa demokrasia.

Kamwe UKAWA hawataweza kumtetea kwenye hili ukizingatia Lowassa alipotoka CCM hakuwa na mbadala zaidi ya kujiunga na upinzani. Ilikuwaje upinzani kumtosa Dr. Slaa na kumkumbatia mgeni ambaye hana itikadi wala mapenzi na chama chochote cha siasa zaidi ya kulinda masilahi yake.

Leo UKAWA wakimtema kugombea URAISI 2020 usishangae akarukia kwa rafiki yake Kabwe ili tu jina lake liwemo kwenye ballot box kugombea urais!
Kwanza, kwa vile wanasiasa ni wasanii, siyo sahihi kumpima mwanasiasa kwa kauli zake. Pia kwa vile wanasiasa wengi wa Kiafrika hawana dira, siyo sahihi kumpina kwa mbwembwe zake za kisiasa (political posturing) kama lilivyo kwa sakata la makanikia. Kitu muhimu hapa ni matokeo.

Hivyo mwanasiasa anapaswa kupimwa kutokana na mitazamo yake ya kiitikadi pamoja na historia yake ya uadilifu katika utendaji na katika kuheshimu demokrasia na haki za raia.

Kiuadilifu, Lowassa na Magufuli wana historia inayotia shaka. Ukiwataka, kwa mfano, watangaze mali zao hadharani na namna walivyozipata wote watapatwa na kigugumizi.

Kiitikadi, Lowassa na Magufuli ni waumini wa sera za uliberali mamboleo ambazo matokeo yake ni kutelekezwa kwa elimu na huduma bora za afya ya umma pamoja na kumilikisha rasilimali za nchi kwa wageni. Wakiwa mawaziri na wabunge wa CCM waliratibu na kuunga mkono kwa dhati miswada yote ya sheria mbovu za uwekezaji.

Lowassa na Magufuli siyo waumini wa demokrasia, haki za raia wala utawala wa sheria. Wakiwa mawaziri na wabunge wa CCM, mbali na kushiriki kuichinjia baharini rasimu ya Warioba, waliunga mkono kwa dhati miswada ya baadhi ya sheria gandamizi kama sheria ya NGO ya 2002, sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao ya 2015.

Lakini kimuonekano, Lowassa seems to be more enlightened, more civil and more level-headed.

Hata hivyo kumpigia kura yeyote kati ya hawa wawili mwaka 2015 lilikuwa ni suala la kuchagua "the lesser devil".

Kwa vile tayari Magufuli automatically ndiye mgombea wa CCM 2020, ni wakati muafaka sasa kwa upinzanni kuandaa mgombea wa urais ambaye "can stand out of the crowd".
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom