Siogopi kulogwa: Dk. Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siogopi kulogwa: Dk. Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, SEPTEMBA 20, 2012 06:32 NA GABRIEL MUSHI

  WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema ingawa majukumu ya wizara yake ni ya hatari na ya mateso, kamwe haogopi kurogwa. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Usafiri wa Haraka (BRT).

  Dk. Magufuli aliyasema hayo mbele ya Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa akimzungumzia Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi, DART, Cosmas Takule, ambaye alisema ameshindwa kutimiza wajibu.

  Alisema pia kwamba, kutokana na kutowajika kwa mkurugenzi huyo, kama angekuwa yuko chini yake angekuwa ameshamfukuza kazi.

  “Mkurugenzi huyu anachelewesha kulipa fidia ili kumaliza migogoro inayoibuka kwenye miradi ya ujenzi jijini Dar es Salaam.

  “Siwachongei kwako Mheshimiwa Rais, lakini DART wanatukwaza, kuna vituo viwili kati ya saba ambavyo huyu mkurugenzi alitakiwa kuwalipa fidia wakazi wanaoathiriwa na vituo hivyo lakini amechelewesha fidia hadi muda wa mkandari kuwapo eneo la kazi umekwisha na kitendo hiki kimetuingiza hasara sisi kwa kulazimika kumlipa mkandarasi huyo.

  “Lakini kwa kuwa Waziri Hawa Ghasia yupo katika sherehe hizi, nadhani atalichukulia hatua kwa sababu suala la kulipa fidia na kushughulikia migogoro ya watu hao lipo chini yake kwa kupitia DART.

  “Kazi hii ya ujenzi tunajua ni mateso, ni risk sana kwa sababu unapomsema mtu wakati anakuangalia anaweza kukuroga ukashangaa umeanguka chini ghafla.

  “Kwa hiyo, nimeamua kumsema hapa huyu mkurugenzi mbele yako kwa sababu siogopi kulogwa, kwani hata kama akiniloga, kwa Jina la Yesu atashindwa tu,” alisema Dk. Magufuli.

  Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete, asitishike na maneno machafu yanayotolewa na baadhi ya watu, badala yake aendelee na safari zake za nje ya nchi ili kuomba misaada zaidi kwa wafadhili.

  “Tunahitaji marais wenye uwezo wa kuzungumza kizungu ili tuweze kupata misaada. Kwa mfano, hivi sasa Rais amezungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia na amekubali kutujengea barabara za juu pale Ubungo.

  “Mheshimiwa Rais, endelea kusafiri kwa sababu hauwezi kukaa ndani kila wakati, kwani hata mwanaume ukikaa ndani tu mkeo atakuuliza, leo huendi hata kusalimia majirani?

  “Kusafiri kwako ni sawa na mvuvi ambaye akitaka samaki lazima aende baharini au ziwani au ukimtaka mke lazima uende kwa mkwe.

  “Usiogope kutukanwa kwa sababu ni jambo la kawaida kwa kiongozi, tena hii barabara ikikamilika wataomba kibali cha kuandamana humo humo,” alisema.

  Kuhusu mradi huo, alisema ujenzi wa barabara hiyo itakayoanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni, itagharimu Sh bilioni 241.

  “Fedha hizi kwa kiwango kikubwa zimetolewa kwa mkopo na Benki ya Dunia ambazo ni Dola za Marekani milioni 225.62 na zilizobakia Serikali yetu imezitoa.

  Naye Rais Kikwete, alimtaka Dk. Magufuli kuacha kuendelea kutenga maeneo ya muda kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali kwa sababu ni hasara kwa Serikali.

  “Kwa mfano hapa Jangwani lilikuwa ni eneo zuri la kucheza mpira, sasa watoto wetu sijui wataenda kucheza wapi, mwisho wa siku watakwenda kucheza michezo mingine kama kubeba dawa za kulevya.

  “Lakini uliniambia hili eneo la Jangwani ni kituo cha muda kwa ajili ya mradi huu, sitaki kusikia tena hili suala la eneo la muda kwa sababu mnaitia hasara Serikali, haina maana kutumia gharama kujenga mahali halafu baadaye pavunjwe eti kwa sababu palikuwa kwa muda.

  “Pia kwako Mkuu wa Mkoa, natoa muda wa wiki mbili mkamilishe suala la Kituo cha Ubungo, kile kituo kinatakiwa kuhamishwa kwa sababu kinahudumia mabasi 300 kwa siku, wakati mradi huu ukikamilika kutakuwa na mabasi mengine zaidi ya 180.

  “Mabasi yote hayo hayawezi kukaa katika kituo hicho, hivyo wewe mkuu wa mkoa nakupa muda wa wiki moja ukae na DART na TANROADS mniletee majibu ya sehemu ya kudumu ya Kituo cha Ubungo,” alisema Rais Kikwete.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, alisema mradi wa ujenzi huo unatarajia kukamilika Machi 8 mwaka 2015 na kukabidhiwa rasmi Septemba 8 mwaka huo huo.

  “Mradi huu utakuwa na vituo vikubwa vitano na vidogo 29, barabara hizo zinajengwa na mkandarasi mkuu kutoka Ujerumani kwa kupitia Kampuni ya Strabag kwa kushirikiana na Mkandarasi Mshauri kutoka Australia.

  “Jambo kubwa linalotukwaza kutekelea mradi huu ni kitendo cha baadhi ya wakazi kufungulia maji machafu ya chooni kwenye barabara, pia baadhi ya mamlaka kama vile TANESCO na DAWASCO kutotoa miundombinu yao haraka kwenye maeneo ya ujenzi na changamoto nyingine ndogondogo,” alisema Mfugale.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Imani hizo toka kwa WAZIRI na Wakati Serikali inasema hakuna vitu kama hivyo?
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,177
  Likes Received: 12,883
  Trophy Points: 280
  huyu atakuwa mchawi
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Huyu waziri mwenye Imani za kichawi anatakiwa kufukuzwa Mara moja hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna usemi kuwa mchawi ukimsema kweupe hakulogi ngoo
  Naona Magufuri ameamua kuuapply huu msemo!
  Chukua tahadhari mwaya maana unawindwa sana na wabaya wako
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  duh...msgufuli nsyr katoa mpya ila binafsi namkubali sana huyu jamaa.........
   
 7. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes,kwa jina la Yesu!
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Bila shaka atakuwa anaamini katika ushirikina!!!!
   
 9. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,336
  Likes Received: 6,683
  Trophy Points: 280
  inakuwaje anajishuku namna hii!!
   
 10. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,336
  Likes Received: 6,683
  Trophy Points: 280
  na huenda anatembea na tunguli kiunoni!
   
 11. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  viongoz wengine hata hawajitambui,
  mi nahis alikuwa anatania manke ni aibu
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mchawi siku zote hushuku kila mtu ni mchawi
  kwa karne hii bad anaamini kulogwa badala ya kutenda kazi
  anajikosha tu huyu mbele ya JK kama juzi alivosema JK
  huwa anasafiri ili kuomba ufadhili na uwekezaji
  ufadhili wa nini wakati tumeachia madini yetu, mfauta na gesi yanachukuliwa tukiwachekea?
  Magufulu amefilisika sera
  hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  Mbona hakuitolea Kibondo, sumbawanga, pangani, singida au hata karagwe?
   
 14. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hizi ni kauli za mtu mwenye Ph.D.!! Aibu! Na inaonyesha hizo phd za UDSM ni za hovyo hovyo tu
   
 15. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hata Ikulu kuna kamati ya wachawi na wana posho kutoka kwa JK, mmeishayasahau ya kule bungeni? List ya viongozi wanaamini uchawi ni ndefu!
   
 16. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Aibu sana tanzania mtu msomi kiwango cha phd bado linamini kazi za kina majimarefu
   
 17. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  kazidi jikomba+kutaka sifa za akina Original comedy..Hajui wachina,Warusi huongea na marekani mambo yahusuyo usalama wa dunia kwa lugha zao?Watu wanaongelea Mabomu ya kuweza angamiza dunia chini ya dk 5, kwa zoezi linaweza rudia hata mara mia ktk hizo dkk 5.Yeti wanaelewana na dunia inakuwa salama.

  Hizi PhD za fasta ni taabu kwelikweli.
   
 18. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaha uwa ni mtu wa kujikomba kwa M.k.w.e.r.e siku zote,mtu msomi level ya phd unakua na kauli za ajabu namna hiyo?ana tofauti gani na layman anaeburuza mikokoteni?eti rais anaejua kiingereza,MANUFACTURING OF TEACHERS ndio kujua kiingereza sahihi?msomi una amini ushirikina tena katika zama za sayansi na teknolojia?no wonder ikulu inalindwa na kuongozwa kwa imani za kishirikina!anasifia kwenda nje kuomba, aibu gani hii??hakuona ile article jinsi Waingereza walivyomchambua na kumdharau kiongozi wetu mkuu?Magufuri ni bure kabisa,kujikomba na kuropoka kunamfanya azidi kujitia aibu na kua kichekesho tu
   
 19. h

  hans79 JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Mwenzake kamwambia unaitia hasara serikali kwa miradi ya muda mfupi na pia kamwambia ile sehemu ya kuchezea watoto,je hao watoto watacheza wapi?Hv jamani huwa pana kikao cha mawazir na mkiti ni jk,inakuwaje hadi waumbuane barabara?Na kwa nini hakumweleza jk kuwa pana uzembe hadi ayaseme barabarani?Kazi kwa sifa zitaleta matatizo,hii kweli serikali dhaifu.
   
 20. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inaelekea hyo jamaa anaempa za uso ndiyo zake kuroga wanaoingilia anga zake.
   
Loading...