Siongei na Mbwa Bali Mwenye Mbwa. Hii Ilikuwa Kauli Ya Tajiri Gani?

Aliitolea wapi? Na nani aliesikia au wote tunaambiana tusichokijua....Nani alisikia akisema hivyo? Mie nilimsikia Juma Nkamia Akitoa Kauli km hiyo au inayofanana na hiyo akiwa Bungeni....
Mkuu sio inafanana, ndio hiyo ni kweli JUMA NKAMIA NDIYE alisema
 
Hata yule aliekuwa meya wa ilala alishatoa kauli kama hii kwa mh kipindi waziri wa ujenzi walitofautiana kwenye inshu ya mabango ya barabarani yaliyokuwa kwenye wilaya yake
 
*Ukweli kuhusu Manji*

Itz known kwamba ana ugomvi wa muda mrefu na mkuu wa kaya, tangu mkuu wa kaya akiwa waziri wa ujenzi. Ugomvi wao haukua solved hadi jamaa alipotangaza kugombea Urais ndani ya CCM ambapo Manji alimwambia anapoteza muda hawezi kupita. Hata alipopitishwa Manji aligoma kumchangia na Tycoons wengi walimchangia Eddo.so from there alijenga chuki na Manji.na ameapa kumkomesha. Kuanzia saga ya wafanyakazi wasio na kibali hadi hii ya sare za jeshi ni kukomoana tu nothing beneficial. Tuachane na hizo nyingine tuongelee hii ya kukutwa na sare za jeshi. The way ilivyowekwa ni kama vile ameiba hizo sare au alikua anazitumia kinyume na utaratibu.yani yanatengenezwa mazingira ya kuonesha Manji ni gaidi anayemiliki sare za jeshi, mihuri ya idara nyeti za serikali na mambo mengine nyeti. Watu hawajiulizi nini kimetokea.hizo sare zimefikaje kwa manji? Kwanini kwake na si mwingine? Je alikua ana matumizi gani nazo?

Sasa ngoja niwasaidie kwa wale wasioelewa. Kampuni ya Quality Group ni moja ya makampuni yaliyopewa zabuni na jeshi la wananchi za kusambaza sare. Ni kama Polisi sare zote wanazovaa supplier ni Lugumi. So Lugumi anatoa sare India kwa majora anakuja kuwashonea polisi hapa bongo. Na majeshi mengine ndivyo ilivyo maana sheria ya manunuzi ya umma inakataza serikali kufanya manunuzi moja kwa moja kwa producer bila kuwa na mzabuni.

Kwahiyo si kosa uniform hizo kukutwa kwenye 'godown' la Manji masna yeye ndo suppplier. Hivi agent wa Tanga cement ukavamia godown lake na kukuta mifuko kadhaa ya cement utahoji kwanini hiyo mifuko ipo hapo? Nonsense. Manji kakutwa na uniform za jeshi maana yeye ni supplier. Period. Tuache siasa za kijinga. Na waandishi wetu wa habari hawajui hata kuuliza maswali wala kufanya uchunguzi. Wameambiwa manji kakutwa na uniform za jeshi harakaharaka wamekimbilia kuripoti bila kutafuta more details. Kwamfano wangewasiliana na viongozi wa jeshi wangewaambia Manji ni supplier wa uniform hizo. Sasa unamkamataje supplier kwa kukutwa na sehemu ya bidhaa anayosullpy? Kukuta uniform za jeshi kwa supplier wa uniform hizo si habari. Hivi unashangaa nini kukuta hirizi kwa mganga? Ingekua habari kama sare za jeshi zingekutwa kwa supplier wa konyagi au cocacola.

Pili majora ya sare hizo yamekutwa godown sio nyumbani kwa manji. Kumbuka Manji sio msimamizi wa kila siku wa godown hiyo kwa hiyo hawezi kuwajibika moja kwa moja kwa issue yoyote ndani ya hiyo godown. Hii ni kwa sababu kuna watendaji wa kila siku wa godown. Kuna warehouse manager, kuna karani na walinzi. Kwahiyo hata mali ya wizi ikikutwa humo ndani primary suspect hawezi kuwa Manji, definatelly watakua watendaji wake. Manji anaweza kuwa secondary suspect kwa factor ya umiliki. Sasa jiulize kwanini hawajamkamata manager wa hiyo godown?kwanini hawajakamatwa walinzi?bado tu hamjaelewa mpango ilioko nyuma ya pazia? Kwanini waache walinzi kwenye godown then waongozane na makamera hadi hospitali kumfuata manji aliyelazwa kitandani?

*Kuhusu mihuri:*
Sheria inasema possesion ya mihuri isiyo yako ni criminal offence, lakini Manji ni mzabuni wa muda mrefu wa mihuri ya taasisi mbalimbali za serikali. Hata mihuri ya ofisi ya PM na idara zote zilizopo chini yake supplier ni manji kupitia Quality group. Sass kama alipewa tender asupply mihuri na bado alikuwa hajadeliver kosa liko wapi?

Kukutwa na bidhaa halali hata kama raisi ametamka vinginevyo bado haikutii hatiani. Manji anafanya biashara halali ya kussuply uniform jeshini na mihuri kwenye baadhi ya taasisi za umma. Ni biashara halali, analipa kodi, hajaanza leo. Kwanini leo ionekana ni kosa mzabuni kukutwa na moja ya bidha anazosambaza, kisa tu raisi kasema?

Je walionunua bidhaa za viroba kihalali na tamko la PM likavikuta kwenye maghala yao wana kosa gani na kodi walilipa?

Manji ni supplier wa muda mrefu wa uniform jeshini na bidhaa nyingine kwenye govt institutions kama hiyo mihuri. Jeshini hadi helicopter wananunuliwa na wazabuni. Sasa tatizo liko wapi?

Hivi hayo majora ya uniform si yametoka nje? Kwani Manji ana textile hapa? Si ameinport na amepitisha Airport au bandarini with proper documents na kalipa import duties na taxes zote? Kama ni kosa si wangeanza kukamatwa watunishi wa bandari na airport waliopitisha mizigo yake? Kisha wakamatwe TRA kwa kutoza kodi kwenye mzigo wa Manji ambao ni sare za jeshi? Hii serikali ya visasi sana inapotosha ili tu kuwakomoa wale isiowapenda.

Tuache kujivisha miwani ya mbao kukataa hata Locomotive Engines zetu, ili tu kutafuta sifa ya kisiasa while its clear kwamba ziliagizwa na TRL? Halafu kwa chuki hizi tutegemee viwanda vijengwe? Ni kukomoana tu na kurudishana nyuma hadi muda wake uishe.

C n P
Mkuu samahani, pamoja na maelezo yako marefu je ni sahihi mtu kuwa na mihuri ya client wake? Kama alishasupply je hiyo alibakiwa nayo ya nini? Pia nijuavyo mimi kama alikuwa anasupply uniform za jeshi ni zamani na siyo sasa. Je hizo uniform alibakiwa nazo za nini wakati yeye si supplier wa uniform za jeshi? Maana kama existing contract na client wake then ni kosa kisheria kumiliki vitu ambavyo sheria haimruhusu kuvimiliki.
 
Hapa kuna ukweli kwamba ni tajiri wa Arusha,jina sina hakika lakini lina walakini sana! Uongo ni kwamba huyo tajiri amefilisika....ukweli mwingine ni kwamba ana Magari mengi sana....

Kauli YA tajiri mmoja... Anaitwa Tango alikua anamiliki magari mengi Sanaa YA kusafirisha mizigo hadi nje YA Nchi pale jijini Arusha Ila baada YA kumjibu moja viongozi WAKATI ule na alikua akihidani serikali pesa nyingi jamaa waliamua kumfilisi Aisee hadi Sasa ukienda Arusha pale friends corner Karbu na soko la samunge... Kama unaelekea NMC utaona magari makubwa yamepaki pale miaka na miaka....[
 
Hiyo kauli ilitolewa na kubwa la majambazi wa madini na aliyekuwa diwani wa Mererani na kada mtiifu wa CCM Justin Nyari ..
 
Kauli YA tajiri mmoja... Anaitwa Tango alikua anamiliki magari mengi Sanaa YA kusafirisha mizigo hadi nje YA Nchi pale jijini Arusha Ila baada YA kumjibu moja viongozi WAKATI ule na alikua akihidani serikali pesa nyingi jamaa waliamua kumfilisi Aisee hadi Sasa ukienda Arusha pale friends corner Karbu na soko la samunge... Kama unaelekea NMC utaona magari makubwa yamepaki pale miaka na miaka....


Na mwenyewe hajaegesha kama magari yake
 
Hii kauli imetolewa na wengi tuu!! Manji, ZHP, Zacharia, Nkamia, Nyari, etc. Hata Sumaye nae alishawahi kupigwa hiyo wakati akiwa naibu waziri mifugo!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom