philosophy
Senior Member
- Nov 11, 2012
- 104
- 42
SIONI MANTIKI YA SERIKALI KUTETEA SUALA LA KUTOKUTENGA PESA ZA CHAKULA KWA SHULE ZA MABWENI YALIYOJENGWA NA WANANCHI KWA KIGEZO CHA USAJILI
Baada ya serikali ya awamu ya tano kuamua kutangaza kuwa elimu ya msingi (elimu msingi) ni bure, raia wengi tumeona ni suala zuri kwa maendeleo ya kuwapatia elimu watu wengi hasa elimu msingi kama kutimiza na kufikia moja ya haki yao. Serikali tayari imeanza kutekeleza jambo hili kwa kupeleka pesa za kuendesha utoaji elimu hiyo, wakigharamia huduma zote. Lakini kumeibuka sintofahamu na lawama za wananchi juu ya serikali kuwa pesa ya chakula ya tsh.1500 kwa kutwa kila mwanafunzi zinatolewa kwa shule za mabweni yaliyojengwa na serikali tu.
Wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa shule ambazo wao kwa nguvu zao wameamua kujenga mabweni ili kuwaepusha wanafunzi kusumbuka na adha za umbali sanjali na majanga mengine ambayo yanaweza kuwakabili na kuwasababisha kutinga kupata elimu yao kwa uhuru; hazikupatiwa pesa za chakula. Wananchi wanadai shule hizi zigharamiwe pesa za chakula kama zilivyo shule za mambweni yaliyojengwa na serikali.
Serikali kupitia waziri wa tamisemi na waziri wa elimu, sayansi, teknolojia na ufundi wametolea ufafanuzi jambo hili leo katika bunge. Hoja ya utetezi wa kutokutoa pesa hizo umejikita katika hoja ya “Usajili wa Shule.” Kwamba, shule zimesajiliwa kwa makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni ‘shule za bweni’ na kundi la pili ni ‘shule za kutwa.’ Kwa hiyo serikali katika bajeti yake shule zilizotengewa pesa ya chakula ni zile ambazo zimesajiliwa kama shule za bweni ambazo kimsingi nyingi ni zile ambazo mabweni yamejengwa na serikali. Na shule zile ambazo zimesajiliwa kama shule za kutwa hazikutengewe bajeti ya pesa ya chakulua, sababu kuu ni kwamba serikali inazitambua kama shule za kutwa na wanafunzi wanatoka makazini kwao au kwa wazazi wao. Ila kwa msisitizo, mh. Simbachawene amekili kuwa serikali inazitambua shule ambazo zimesajiliwa kama shule za kutwa ila zina mabweni na wanajua wazi kuwa zipo shule zaidi ya 3000 zenye mabweni (yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi) kwa usajili wa shule za kutwa. Kwa hiyo ndio sababu hawakutenga pesa za chakula kwa shule hizo.
Hakika kwa kigezo cha usajili, kweli wako sahihi. Lakini majibu haya hayaridhishi hasa ukitafakari kwa kina na bado hakuna mantiki katika utetezi huo na si busara yoyote katika uamuzi huo kwa sababu zifuatazo:
· Ebu tujiulize lengo au mantiki ya serikali kutoa chakula kwa shule za bweni zilizosajiliwa kama shule za bweni ni nini? Jibu ni kwamba kwa kuwa wanafunzi hawakai nyumbani kwao na wanakaa shuleni, kwa hiyo ni jukumu la serikali kuwapatia chakula. Ni kweli kabisa!
· Je, maana ya shule ya bweni ni nini? Hakika ni shule ambayo wanafunzi huishi pale shuleni wakati wa masomo na kuendesha shughuli zao za kimasomo hapo shule pasi kwenda nyumbani, ina maana wanafunzi hushinda mchana kutwa na usiku kucha wakiwa hapo shuleni. Je, shule zilizo na mabweni lakini hazikusajiliwa kama shule za mabweni wanafunzi hawaishi pale? Au zina utofauti gani na zile ambazo zimesajiliwa kama shule za bweni?
· Lakini, tujiulize pia, kuwa nani alikuwa mhamasishaji wa kuelimisha wananchi faida za kujenga mabweni katika shule za kutwa? Jibu ni serikali.
· Kama serikali walihamasisha ujenzi wa mabweni katika shule za kutwa, hawakujua kuwa wanafunzi wanatakiwa kuishi pale na watakuwa hawatoki na kurudi nyumbani kwao? Na je hao wanafunzi hawatakiwi kula?
· Kama ni shule zenye mabweni hata kama hazijasajiliiwa hivyo na serikali inazitambua zipo, inawezekanaje kuhitimisha kuwa kwa kigezo cha usajili tu kinaondoa dhana ya wanafunzi kuishi pale na kusema wanafunzi wanatambulika kama wanatoa makwao na kula makwao?
· Kama shule za kutwa zenye mabweni serikali wanajua zipo na wanazitambua, wanashindwa nini kuzipa usajili wa kutwa shule za bweni? Kwanini sheria isizitambue kama shule za bweni mara shule ya kutwa inapojengwa mabweni?
Kimsingi, mantiki ya kutoa chakula kwa shule zilizosajiliwa na kama shule za bweni ni kwa kuwa wanafunzi wanaishi pale shuleni muda wote wa masomo. Hivyo, matiki hiyo hiyo haipaswi kukiukwa kwa shule zile ambazo mabweni yamejengwa kwa nguvu ya wananchi kwa ajili ya kuwaepusha wanafunzi na adha za kutwa, kwa sababu wanafunzi napo wanaishi pale muda wao wote wakati wa masomo. Kumbe kitendo cha serikali kutogharimia chakula kwa shule hizo ni uonevu au ni ubaguzi wa hali ya juu na wala suala hilo halina mantiki msingi ya kulitetea, na maamuzi hayo hayana busara yoyote hata kama wamefuata sheria. Sijawahi kuona shule ya bweni na wakati huo huo ni shule ya kutwa – kwamba mabweni yapo na wanafunzi wanayatumia ila inafika muda sasa wanarudi nyumbani kwao. Kama ni hivyo hakuna faida ya kuwepo mabweni.
Ni ushauri wangu kwa waziri wa tamisemi na elimu mh. Simbachawene na Ndalichako kutafakari kwa kina na kwa busara zaidi kuona kuwa kwa hili serikali imekengeuka, imekosea na ikubali udhaifu huo na inatakiwa ifanye iwezekanavyo kuanza kutoa pesa za chakula kwa shule zenye mabweni ila hazijasajiliwa kama shule zenye bweni ilihali wanakili wazi kuwa wanajua na kutambua zipo isipokuwa ni kutambulika kisheria katika usajili. Hivyo basi bila kuzipatia chakula au kuzisajili mara baada ya kuwa na mabweni ni kuendelea kulea malalamiko ya msingi na yenye matiki kuwa serikali imezibagua shule hizo. Haiingii akili ati kwa kuwa shule hizo hazikusajiliwa kwa usajili wa shule za bweni basi ni sahihi kusema kuwa serikali inatambua kwamba zile ni shule za kutwa na hivyo wanafunzi wanatoka kwa wazazi wao na kurudi na chakula wanakipata nyumbani kwao. Jambo ambalo kimantiki si sahihi na kuchukulia hivyo ni kujikanganya pakubwa kwa serikali. Suala hili hakika linawakatisha tama wananchi na wazazi ambao kwa moyo wanaamua kujenga mabweni kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi lakini serikali inashindwa kutambua juhudi hizo kwa kugharimia chakula kwa wanafunzi.
YANGU NI HAYO