Sioi akataliwa kikao cha Kamati ya siasa Mkoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sioi akataliwa kikao cha Kamati ya siasa Mkoa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Feb 26, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MVUTANO mkali unadaiwa kuibuka katika kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM mkoani Arusha baada ya baadhi ya wajumbe kupinga uongozi wa chama hicho Wilaya ya Arumeru, kumpitisha Sioi Sumari kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.

  Chanzo cha habari ndani ya kikao hicho kilichoanza saa 5:00 asubuhi hadi saa moja usiku juzi, zinadai kuwa kitendo cha kupitishwa kwa jina la Sumari ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremiah Sumari, kimeibua malumbano makali ndani ya chama hicho.

  Habari hizo zimeeleza kuwa wajumbe wawili waliokuwa katika kikao hicho ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Katibu wa CCM mkoani Arusha Mary Chatanda, walipinga kupitishwa jina la Sumari, kwa sababu ushindi wake umelalamikiwa kila kona.

  Taarifa zimedai kuwa kitendo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira kuhudhuria kikao hicho kama msikilizaji, kimezua utata baada ya baadhi ya wajumbe kuhoji ugeni wake ndani ya kikao hicho cha maamuzi ya chama.

  Baadhi ya wajumbe waliokuwa wakipinga kupitishwa jina la Sumari, wametaja sababu iliyowafanya kutopitisha jina hilo kwa kutoa hoja kwamba ushindi wake umegubikwa na malalamiko mengi, hususan madai ya rushwa.

  “Mkuu wa Mkoa pamoja na Chatanda ndio walikuwa wakipinga kupitishwa kwa jina la Sioi kulikuwa na mvutano mkali sana, lakini hadi dakika ya mwisho kikao kilipitisha majina ya watu wawili ambao ni Sioi na Sarakikya,” kilisema chanzo chetu.

  Hata hivyo, mvutano huo unasemekana kukiweka CCM katika wakati mgumu katika harakati za kutetea jimbo la Arumeru Mashariki ambapo kwa sasa makundi mawili, yameonekana kuvutana rasmi ambapo moja linaunga mkono jina la Sioi kupitishwa huku lingine likipinga.

  Baadhi ya wanachama wa CCM mkoani Arusha wamekosoa utaratibu uliotumika kupitisha majina mawili (Sumari na William Sarakikya) ambayo yatapelekwa katika ngazi za juu kwa uamuzi wa mwisho wakisisitiza kwamba lililopaswa kupitishwa jina moja.

  Wanachama hao bila kutaja majina yao, wamepinga vilevile kitendo cha Wassira kuhudhuria kikao hicho kama msikilizaji huku wakisema, kiongozi huyo hakustahili kuhudhuria kikao hicho kama msikilizaji kwa vile kilikuwa kikao cha maamuzi.
   
 2. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu muuaji Chatanda bado yupo Arusha?!
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ila wakumbuke Lowassa ana mkono wa chuma na pia ushawishi mkubwa
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  Kosa la siyoi ni kuwa mkwe wa lowassa....du siasa hizi....
  Ukizingatia mkuu wa mkoa ,...katibu wa ccm mkoa na mlezi ..Stephen wassira wapo pale kumkaba...lowassa.
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hebu ngoja watu wake waje watupe majibu sahihi!
   
 6. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa la CCM ni Rushwa ambayo imekita mizizi,Ufisadi ni kitu cha kawaida CCM.Usishangae hata hao wanaolalamika kwamba sioi kachaguliwa kwa rushwa nao wametoa rushwa isipokua sioi kawazidi dau.Ni vigumu kuitenganisha CCM na rushwa.Hii equation ina hold sana kwa CCM; Corruption=CCM.Tatizo kubwa pia no one is clean there.Lowassa kamsaidia mkwewe Sioi,kampa hela kutoa mlungura.Lowassa mwenyewe ndo the Master Corrupt King No 1 in Tanzania.

  Hii sinema itaishia pagumu,kwa sababu katika ulingo wa kawaida i mean fair play sasa CCM wameshaishiwa nguvu.Kazi kubwa atapewa Lubuva (Mzee wa NEC) Huyu Lubuva ni shemeji wa Lowasa.So mnaweza kupata picha hapo jinsi mbinu chafu zitakavyotumika.

  CDM Wanatakiwa kuwa makini.Linda kura,Piga kampeni wakiwa werevu kama NYOKA na wapole kama NJIWA lakini wakiwa na hekima kama mfalme SULEIMAN.Pamoja Tutashinda,divided we fall.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Nguvu ya white hair naanza kuiona hapo....nadhani kama kuna mkono wa white hair ni ngumu huyo Sioi kupigwa chini CCM,mwacheni apite ila hukumu yake ni April kwenye sanduku la kura....
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Chatanda kuwepo Arusha ni mipango ya Mungu, ngoja awepo asaidie kuharakisha ukombozi.
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mamvi ananguvu ya pesa hvy sioi lazma awaoe wote wanaompinga sasa
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Weare ready for the seige hata wakiwapitisha wote (Sioi na William) waunde jina moja waitwe Siwi tutawapiga kwa knock out.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Magwanda wanapotafuta pakutokea huwa ni raha sana.
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tz ndo utaicheka sana. Mkuu wa Mkoa anaingia/kuongoza kikao cha chama ilhali ye ni mtu/muwakilishi wa serikali. There is no place unamtofautisha na shughuli za kiserikali na zile za kichama
   
 13. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hahahahahhaaahaha, umenichekesha wewe gamba! kwa hiyo yanayosemwa siyo ya kweli mkuu zomba?
   
 14. Nkanaga

  Nkanaga JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 620
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 80
  Kwa kuwa kuna dalili za rushwa ktk kupatikana Sioi, na mwenyekiti wetu ccm ni mpinga rushwa mahiri, basi Sioi akataliwe na kamati za juu. Kisha wilayani wote wawajibishwe kwa kuichafua CCM SAFI
   
 15. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Me and other 15,000 peoples like this
   
 16. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti?! Yupi? Majivuno(Lowassa) au?
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mmeshaanza kuchanganyikiwa kwani Chadema walikuwepo kwenye kikao au leo Chatanda ameanza kuisaidia Chadema.
   
 18. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Makinda anasema ubunge ni umaskini huku watu wanatumia mamilioni kuupata! Dah yule mama anazeeka vibaya.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Tanzania is descending into a hereditary feudalism.

  Mara tu unaweza kushtukia Sioi, William, January,Vita , Adam, Hussein,Amani na wenzao wa ilk yao sio tu wako bungeni, bali pia wanagawana urais kwa zamu.

  Maumivu huanza pooole pole.
   
 20. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wadau huo ni utaratibu wa Chama, maamuzi yatatoka juu. Tuache kufanya utabiri usiokuwa na tija na kuanza kukashifu watu kwa maisha binafsi.
   
Loading...