Siogopi kulogwa: Dk. Magufuli

Kwa wewe muelewa utaona na kugundua ilo kua kweli tuna serikali ya wachekeshaji,dhaifu,uswahili na wanaoamini kulindwa na ushirikina katika uongozi na maisha yao.

Ila kwa wale wasio na uwezo wa fikra wala kujenga hoja watakuambia hiyo ni sawa,halafu yatafuata matusi tu maana uwezo wa hoja ndio umeishia hapo
.
 
Hao ndio mawaziri wetu na huyu ndio mmoja kati ya wachache wanaojifanya wachapa kazi, wenye akili, wasomi na waadilifu.

Binafsi sijawahi kumkubali huyu jamaa hata siku moja,ni mpenda sifa, mtu wa kujikomba, mnafiki, mzinzi, na fisadi just like others.

Na sasa kaongeza sifa nyingine ya kijinga,mshirikina. Hilo daraja lina uhusiano gani na safari za nje za rais wakati linajengwa na pesa zetu wenyewe? I doubt if these guys have speech writers or even rehearse what the are about to speak before the public.
 
Huwezi kuwa na busara ukamsema hivyo kiongozi mwenzako tena mbele ya mteule wenu...alikuwa na nafasi ya kumlalamikia Rais na Ghasia kuhusu huyu bwana. Juu ya yote ukisoma between lines Magufuli anaamini kuwa huyu bwana ni mshirikina na atarevenge kwa kumloga!! This is very hatarious!....Ni kwenye serekali ya dhaifu tu haya yanaweza kufumbiwa macho.
 
ha ha ha ndiyo utamaduni wetu mkuu angalia kwenye vidole vya viongozi wetu wanavaa pete za madini mbalimbali unajua maana yake?"pete za bahati" wanaamini katika "bahati".
 
OMG THIS IS PATHETIC!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Huyu ndiye baadhi ya watu hudai kuwa ni waziri mchapakazi na kumpendekeza katika orodha ya watu wanaofaa kuwa rais? Kama wachapakazi ndio hawa, basi mimi najipeleka Gezaulole kufungua shamba la mihogo:alien:
 
Hizi ni kauli za mtu mwenye Ph.D.!! Aibu! Na inaonyesha hizo phd za UDSM ni za hovyo hovyo tu

Huu ni uthibitisho mwingine kuwa magamba wamechoka na wanahitaji kupumzishwa.hivi kwenye nchi ambayo siku zote tunalaani mauaji ya vizee vikongwe, hasa hasa wenye macho mekundu, kwenye kanda ya ziwa, tukiwaomba wananchi waache hizo imani potofu za uchawi, hadi kusababisha mauaji, sasa anajitokeza waziri mwenye heshima kubwa kama Magufuli, anatamka hadharani kuwa haogopi kulogwa! Hivi kiongozi mwingine atakapoenda kwa wananchi nakuwasihi waache imani za kishirikina, hivi wananchi hao wakimgeukia kiongozi huyo kuwa kaanze kwanza kumwambia Magufuli, hivi kiongozi huyo ataamrisha askari wa Mwema awalipue kwa mabomu, waliosema maneno hayo??!!
 
OMG THIS IS PATHETIC!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Huyu ndiye baadhi ya watu hudai kuwa ni waziri mchapakazi na kumpendekeza katika orodha ya watu wanaofaa kuwa rais? Kama wachapakazi ndio hawa, basi mimi najipeleka Gezaulole kufungua shamba la mihogo:alien:
Tena maneno hayo, ameyatamka huyo waziri msomi, anayajiita kuwa ana Ph.D, tena kwenye karne ya 21, ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia, sijui wananchi tutoe tafsiri gani kwa wasomi wetu wa nchi hii??!!
 
ALHAMISI, SEPTEMBA 20, 2012 06:32 NA GABRIEL MUSHI

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema ingawa majukumu ya wizara yake ni ya hatari na ya mateso, kamwe haogopi kurogwa. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Usafiri wa Haraka (BRT).

Dk. Magufuli aliyasema hayo mbele ya Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa akimzungumzia Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi, DART, Cosmas Takule, ambaye alisema ameshindwa kutimiza wajibu.

Alisema pia kwamba, kutokana na kutowajika kwa mkurugenzi huyo, kama angekuwa yuko chini yake angekuwa ameshamfukuza kazi.

“Mkurugenzi huyu anachelewesha kulipa fidia ili kumaliza migogoro inayoibuka kwenye miradi ya ujenzi jijini Dar es Salaam.

“Siwachongei kwako Mheshimiwa Rais, lakini DART wanatukwaza, kuna vituo viwili kati ya saba ambavyo huyu mkurugenzi alitakiwa kuwalipa fidia wakazi wanaoathiriwa na vituo hivyo lakini amechelewesha fidia hadi muda wa mkandari kuwapo eneo la kazi umekwisha na kitendo hiki kimetuingiza hasara sisi kwa kulazimika kumlipa mkandarasi huyo.

“Lakini kwa kuwa Waziri Hawa Ghasia yupo katika sherehe hizi, nadhani atalichukulia hatua kwa sababu suala la kulipa fidia na kushughulikia migogoro ya watu hao lipo chini yake kwa kupitia DART.

“Kazi hii ya ujenzi tunajua ni mateso, ni risk sana kwa sababu unapomsema mtu wakati anakuangalia anaweza kukuroga ukashangaa umeanguka chini ghafla.

“Kwa hiyo, nimeamua kumsema hapa huyu mkurugenzi mbele yako kwa sababu siogopi kulogwa, kwani hata kama akiniloga, kwa Jina la Yesu atashindwa tu,” alisema Dk. Magufuli.

Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete, asitishike na maneno machafu yanayotolewa na baadhi ya watu, badala yake aendelee na safari zake za nje ya nchi ili kuomba misaada zaidi kwa wafadhili.

“Tunahitaji marais wenye uwezo wa kuzungumza kizungu ili tuweze kupata misaada. Kwa mfano, hivi sasa Rais amezungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia na amekubali kutujengea barabara za juu pale Ubungo.

“Mheshimiwa Rais, endelea kusafiri kwa sababu hauwezi kukaa ndani kila wakati, kwani hata mwanaume ukikaa ndani tu mkeo atakuuliza, leo huendi hata kusalimia majirani?

“Kusafiri kwako ni sawa na mvuvi ambaye akitaka samaki lazima aende baharini au ziwani au ukimtaka mke lazima uende kwa mkwe.

“Usiogope kutukanwa kwa sababu ni jambo la kawaida kwa kiongozi, tena hii barabara ikikamilika wataomba kibali cha kuandamana humo humo,” alisema.

Kuhusu mradi huo, alisema ujenzi wa barabara hiyo itakayoanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni, itagharimu Sh bilioni 241.

“Fedha hizi kwa kiwango kikubwa zimetolewa kwa mkopo na Benki ya Dunia ambazo ni Dola za Marekani milioni 225.62 na zilizobakia Serikali yetu imezitoa.

Naye Rais Kikwete, alimtaka Dk. Magufuli kuacha kuendelea kutenga maeneo ya muda kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali kwa sababu ni hasara kwa Serikali.

“Kwa mfano hapa Jangwani lilikuwa ni eneo zuri la kucheza mpira, sasa watoto wetu sijui wataenda kucheza wapi, mwisho wa siku watakwenda kucheza michezo mingine kama kubeba dawa za kulevya.

“Lakini uliniambia hili eneo la Jangwani ni kituo cha muda kwa ajili ya mradi huu, sitaki kusikia tena hili suala la eneo la muda kwa sababu mnaitia hasara Serikali, haina maana kutumia gharama kujenga mahali halafu baadaye pavunjwe eti kwa sababu palikuwa kwa muda.

“Pia kwako Mkuu wa Mkoa, natoa muda wa wiki mbili mkamilishe suala la Kituo cha Ubungo, kile kituo kinatakiwa kuhamishwa kwa sababu kinahudumia mabasi 300 kwa siku, wakati mradi huu ukikamilika kutakuwa na mabasi mengine zaidi ya 180.

“Mabasi yote hayo hayawezi kukaa katika kituo hicho, hivyo wewe mkuu wa mkoa nakupa muda wa wiki moja ukae na DART na TANROADS mniletee majibu ya sehemu ya kudumu ya Kituo cha Ubungo,” alisema Rais Kikwete.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, alisema mradi wa ujenzi huo unatarajia kukamilika Machi 8 mwaka 2015 na kukabidhiwa rasmi Septemba 8 mwaka huo huo.

“Mradi huu utakuwa na vituo vikubwa vitano na vidogo 29, barabara hizo zinajengwa na mkandarasi mkuu kutoka Ujerumani kwa kupitia Kampuni ya Strabag kwa kushirikiana na Mkandarasi Mshauri kutoka Australia.

“Jambo kubwa linalotukwaza kutekelea mradi huu ni kitendo cha baadhi ya wakazi kufungulia maji machafu ya chooni kwenye barabara, pia baadhi ya mamlaka kama vile TANESCO na DAWASCO kutotoa miundombinu yao haraka kwenye maeneo ya ujenzi na changamoto nyingine ndogondogo,” alisema Mfugale.


Halafu namshauri huyu Mheshimiwa, namna alivyo mchapakazi, inabidi tumshauri aende kwa "BWANA YESU" ili awe na uhakika kabisa wa kuwa "ROGWA PROOF" halafu aendelee kuchapa kazi kwa uhakika zaidi pasipo wasiwasi wa kurogwa tena
 
Back
Top Bottom