Sioni kosa la OCD wa Hai kumwambia Mbowe kuwa hatomshinda Mgombea wa CCM

Allan Clement

Verified Member
Aug 14, 2013
1,906
2,000
'Hutashinda!, nani kakuambia utashinda? Unawadanganya wananchi wako kuwa utamshinda huyo?.. HUTASHINDA HATA UFANYAJE" Hayo ni maneno niliyojaribu kuyanukuu kutoka kwenye ile video inayoendelea kutrend kwasasa,

Kama tujuavyo wapinzani wamelalamika mara nyingi kuhusu mwenendo wa jeshi la polisi nchini na baadae wengine wakadiriki kuliita POLICCM, kupitia ile video na hakuna TAMKO lolote hadi sasa ni wazi kuwa OCD amezungumza kutoka moyoni mwake, ama amezungumza ya huko JIKONI, hebu tafakari ile kauli ya HATA UFANYAJE, hii ina maana hata huo uchaguzi hapo ni kiini macho tu!
maana hata AFANYEJE!

Badala ya kumshambulia na kumnanga OCD ni vyema tukamshukuru Mungu ambaye amefunua wazi kitu gani kina happen ,
any way hivi game ya watani ni tarehe 18 au tarehe 7?

Na sisi tutawafunga tu HATA WAFANYEJE!!
 
Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,336
2,000
Kwa mujibu wa PGO, hakupaswa kuzungumzia masuala ya siasa Tena hadharani. Alipaswa kumwambia Mbowe kosa lake na nini Mbowe anapaswa kufanya na so vinginevyo.

Kushinda au kutokushinda au Nani anapaswa kushindwa alipaswa kuwaacha washindani wa kisiasa wajitambe.

Sasa kasahau majukumu yake badala yake amejiona na yeye ni mgombea.

Hivyo hawezi kuwa refa Tena kwenye wilaya husika
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,908
2,000
OCD alireact baada ya kwanza "kushambuliwa" kwamba anampendelea mgombea wa CCM.

Police wanaweza wakaipotezea ilekitu na kuacha ionekanae kuwa ilikuwa majibizano na mkwaruzano binafsi kati ya Mbowe na bwana yule. Tanzania wafanyakazi hawajui maana na umuhimu wa kubehave unapokuwa umevaa gwanda la Jeshi
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
19,924
2,000
Kwa mujibu wa PGO, hakupaswa kuzungumzia masuala ya siasa Tena hadharani. Alipaswa kumwambia Mbowe kosa lake na nini Mbowe anapaswa kufanya na so vinginevyo.....

PGO ndio utumbo gani unaleta hapa!

Mbowe kaambiwa mara ngapi!! tena kwa kubembelezwa"ingia kwenye gari basi tuondoke"

Anajifanya haelewi, dawa ndio hiyo maana nayeye inaonekana ananaju,ndio sababu akaliza "kumbe unajua eh".
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Mbowe inabidi aache tabia ya kuprovoke askari polisi. Askari hao wamemlinda tangu kampeni zimeanza. Anatakiwa kuwashukuru kwa kazi nzuri wanayofanya.

Ukimprovoke polisi, anaweza kutumia njia mbalimbali za maneno au nguvu kukuweka kwenye mstari. Kamanda alitumia busara kutumia maneno badala ya nguvu.

Nampongeza kamanda kwa kulinda amani kwenye kipindi hiki fragile cha kampeni.
 
Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,336
2,000
PGO ndio utumbo gani unaleta hapa!!!

mbowe kaambiwa mara ngapi!!,tena kwa kubembelezwa"ingia kwenye gari basi tuondoke"
anajifanya haelewi,dawa ndio hiyo maana nayeye inaonekana ananaju,ndio sababu akaliza "kumbe unajua eh".
PGO ni utumbo wako mpana wa kutokea body wastes unaounganika na ubongo wako.

Kuna siku utaelewa Nini maana yaa utawala wa Sheria Kama hujui PGO ni kitu gani.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
19,924
2,000
PGO ni utumbo wako mpana wa kutokea body wastes unaounganika na ubongo wako.

Kuna siku utaelewa Nini maana yaa utawala wa Sheria Kama hujui PGO ni kitu gani.

una BP mkuu tuliaza............

Sasa kama ni utumbo wangu unauleta hapa ili tuubanike au!

Utawala wa sheria ambao polisi anamuamuru mbowe aondoke,halafu mbowe anakaidi ndio PGO hiyo!
 
J C

JF-Expert Member
Dec 12, 2013
2,704
2,000
Sio utamshinda ni utamushinda utamhshinda? . Sijui jamaa hili ni kabira gani?.
 
sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
3,861
2,000
Mapolisi wengi hua hawajui majukumu yao ni yepi. Tatizo hua linaanzia kwenye elim zao.
 
Elicie

Member
Sep 26, 2020
43
125
Huyo OCD aliwasiliana na wapiga kura wakamwambia kuwa hawatampigia Mbowe kura? Mambo mengine ni ya kutumia tu akili ya chekechea.
 
Nkobi

New Member
Oct 3, 2020
1
20
KongolI sana. Hii tabia ya viongozi wa upinzani kusema maneno ya kashafa dharau na ya kukejeli kwa polisi, vyombo vingine vya usalama na hata viongozi wa kuu vyombo hivi na wa serikani .Pia kwa Rais na Amiri Jeshi Mkiu lazima ifike nahali ipatiwe dawa na ikomeshwe kwa maana halisi ya neno kukomeshwa. Ikiachwa Taifa hili litageuka kuwa familia ya kambale.

Na pendekeza ije kupitiwa na sheria ya maadili iongezewe meno. Ili mtu awe kiongozi wa umna kwa ngazi yetote ile kufanyike vetting ya uhakika hasa. Viongozi wa umma upande wa kisiasa ni kama tumepotoka kiasi kikubwa sana Taifa. Unategemea nini historia ya uDj, Meneja na Umiliki wa danguro? Unategemea nini hapo?

Tabia hizi za Mbowe na watu kama Lema, Sugu ndio zimewa contaminate na kunajisi mpaka wana sheria kama Lissu na sasa wamegeuka vituko na wehu kwa jamii ya wanao jielewa.
Alipaswa kumuonya Mbowe kwa taratibu za kazi na kisheria lkn sio kumtakia hivyo .hi nikunyume kabisa na misingi ya kazi yake hatakama mbowe alikaidi
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
1,614
2,000
Mgombea wa CCM Jimbo la Hai. Ni Yahaya unaishi wapi. Tunasikia Hana makazi Jimboni Hai anaishi nyumbani kwa baba yake.

Mwenye kufahamu nyumba ya mgombea wa CCM Jimbo la hai nitampatia tsh 1,000,000 na gari land cruiser VX V8 ya mwaka 2019.
 
CHIBURABANU

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
1,007
2,000
Mk
PGO ndio utumbo gani unaleta hapa!!!

mbowe kaambiwa mara ngapi!!,tena kwa kubembelezwa"ingia kwenye gari basi tuondoke"
anajifanya haelewi,dawa ndio hiyo maana nayeye inaonekana ananaju,ndio sababu akaliza "kumbe unajua eh".
Mkuu relax, chukua hayo maji hiyo chupa ndogo iliyoko hapo mbele yako piga fundo mbili au tatu,baada ya dk 15 pressure itashuka mkuu.
 
Mjamaa86

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
472
500
Jamaa akavue gwanda ya Police avae ya kijani akawe campaign manager wa mgombea wa mbogamboga, hadi hapo kashakosea sana.. Hastahili kuendelea kuvaa sare za police.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,565
2,000
Huyo OCD ame - panic, anadhani wataachea waibe kura kizembe tu, wanachokipanda huko Hai watakivuna, ole wao, uhuni wao hautavumiliwa tena.
 
RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
971
1,000
'Hutashinda!, nani kakuambia utashinda? Unawadanganya wananchi wako kuwa utamshinda huyo?.. HUTASHINDA HATA UFANYAJE" Hayo ni maneno niliyojaribu kuyanukuu kutoka kwenye ile video inayoendelea kutrend kwasasa,

Kama tujuavyo wapinzani wamelalamika mara nyingi kuhusu mwenendo wa jeshi la polisi nchini na baadae wengine wakadiriki kuliita POLICCM, kupitia ile video na hakuna TAMKO lolote hadi sasa ni wazi kuwa OCD amezungumza kutoka moyoni mwake, ama amezungumza ya huko JIKONI, hebu tafakari ile kauli ya HATA UFANYAJE, hii ina maana hata huo uchaguzi hapo ni kiini macho tu!
maana hata AFANYEJE!

Badala ya kumshambulia na kumnanga OCD ni vyema tukamshukuru Mungu ambaye amefunua wazi kitu gani kina happen ,
any way hivi game ya watani ni tarehe 18 au tarehe 7?

Na sisi tutawafunga tu HATA WAFANYEJE!!
Ni kweli kabisa, na hii ni wake-up call kwa CHADEMA kuwa hawapambani na CCM bali mapambano ni Kati yao na Jeshi la polisi.
Matukio ya Shinyanga mjini, Kyerwa, Tarime na Arusha ni ushahidi kuwa Jeshi la polisi kazi lililo nayo kwa sasa ni kulinda maslahi ya CCM na so usalama wa raia na Mali zao.
 
Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,109
1,500
'Hutashinda!, nani kakuambia utashinda? Unawadanganya wananchi wako kuwa utamshinda huyo?.. HUTASHINDA HATA UFANYAJE" Hayo ni maneno niliyojaribu kuyanukuu kutoka kwenye ile video inayoendelea kutrend kwasasa,
Kama mimi ningekuwa IGP huyu askari ningekuwa nimeshamshusha cheo na kumwondoa kwenye nafasi yake ya OCD. Kwa wakati kama huu, OCD kumwambia mgombea wa chama chochote maneno kama hayo tena wakati huu wa uchaguzi ni makosa yaliyopindukia na kulitia doa kubwa jeshi la polisi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom