Sioni dalili za malaika kuishi Kama Mashetani.

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,123
2,000
Kwa hali inavyoonekana hali bado mbaya sana kwa wanaoishi kama mashetani mpaka sasa.

Kama kulikuwa na mpango wa malaika kuishi Kama mashetani na mashetani kuishi Kama malaika basi mpango huo huenda Mungu ameukataa. Huenda ameukataa kwa kuwa Mungu huwa hapendi binadamu kulipa visasi.

Vyakula vimepanda bei, na sasa umeme kupanda bei umeongeza msumari ktk jeneza. Hapa tunategemea mfumuko wa bei na kupanda zaidi gharama za maisha kwa walala hoi.

Wakati serikali ikipandisha bei ya umeme yenyewe haijapandisha maslahi kwa wafanya kazi wake kibaya zaidi imeongeza makato ya 15% ktk mishahara hiyo hiyo midogo inayolalamikiwa kwa wanufaika wa Elimu ya juu.

Rafiki yangu mmoja anasema alikopa mkopo benki akabakiza laki zake mbili zimlinde kimaisha lakini sasa ongezeko la makato ya bodi ya 15% ghafla tuu yanamchanganya kiasi cha kupagawa.

Anasema kwa hali hii mbona yeye hataishi tuu Kama mashetani Bali atakuwa pepo mbaya kabisa hapa duniani. Amekata tamaa anatia huruma Sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom