Sioni sifa za Tundu Lisu wala Zitto Kabwe kuwa kiongozi Mkuu kabisa wa nchi

Niungane na watanzania wanaendelea na maombolezo ya Ndugu Ruge Mutahaba, ni jambo lisilobishaniwa kwamba kwa namna msiba huu ulivyopokelewa kuna Jambo la kujifunza!

Binafsi nimependa sentesi iliyosemwa na Profesa Jay, Mbunge anayeongoza binadamu na wanyama pale mikumi kwamba " thamani ya binadamu haipimwi kwa umri atakaoishi bali kwa aliyoyafanya wakati wa uhai wake"

Baada ya hayo turudi kwenye mada husika.

Yanasemwa mengi kuhusu viongozi hawa Tundu Lisu na Zitto Kabwe, majabari ya siasa za upinzani kuelekea uchaguzi wa 2020.

Haya majabari yana vitu vingi sana kichwani na yana uwezo mkubwa sana wa kutenda, kifupi ni sehemu ya watanzania wenye "akili kubwa"

Hata hivyo, kwangu hawa siwaoni kama Presidential material.

Uongozi wa juu unahitaji zaidi busara, hekima, maono, ustahimilivu, usikivu na uwezo wa kuthubutu lakini bila kutumia papara, nguvu wala hisia! Yaani, maamuzi au ujasiri wa kuthubutu unatakiwa kufikiwa baada ya tafakuri ya kina, kupima (predict) matokeo ya kinachaamriwa

Ukiwaangalia Tundu Lisu na Zitto, ni watu wanaofaa kushika nyazifa ambazo hazihitaji kuwa za mwisho kutoa maamuzi ya mwisho. Hii ni kwa sababu kwa asilimia kubwa wana hulka ya ki uanaharakati zaidi kitu kinachoweza kusababisha wasisikilize baadhi ya ushauri kutoka kwa wataalamu na kuenda na kile wanachokiamini wao.

Kwa haraka haraka, japo wengi hawampi nafasi na pengine wamemchoka, kwa upinzani presidential material namuona Mbowe kwa chadema, Profesa Safari na wengine ni Mbatia japo wengi wanaona kama amechuja!

Hata hivyo, Tanzania salama inayoweza kufuta makovu yanayoendelea kuwekwa na uongozi uliopo unahitaji kiongozi Mkuu mwenye uwezo wa tafakuri kabla ya kufikia maamuzi.

Namuona Mark Mwandosya, Jaji Samata na watu aina ya Warioba wakifaa zaidi kuja kufuta makovu.

Mtu kama Membe bado anaweza asifanikiwe sana hasa hasa kwa sababu ya kumbukumbu ya alichofanyiwa mwaka 2015. Binadamu ni binadamu tu, huenda ikawa ngumu kufutika kirahisi na yeye anatamani aonyeshe umwamba wake na pia huenda washirika wake wakamkwamisha pale atakapotaka kulipa fadhila.

Kwa kuhitimisha, timu nayo itamani ni Mark Mwandosya awe top, Freeman Mbowe awe Waziri Mkuu, Tundu Lisu awe jaji Mkuu na Zitto Kabwe awe pale BOT au basi aongoze wizara ya fedha ila sioni TL na ZK wakifaa kuwa katika top position.



Sent using Jamii Forums mobile app
Wenye akili wamwziona akili zao ninyi msio na utimamu endeleeni na kichaa wenu
 
Magufuri amefikisha miaka mitatu sasa pamoja na kuwa hana sifa kabisa za kuongoza ije kuwa miamba Lissu na Zitto .
 
Siasa za kikondoo hazitakiwi ukombozi ni vita,Uhuru aukupatikana kwa watu kucheza bao, ni mapambano kwa hoja na vitendo,ukipigwa shavu la kushoto nawe unapiga la kulia, wazee awatakiwi Lisu na zitoo wanaweza mikimiki na purukushani.
sio kwa hii nchi ya watanzania hawajazoea purukushani na mapinduzi ndo maana kwanye machafuko tz hayawezi kudumu kwa siku 3 hofu imetawala
 
sio kwa hii nchi ya watanzania hawajazoea purukushani na mapinduzi ndo maana kwanye machafuko tz hayawezi kudumu kwa siku 3 hofu imetawala

Msikariri mawazo hayo hayo siku zote zama zimebadilika ugumu wa maisha uleta ujasiri.
 
Back
Top Bottom