Sioi Sumari kuapishwa tarehe 10 april 2012 saa tatu asubuhi - Lowassa

Mujumba

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
853
306
lowassa-akihutubia-ccm.jpg Mheshimiwa Edward Lowasa akimnadi mgombea wa ccm,kijana mtanashati na mjenga hoja za nguvu mheshimiwa Sioi Sumari alisema"Nawaahidi, kuwa sasa matatizo yenu yamekwisha, nimekuja kufunga mjadala wa ajenda ya matatizo ya ardhi, maji na umeme, mkimchagua Sioi … Aprili 10 saa 3.30 asubuhi ataapishwa na ikifika saa 7.30 mchana mimi Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM wa Mkoa wa Arusha na wabunge wenzangu, tutamwita Waziri wa Ardhi, Mama Tibaijuka (Profesa Anna) ili achukue jalada la suala la ardhi na maji na kulipeleka kwa Rais. Aliendelea kumnadi mbunge mtarajiwa kuwa Sioi "Ni mtu makini na mwenye uwezo. Naomba mumwamini na mumchague, nimekuja kumwombea kura kama mwana CCM mwenzangu. "Lakini hata nikimnadi kama mkwe si dhambi. Alimpenda Pamela, watu waache kidomodomo. Ni kijana safi, kwa hivyo nisimsifie kwa vile mimi ni mwanasiasa? Mkimchagua Sioi nawaahidi kuwa mtapata maendeleo makubwa maana tutashirikiana naye… nawaahidi hivyo mimi si mtu wa domo ni mtu wa kazi,"
 
Mheshimiwa Edward Lowasa akimnadi mgombea wa ccm,kijana mtanashati na mjenga hoja za nguvu mheshimiwa Sioi Sumari alisema"Nawaahidi, kuwa sasa matatizo yenu yamekwisha, nimekuja kufunga mjadala wa ajenda ya matatizo ya ardhi, maji na umeme, mkimchagua Sioi … Aprili 10 saa 3.30 asubuhi ataapishwa na ikifika saa 7.30 mchana mimi Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM wa Mkoa wa Arusha na wabunge wenzangu, tutamwita Waziri wa Ardhi, Mama Tibaijuka (Profesa Anna) ili achukue jalada la suala la ardhi na maji na kulipeleka kwa Rais. Aliendelea kumnadi mbunge mtarajiwa kuwa Sioi "Ni mtu makini na mwenye uwezo. Naomba mumwamini na mumchague, nimekuja kumwombea kura kama mwana CCM mwenzangu. "Lakini hata nikimnadi kama mkwe si dhambi. Alimpenda Pamela, watu waache kidomodomo. Ni kijana safi, kwa hivyo nisimsifie kwa vile mimi ni mwanasiasa? Mkimchagua Sioi nawaahidi kuwa mtapata maendeleo makubwa maana tutashirikiana naye… nawaahidi hivyo mimi si mtu wa domo ni mtu wa kazi,"
Hakika Lowassa ni mtu mstaarabu sana hapendi siasa za majitaka. Lowassa for presidency 2015.
 
KUTOKA MAHAKAMANI

Kesi ya kupinga matokeo

Mshitakiwa: Joshua Nassari

Mlalamikaji (mshitaki): Sioi Jeremiah Sumary

SINEMA YA KIHINDI INAENDELEA.................................................:A S crown-2::A S crown-2:
 
kwa nini huyo Lowassa asiufunge huo mjadala toka enzi za baba yake Sioi??? Kwa nini hayo matatizo yasiishe toka baba yake Sioi akiwa madarakani??? Acheni kuwa na akili fup namna hyo.
 
Mmmh mbona twarudishana enzi za ulimwengu ulokwisha pita; sasa hiyo title yako jombaa mbona haishabihiani na msimu husika maana kama upigaji kura ni tar 1 April 2012 iweje kuapishwa kwa mgombea kuwe tar 10Apr 1012??????
 
Mmmh mbona twarudishana enzi za ulimwengu ulokwisha pita; sasa hiyo title yako jombaa mbona haishabihiani na msimu husika maana kama upigaji kura ni tar 1 April 2012 iweje kuapishwa kwa mgombea kuwe tar 10Apr 1012??????

inaonekana dogo hujui hata vikao vya bunge vinafanyikaga miezi gani! april huwa kuna kikao cha bunge, so tarehe hiyo ndo tunategemea kumuapisha SIOI! kwani ushindi kwake ni lazima
 
inaonekana dogo hujui hata vikao vya bunge vinafanyikaga miezi gani! april huwa kuna kikao cha bunge, so tarehe hiyo ndo tunategemea kumuapisha SIOI! kwani ushindi kwake ni lazima

Acha kukurupuka kashaga, soma vizuri swali la pinokyo. Concern yake hapo ni hou mwaka. Thread inaonyesha mwaka 1012. Mjibu sasa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom