Sioni faida ya Bunge hili kwa Wananchi, sio kwa uwakilishi wa kero zao wala kuisimamia Serikali, livunjwe tusipoteze muda

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Ni dhahiri hili bunge linaweza kuwa Bunge lisilo na tija kwa wananchi tangu nchi yetu imepata uhuru. Hata bunge la Chama kimoja enzi hizo wala halikuwa kama hili la sasa

Kitendo cha kufanyia 'figisu' wapinzani na kuwabeba wagombe wa Chama kimeleta madhara makubwa sana kwa Taifa letu . Wawakilishi hawa hawaoni kama wanadeni kwa watu wanao wawakilisha na hawaoni uzito wa dhamana waliyobeba.

Ataona vipi uzito wa dhamana wakati alishinda 'kiulaini' kuna waliopita bila kupingwa, kuna waliofanga kampeni 'kiduchu' , kuna ambao hata jasho halikuwatoka wala sauti kuwakauka na 'figisu' zingine nyingi katika kuhakikisha wanashinda

Ndio maana KIBAJAJI alitamka wakati amesimama Bungei kuwaambia wenzake bila yule Mzee MSINGEKUWEPO na mlikuwa HAMCHAGULIKI.

Kwa kauli hii hili Bunge haliwezi kuwa na faida kwa wananchi. Wanaoma uzito kwa wale waliofanikisha kuingia Bungeni. Ndio maana hata watu wakisema haya baadhi ya ni kuyarebisha badal michango kujikitika katika namna ya kurekebisha ili mwisho wa siku wananchi wapate ahueni ya maisha wao wanajivika utetezi kwa aliowasadia kuingia Bungeni. Zinatoka dhihaka, shutuma na ulinganisho. Hakuna binadamu mkamilifu.

Bunge limekosa mvuto, kila siku ni kuparurana, limegeuka kituko kwa wananchi, watu wanachuku tu mishahara na posho muda unaenda tunachoona na kusikia kinasikitisha.

Wananchi wanategema Bunge liisimamie serikali, liondoe sheria zinazowaumiza na kutunga sheria ya kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo. Wastaafu wanategema kusikia marekebisho ya fao la kujitoa. Watumishi wanategemea Bunge likiibana serikali kuhusu kuboreshwa kwa maslahi yao, wanufaika wa bodi ya mkopo wanategema Bunge liibane serikali kuhusu kupitiliza makato n.k

Kuna Mbunge wa CCM atakuwa mkali kwa Mbunge mwenzake ambaye ni Waziri ili awajibike? Kuna Waziri ambaye atakuwa na hofu yeyote katika utendaji wake mbele Mbunge mwenzake wa CCM.

Mama yetu hata wewe hili Bunge halitokusaidia ikiwa Mawaziri ambao ni wasaidizi wako hawasimamiwi vizuri katika utendaji wao wa kazi.

Maoni yangu Bunge lingevunjwa, warudi kuomba ridhaa ya wananchi bila 'mbeleko' ili wakiwa Bungeni wajua kuwa wana dhamana kwa waliowaweka katika nafasi hiyo ya kuwawakilisha.

Ilivyo sasa tunapoteza kodi zetu kwa mishahara na posho kubwa wanazolipwa na pia tunapoteza muda zaidi kwani kwenda na Bunge hili miaka minne ni hasara kwa wananchi haliisaidii serikali katika utungaji sheria na usimamizi ili kuleta maendeleo.

Mama yetu warudishe kwetu waombe ridhaa bila 'figisu' wala 'mbeleko'

BUNGE LINATUZINGUA WANANCHI, MAMA TUSAIDIE TULIZUNGUE
 
Sio bungeni tu, hata mabaraza ya madiwani imekuwa kama vijiwe vya kahawa. Kosa kubwa la CCM ni kulazimisha CCM pekee ndio itawale. Kibaya zaidi wakurugenzi wote ni makada wa CCM, UKIWAKUTA VIKAO VYAO UTADHANI KITCHEN PARTY.
 
Sio bungeni tu, hata mabaraza ya madiwani imekuwa kama vijiwe vya kahawa. Kosa kubwa la CCM ni kulazimisha CCM pekee ndio itawale. Kibaya zaidi wakurugenzi wote ni makada wa CCM, UKIWAKUTA VIKAO VYAO UTADHANI KITCHEN PARTY.
Hawatutendei haki wananchi
 
Unashauri alhamis mama avunje hili dubwasha?
EzEbMraWYAMjajW.jpeg
 
Back
Top Bottom