Sioni dalili ya maisha ya watanzania kuboreshwa

cyrax

Senior Member
Mar 12, 2017
105
88
Kama Sera y serikali ya awamu ya 5 ya viwanda na kurahisisha maisha ya watanzania hasa kauli mbiu ya serikali ya maskini na Tanzania ya viwanda ambayo shabaha kuu ni maisha ya watanzania.

Binafsi sioni kama kuna dalili ya maisha ya Watanzania kupunguzwa makali yake, na hata kama dalili hiyo itaonekana tuitarajie kwa miaka mingi kwa Sera hizi za sasa.

Naangalia Sera ya viwanda na kulinda na kuongeza uzalishaji wa ndani ikiambatana na kufufua na kujenga viwanda vipya. Dalili za hatari zimeshaonekana hasa katika mafuta na sukari.
*Kuongeza tozo la mafuta ghafi kwa 25% kwa lengo la kulazimisha uzalishaji wa mafuta ya kupikia hapa nchini ambapo yanazalishwa chini ya asilimia arobaini (tani 150,000 hivi) kwa kutegemea mazao yanayozalishwa hapa nchini ili uzalishaji ufike tani 450,000 zinazohitajika kwa mwaka.

Wakati hakuna mikakati imara ya kuongeza uzalishaji wa mazao ghafi ya mafuta ndiyo maana uzalishaji upo chini.

Sioni kama kuna muwekezaji atakayeingiza malighafi kwa kodi ya asilimia 25% nje ya gharama zingine ni lazima bei ya mafuta itapanda zaidi kufidia gharama za uzalishaji.

WE HAVE A LONG JOURNEY TO GO.
 
Akili yako ndogo huwezi kuona.. nini kinapelekea nchi za wenzetu kupata maendeleo kuliko sisi hujui?we ingia istagram anza kuimba na nampenda mamaaaaaaa,nampenda bibiii, nampenda binamuuuuu, nampenda mama mdogoooo, nampenda mke mkubwa wa babuuuuu,nampenda anko na mke wakeee,nampenda aminaaaa,ukimaliza kakojoe ukalale mafanikio sio kwa ajili ya watu wenye akili ndogo hata harufu yake huwezi ijua pamoja yakuwa una pua...
 
Aisee!! Akifanya hivyo utamuita mzalendo?
 
Asieona haoni hata akionyeshwa
 
yani unategemea MAGUFULI aboreshe maisha ya mtanzania? acha mara moja hiyo ndoto, hapa ni mwendo wa kuisoma namba tu
 
Naomba serikali ya awamu ya 5 izidi kubana kila upenyo ili kila mbongo atie akili katika kutafuta maisha; mlilegezewa kipindi cha awamu ya 4 basi mkawa kila thread bongo ni new york; pesa za deals zimekata kelele mtindo mmoja. JPM kaza zaidi baba ili tuzidi kuheshimiana mjini.
 
Back
Top Bottom