Sioni namna Rais Samia anaweza kuinua uchumi wa Watanzania uliodorora

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,115
35,126
Tanzania kwa sasa ina serikali mpya ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu baada ya kifo cha Rais Magufuli.

Kwa sasa hatuna sababu nyingine yoyote ya kusubiri kuufahamu utawala wa Samia Suluhu utakuwaje, maana sura nzima ya serikali yake iko tayari.

Utawala huu mpya kwenye uchumi una mtihani mkubwa sana wa kuendeleza yale yaliyofanywa na Magufuli sera (ikiwa tunaamini Magufuli alifanikiwa kiuchumi) ama kupindua yaliyofanywa na Magufuli ili kufanya upya kisera (ikiwa tunaamini Magufuli alishindwa kiuchumi).

Vyovyote atakavyochagua Rais Samia Suluhu, sioni namna yoyote ile anaweza kufanya kitu chenye mafanikio makubwa ya kiuchumi.

Kwa mfano, kama Samia ataamua kutaka kuvaa viatu vya kiuchumi vya Magufuli (kuwakazia mabeberu, kujenga miradi mikubwa ya miundo mbinu pasipo uwiano wa pesa za kibajeti, kununua ndege, kuibana sekta binafsi nk) bila shaka atashindwa vibaya. she will underperform!

Kwa sababu, ni Magufuli pekee yake (kama alivyokuwa akiamini hivyo) aliyekuwa na ujasiri wa kiwango kile kufanya vile. Sera zake kiuchumi zilikuwa ngumu na hatari, kuendelea kuzibeba zilikuwa ni mzigo mzito kwake na kwa taifa, huenda hata Magufuli mwenyewe ipo siku huenda angechoka na kukubali yaishe, lilikuwa ni suala la muda tu.

Upande mwingine, kama mama ataamua kubomoa sera za kiuchumi za Magufuli ili aanze upya kwa kujenga za kwake, bila shaka angepaswa kwanza kuja na watu wapya kabisa kwenye serikali yake. Yaani kuanzia makamu wa rais, waziri mkuu na angalau nusu ya baraza lake la mawaziri lingekuwa ni sura mpya kabisa katika serikali yake.

Kitendo cha zaidi ya 95% ya baraza la mawaziri kuwa watu wale wale tena katika nafasi zile zile ni kiashirio kikubwa kuwa mama Samia Suluhu hana mawazo mapya wala fikra zozote pana nje ya kile kile kilichokuwepo.

Tujipe muda lakini tusichoke kuchambua!
 
Ni vile tu kulikuwa na kutishana na kupikwa kwa takwimu lakini hali yetu kiuchumi sio nzuri

Miradi mikubwa haijakamilika
Wastaafu mafao yao kizungumkuti
Watumishi mishahara mwaka 6 sasa
Biashara nyingi zimefunga wawekezaji wamepungi
Wakulima vilio
Deni la Taifa nimekuwa kubwa

Namuonea huruma sana Mama, kapokea mfupa mgumu mno, sijui ataanzia wapi. Kila la kheri.
 
Wanasema Adui yako muombee njaa, kinyume chake sasa.

Kama si adui yako kwa nn umuombee njaa na mabalaa.

Wengine husema aliwazalo mjinga ndilo litalomtokea
 
Mkuu kwani wewe ni mchumi au unazijua ABC's za uchumi

Maana isije kuwa unakitolea kitu ufafanuzi ilhali huna ufahamu nacho
 
Huyu mama ni kama debe tupu, sijui hata kama anajua anatupeleka wapi.
Mmh mkuu mbona mapema sana kuitana majina mabovu hivyo?

Amini nakuambia, kile udhaniacho ndio Kumbe sicho na kinyume chake.

Mimi si mfuasi wa hivi vyama lakini kwa huyu mama naamini kutakuwa na unafuu mkubwa sana kimaisha na kimaendeleo.
 
Unamshauri afanye nini mkuu tufunge uzi?
haha
giphy.gif
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom