Sioi akataliwa kikao cha Kamati ya siasa Mkoa

Magwanda wanapotafuta pakutokea huwa ni raha sana.
CCM Arumeru Mashariki hatutoki hata kwa tindo tukubali yaishe

FLASHasinkingboat.gif
 
Mkuu Gracious umesema maneno mazito na haswa hiyo para ya mwisho!.

Rushwa ndio utaratibu rasmi wa kupata uongozi ndani ya CCM, this is order of the day!. Wagombea wote walikata kitu kidogo, ila mwenye kisu kikali, ndie aliyekula nyama!. Hata hivyo vikao vya maamuzi vitawajibika kumpitisha Sioi ili kulinusuru hilo jimbo!.

Siwajui sana Wameru kama ni watu wa msimamo, matokeo ya sanduku la kura ndio yatatupa picha halisi ya Wameru. Uchaguzi huu pia ndio kipimo cha kwa cha kupima upepo Jee EL anakubalika?. CCM ikishinda Arumeru, means 2015 ni EL Magogoni!. Chadema ikishinda Arumeru, hiyo itakuwa ndio kitchen Party ya CCM kujiandaa kwa send-off ya kuelekea kuwa Chama kikuu cha ipinzani, kwani ndio ufunguo wa Chadema kuingilia Magogoni!.

Kunusuru jimbo ndio nini mkuu, bado mna fikra kuwa majimbo ni ya ccm? kwenye maswala ya rushwa nakuaminia, wenyewe mnaita vibahasha vya khaki, mtasoma plate namba safari hii.
 
Kosa la siyoi ni kuwa mkwe wa lowassa....du siasa hizi....
Ukizingatia mkuu wa mkoa ,...katibu wa ccm mkoa na mlezi ..Stephen wassira wapo pale kumkaba...lowassa.

Damn if they do, damn if they don't. It will be bad kama watampitisha Sioi, but it will be worse if they don't.
 
Nimemsikia Nape akisema kupitia TBC1 kuwa ETI si lazima aliyeshinda kura za maoni Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Magamba(CCM) akateuliwa na vikao vya CCM kuwa mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao!! Hii imenistua kwanini Nape aseme hili kwa Arumeru na hakusema kwa Igunga mbona???.... Nahisi panamchezo wa kumuondoa SIOI mkwe wa Waziri Mkuu aliyefukuzwa na bunge kwa kashifa ya Richmond na Dowans asigombee ubunge pale na sasa vuvuzela wao anauandaa umma kupokea maamuzi hayo...
PEOPLES.........................
Wanataka kubadilisha wachezaji dakika za majeruhi.
 
Kunusuru jimbo ndio nini mkuu, bado mna fikra kuwa majimbo ni ya ccm? kwenye maswala ya rushwa nakuaminia, wenyewe mnaita vibahasha vya khaki, mtasoma plate namba safari hii.

na plate number yenyewe ni T2015CDM
 
Jina lolote litakalopitishwa lazima ccm igawanyike vipande vipande.
 
Jina lolote litakalopitishwa lazima ccm igawanyike vipande vipande.
Kinachotakiwa Chadema wasionyeshe kumtaka fulani acha CCM ijikoki yenyewe, ila CDM wawe tayari kumkabiri yeyote atakayepitishwa.

Hizi ni siasa you never know, never under estimate your enemy hata kama amejeruhiwa, CDM should walk CCM toe to toe bear in mind that CCM has every weapon it needs from money to electoral organs, on top of that it has experience on vote rigging.
 
Kunusuru jimbo ndio nini mkuu, bado mna fikra kuwa majimbo ni ya ccm? kwenye maswala ya rushwa nakuaminia, wenyewe mnaita vibahasha vya khaki, mtasoma plate namba safari hii.
Kwa vile jimbo lilikuwa CCM, na mgombea alichaguliwa in absentia, CCM wana kibarua kidogo tuu kulinusuru libaki kwao na Chadema ndio wana kazi ya kulitwaa!. Kwenye issues za little brown envelopes, hiyo ndio "modus operandus" ya siasa za CCM!.
 
Angalau hapa umetoa a balanced statement sijui labda kwa sababu inamhusu EL au vipi, ila sikubaliani na wewe kuwa kumpitisha Sioi ni kulinusuru jimbo maana sioni safari hii CCM watatokea wapi.
Asante, ushindi wa Sioi ni obvious, kama baba alishinda in absentia, na Chadema ilimsimamisha mtu huyo huyu, what chances does he stand kushindana na mwana mfalme?!. Usitegemee kupata matokeo tofauti, ukitumia watu wale wale na mbinu zile zile!.
 
Asante, ushindi wa Sioi ni obvious, kama baba alishinda in absentia, na Chadema ilimsimamisha mtu huyo huyu, what chances does he stand kushindana na mwana mfalme?!. Usitegemee kupata matokeo tofauti, ukitumia watu wale wale na mbinu zile zile!.
Pasco CCM ya mwaka jana si hii tunayoiona leo ya kina Nape ya kujivua magamba it is divided and you know that you cant deny na Chadema ya mwaka jana si hii ya leo hapo hakuna ubishi. Tukirudi kwa mwana wa mfalme-kwanza kuitwa hivyo tu kunampunguzia kura kwamba jimbo liwe kwenye familia moja kwa miaka 30? ina maana hakuna familia zingine? pili, Sioi anapingwa si tu na wanachama wa kawaida bali na viongozi wa juu, tatu jimbo liko Arusha bwana si Uzini, kumbuka Arusha mjini liliangukia Chadema pamoja na mgombea wa CCM kusimamiwa na manywele.
 
Asante, ushindi wa Sioi ni obvious, kama baba alishinda in absentia, na Chadema ilimsimamisha mtu huyo huyu, what chances does he stand kushindana na mwana mfalme?!. Usitegemee kupata matokeo tofauti, ukitumia watu wale wale na mbinu zile zile!.

Makundi ndani ya chama tawala yanaweza kusababisha wakapoteza jimbo hilo. Watahujumiana wao kwa wao. Kitendo cha Millya kuonyesha yuko nyuma ya nani, kinampa nafasi Mary Chatanda kufungua makucha yake ili lile beef lao liendelee kwa awamu nyingine na kuonyeshana kwamba nani zaidi ndani ya CCM Arusha.

Kitendo cha Wassira kuhudhuria kikao sidhani kama ni dalili njema. Mgogoro wa CCM Arusha unaweza kuwapa nafasi nzuri sana CHADEMA wakashinda.

Majimbo yote ambayo kulikuwa na hujuma/kuzidiana speed ya uhongaji kwenye kura za maoni, CCM ama walipoteza au walishinda kwa kuiba kura kwa kusaidiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa hiyo angalia sana mkuu inaweza kula kwao.

Halafu ukimuona zamwamwa amekuja kumwaga ***** wake jua kwamba kuna kitu kinakuja. CCM ya leo si wamoja tena, kila mtu kivyake.
 
Kwani siyo kweli? ingekuwa jambo jema kama ungekanusha kwa hoja.

Sio kweli hii habari ni ya udaku ungeipeleka kwenye gazeti pendwa la Kiu.

Kamati Kuu ya CCM ndiyo inakaa leo mjini Dar es Salaam, kupitisha jina la mgombea Arumeru.
 
mbona sielewi sasa magazeti ya yanasema eti SIOI si MTZ



Jamaa haijui hata Akheri vizuri na ndio mitaa ya kwao, na wananchi wengi wa Akheri pia hawamjui vizuri hata kwa sura. Nilipita pale "Fikiria Kwanza" juzi walipokuwa wanapiga kura za maoni, wajumbe kibao ndio walikuwa wanamuona Sioi kwa mara ya kwanza. Stori zao zilikuwa hivi,
Kumwishii Sioi? (unamjua Sioi)
Aaaan Nimwishii Ndii. (ahh simjui).

Anaijua zaidi Ulaya na Marekani
 
Back
Top Bottom