Sio ufisadi ni urais ndiyo unaomfanya Lowasa achukiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio ufisadi ni urais ndiyo unaomfanya Lowasa achukiwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jun 13, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Jana Lowasa alikuwa amehudhuria ibada kwenye kanisa la kiroho SCOAN nchini Nigeria
  Nampongeza sana Mh. Lowasa kwa namna ambavyo ameonyesha dhahiri kuwa yeye ni mtu wa Mungu, kwa wanaomjua Lowasa watakubaliana nami kuwa mara nyingi amekuwa mstari wa mbele kwenye mambo ya Mungu, na hii ndiyo maana wakati wa uongozi wake alikuwa mchapakazi hodari na msimamizi mzuri wa shughuli za serikali kitu kilichosabababisha apate maadui wengi kwani watanzania wengi hawajazoea utamaduni wa kusukumwa wengi hufanya kazi kwa mazoea bila kuzingatia taratibu zilizowekwa. Uchapakazi wa Lowasa ulifanya amfunike rais, yeye alikuwa ndiyo tegemeo la mwisho la watanzania wapenda maendeleo, ndiyo maana kama sio Lowasa wimbo wa ukosefu wa shule kwa vijana wanaofaulu kwenda kidato cha kwanza ungekuwa unaendelea kuimbwa kwa kupokezana. Leo hii watu wamesahau kuwa ni juhudi binafsi za Lowasa ndiyo maana hilo la shule za kata lilifanikiwa, alipoondoka ameondoka nalo kwani viongozi wengine hawakuwa na maono. Baadhi ya watu wachache hujaribu kumchafua Lowasa ili achafuke mbele za watu wakiwa na hofu kuwa huenda akagombea urais mwaka 2015 ukweli ni kuwa mpaka sasa kwenye chama cha CCM hakuna mtu anayeweza kumshinda Lowasa linapokuja suala la Utendaji na uwajibikaji. Nilishangaa sana kuona kuwa kampuni iliyosababisha mheshimiwa Lowasa ajiuzuru imenunuliwa na wamarekani khaaaaa!!! si tuliambiwa ni ya kitapeli hata serikali isiiguse mitambo hiyo? mitambo hii tuliambiwa ni michakavu iweje leo ionekane mitambo hiyo niyamaana kwa nchi iliyopiga hatua katika medeni za viwango? ndiyo maana nijuavyo mimi tatizo la Lowasa kuchukiwa sio ufisadi bali ni urais maana kwa vyovyote nia ya wenzetu ni
  kuhakikisha mwenzao anapata urais hivyo kila atakae inuka kama sio mwenzao lazima ataondoshwa!!! Ingekuwa Lowasa ni mwenzao tusingesikia habari ya fisadi maana wanalindana ndiyo maana mwenzetu akifanya maandamano hatusikii tamko ila mwenzao akifanya ni ruksa. Nasikitika sana kwa wale wenzangu mimi ambao hawajui haya mambo!!!
   
 2. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  we na wewe tuondolee kampeni zako za kijinga hapa lowasa hata aende kuhiji maka haniingii akilini ng'oo bora kura yangu nimpe nguruwe japo mi ni muislam.
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Na mtu anayeutafuta urais kwa hali na mali muogopeni kama ukoma!
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Jifunze vitu muhimu katika uhandishi, kama nukta, herufi kubwa mwanzo wa sentensi, space kutenganisha line, comma, semmi collon na shift line.
  Ni hayo tu.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ni ajabu uchukiwe na watu wote kwa pamoja halafu udai wewe ni mtu safi. Either wote wana matatizo au wewe ndio tatizo. Wangelikuwa watu wawili au watatu hawakutaki tungelielewa EL ni mtu safi ila kama wananchi wengi hawamtaki akiwamo baba wa Taifa basi ufahamu tatizo ni Lowassa. apumzike tu urais ni bora nichukue kura yangu nichanechane nikae bar nikate kilaji kwani sitakubali kushiriki kumsimika Hosni Mubarak wa Tanzania.
   
 6. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Huyo Lowasa ni mnafiki, arudishe kwanza fedha zetu za RICHMOND and surender the big houses in London alizonunua kama uyoga na mtoto wake!!!!!!!!! Mungu si mnafiki kihivyo, hata aende kwa Pope record yake ni ya ovyo saana the man is so greedy, be carefull to fall in his antics. Msanii kama jamaa yake, nchi hii hahitaji wezi na wasanii, inahitaji wakombozi kutoka kwenye utumwa wa wana maghamba CCM wanaoendelea kufanya nchi masikini, USANII HAUTUPELEKI KOKOTE TUNAZIDI KUDIDIMIA!!!!!!
   
Loading...