Sioni sababu ya kumuachia Lissu Mapema, akiachiwa mapema asikamatwe tena tumeuchoka mchezo huu

Samweli Mathayo

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
1,577
1,700
Hallo jamii mko salama ndo matumaini yangu,

Haya ni maoni yangu kama mtanzania, nina sababu zangu zinazopelekea niamini kuwa sioni sababu ya kumuachia Lissu mapema, anastahili kukaa angalau miezi minne au mitano,

Lissu anapaswa kuwekwa hapo hadi mazungumzo ya Tanzania na Barrick yaishe, maana kwa imani yangu lissu ana mkono sana katika kuyumbisha mazungumzo yanayoendelea pale jijini dsm, kuwekwa kwake ndani kutakata ushirikiano au cordination ya sehemu zinazotoa maelezo ya kusaidia upande wa pili.

Lissu akiendelea kuwekwa ndani inasaidia sana katika kudhoofisha hatua zinazopangwa kuchukuliwa na ACCACIA dhidi ya serikali ya Tanzania hakuna asiyeelewa kuwa Lissu ni miongoni mwa watu watanzania wanaotegemewa na ACCACIA kukamilisha suala lao.

Lissu kuwekwa ndani ni kwamba inarudisha heshima ya kitengo cha usalama na ikulu ya Tanzania maana tumedharauliwa sana na wageni hawa wanaotusumbua sana, na litakuwa fundisho kuwa ukitoa habari ya kupototsha Umma kuhusu rais wao mamlaka hazijanyamaza.

Lissu kuachwa azurure mtaani ingeshangaza ulimwengu kwa kuwa wangeamini rais alifanya ambayo Lissu amesema.

Lissu kuendelea kukaa ndani tutaona hata reaction za wale wenye maslahi naye, yaani wa nje wanaotaka kumtumia katika masuala yao kukwamisha taifa,

Kuachiwa kwa Lissu haraka kutasababisha mzaha kila siku kwa watanzania na police, huu utakuwa mchezo sasa, kila siku kamata achia.

Lissu kuendelea kuwa ndani inakumbusha kuwa rais ana nguvu sema nguvu hiyo watu waliisahau kwa sababu ya upole wa Kikwete.

Kwa maoni yangu wakimuachia mapema sitaona sababu ya kumkamata tena pindi akifanya kosa.

Njia pekee ni kumuweka mahabusu na kesi kuahirishwa, mara hakimu kuumwa kupata udhuru, mara utaratibu wa kumpeleka mahakaman unaandaliwa, mara bado tunasubiri maelezo ya juu.

Itasaidia kujua hata mengine ambayo hatujui maana kila mmoja ataanza kufunguka, na pili itasaidia kuwaelimisha vijana watovu wa nidhamu wa mitandaoni kuwa kashikiliwa Lissu tunayemuamini, je sisi wa hapa Manzese tukipotosha ndo itakuwaje?

Ninavyojua mimi rais wa nchi yeyyote ile hueshimiwa, uwe ulimchagua au hukumchagua,

Ikumbukwe Lissu hakuwekwa ndani kwa sababu ya ishu ya ndege ya CANADA, ila kumkashifu rais wa nchi ya Tanzania na Usalama wake, maana wanachi wenye hasira kali hawana mchezo

Samuel
 
Akae hata MAISHA.... ilimradi tu muwe na cha kueleza kwa nini anakaa huko...
1. Amekataa kupimwa mkojo.... HAMKUWA NA LA KUMFANYA
2. Amekataa kutoa maelezo pilisi.... HAMNA CHA KUMFANYA
3. AMeitwa mchochezi mara kadhaa.... HAKUNA HATA UCHOCHEZI WOWOTE ULIMTIA HATIANI

Ndugu, kumbuka kuwa

1. Wa Manzese naye ni raia kama alivyo wa huko unakoamini ndo RAIA ZAIDI
2. Kila binadamu anastahili heshima... uwe au usiwe na cheo, unastahili heshima
 
Halafu ww mtoto huwa una siasa za kipuuzi ile mbaya. Kwa taarifa yako Lissu hajawahi kukamatwa kwa kuvunja sheria za nchi hii, bali hukamatwa kwa sababu za kiitikadi kwani anaotafautiana hawapendi ukweli anaousema. Ww kwa sababu ya siasa zako za kipuuzi unamshawishi rais afuate hisia zako kumuweka Lissu ndani kinyume na sheria. Kitu usichofahamu hata akimuweka Lisu ndani kinyume na sheria hawezi kupunguza hata nukta ya ukweli anaosema. Nguvu ya rais iko wazi na kila mtu anaifahamu ila ukweli una nguvu kuliko nadaraka ya rais. Kwa hiyo sema kwa urahisi tu, hata kama Lisu anasema kweli awekwe ndani kwani ukweli anaosema unawachoma sana.
 
Back
Top Bottom