Uchaguzi 2020 Sioni sababu ya kufanya mikutano na kuwatukana wengine wakati wa kutafuta wadhamini

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,689
1,941
Mchakato wa kupata tiketi ya kugombea Urais ni kwamba unatakiwa upitishwe na chama na baada ya kupitishwa na chama unaenda kutafuta wadhamini katika mikoa ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

Kilichotakiwa ni kupata wadhamini kwa wanachama wa chama chako na hii haiitaji kupiga makele mengi au kukosoa au kuwatukana wengine Bali chama kilitakiwa kiweke utaratibu wa kuwapata wadhamini bila mikutano mikubwa yenye kutumia hela nyingi utaratibu wa sasa kama tunavyoona kwa chadema ni kama kampeni sasa zimeanza maana mgombea kupitia chama hicho kila anakopita nikuiponda Serikali na hasa personal attacks kwa rais JPM. Kwenye kuhutubia wananchi anatoa vitisho na ahadi nyingi. kwangu Mimi sioni tofauti ya kusaka wadhamini na kampeni.

Tume ya uchaguzi ilitakiwa itoe ufafanunuzi wadhamini wanatafutwaje na ni kina nani hao .kwa utaratibu wa sasa naona ni kupoteza muda,kupoteza fedha, kuanza kampeni mapema nk.Next time NEC ije na utaratibu mwingine siyo huu wa sasa.
 
Wao wanajiita wanasheria kwa hiyo Kila kitu wanakijua, ndio maana waliongeza beti katika wimbo wa taifa, Ukimuona mtu asiyekifahamu kitu harafu akieleweshwa anabisha na wewe unajifanya kumuona anaweza ila kwenye akili yako unakuwa na majibu.
 
Uwe na aibu basi, mbona CCM hujawasema ambao wamefanya kampeni miaka yote mitano? Hivi binadamu tukoje sie au ndio "nyani haoni kundule"? CCM walichokifanya jana taifa hujakiona sio? Mengine tujifunze kunyamaza basi.
Hahaha, vijana mna vibwagizo kwelikweli.
 
Kama ni kutukanwa, tuseme tu ule ukweli kuna mtu alietukanwa na kudhalilishwa hii nchi kama Tundu Lissu? Pamoja na madhila yote yaliyompata bado wanaccm hawakuwa na simile wala ubinaadamu wakamsema na kumtukana kwingi tu na mpaka sasa bado wanamtukana, sasa yeye ni malaika!? Acha awape vyenu na huyu mungu wenu ambae anapenda kusema wenzie ila akisemwa yeye mnakuja hapa hapa juu juu mnabwabwaja tu. Ukitaka kuheshimiwa jiheshimu kwanza.
 
Uwe na aibu basi, mbona CCM hujawasema ambao wamefanya kampeni miaka yote mitano? Hivi binadamu tukoje sie au ndio "nyani haoni kundule"? CCM walichokifanya jana taifa hujakiona sio? Mengine tujifunze kunyamaza basi.
Tofautisha tamasha na kutafuta wadhamini.lakini kama na hili ni kosa nalo linaitaji kukemewa!!
 
Tofautisha tamasha na kutafuta wadhamini.lakini kama na hili ni kosa nalo linaitaji kukemewa!!
Nadhani concern yako kuu ni kuanza kwa kampeni kabla ya muda husika ndugu yangu. Nami nimekujibu nikihusianisha na matukio hayo. Wewe reference yako kwa hilo ni tukio la mikutano ya Lisu kuongea na wanachama wenzake wa Chadema.
 
Mbona magufuli ameanza kampeni tokea mwaka 2016 miaka yote anafanya kampeni hajawahi kuacha mpaka sasa anagawa vyeo anafanya atakalo anatumia polisi kuwanyanyasa wapinzani .
 
Hilo halikuwa tamasha bali ni KAMPENI 100%
sababu kila msanii alimwimba Magufuli mwanzo mrisho, na wamevaa sare za chama karibu wote.

Ashukuriwe Mungu aliyeachilia roho ya faraka kwao wakaanza kupigana MITAMA🤏🦿
Kama ni campaign nalo hili ni kosa .ndiyo maana nilasema next time NEC ije na utaratubu mwingine .mgombea akishapitishwa na chama campaign imeanze Mara moja
 
Hilo halikuwa tamasha bali ni KAMPENI 100%
sababu kila msanii alimwimba Magufuli mwanzo mrisho, na wamevaa sare za chama karibu wote.

Ashukuriwe Mungu aliyeachilia roho ya faraka kwao wakaanza kupigana MITAMA🤏🦿
Yule aliyemwita mwenzake Bangi ni ccm kindakindaki, Mbasha ameonyesha Akili za ccm zilivyokuwa na yule aliyempiga mtama kaonyesha kuwa wapo wana ccm wengi hawapendi Ujinga wa ccm hii ya awamu ya kinyanyasaji.
 
Back
Top Bottom