Masha, Mkumbo, Mwigamba, Albert Msando na Katambi Mwenyekiti BAVICHA, wajiunga CCM

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
kata.jpg

Kutoka kushoto ni: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Bw. Patrobas Katambi, Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA Bw. Lawrence Masha, Aliyekuwa mwanachama mwandamizi wa ACT Wazalendo Bi. Edna sunga, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Samson Mwigamba na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo aliyekuwa kuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT Wazalendo.

CCM imesajili washambuliaji makini leo ambapo mbele ya mkutano wa NEC ya chama hicho waliokuwa viongozi wakubwa kabisa wa vyama vya upinzani wamejiunga CCM, nao ni Samson Mwigamba aliyekuwa katibu mkuu wa ACT, Kitila mkumbo aliyekuwa mshauri mkuu wa ACT na kabla ya hapo mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.

Naye Patrobas Katambi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa BAVICHA taifa ameamua kujiunga na chama cha mapinduzi mbele ya mkutano wa NEC.

Yumo Albert Msando mwanasheria mkuu wa ACT na mshauri wa sheria wa chama hicho. pia Lau masha kada wa CHADEMA.

Aliyosema Albert Msando

=> CCM ni chama ambacho mimi kama kijana sioni aibu kujihusisha nacho

=> Kipindi cha nyuma watu walikuwa wanaona aibu kusema wako CCM lakini sasa hivi ni ufahari.

=> CCM iliahidi kupapamba na ufisadi na rushwa na sasa hivi tunaona watu wanavyoshughulikiwa. Zamani taarifa zilikuwa zikitolewa watu hata hawafikishi polisi.

=> Nidhamu ya kazi imerudi pamoja na uwajibikaji na kila mtu natekeleza majukumu yake.

=> Ni mtu ambaye ni punguani ndio anaweza kupinga jitihada zinazofanyika.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha akiongea baada ya kukaribishwa

Kitila Mkumbo akikaribishwa CCM

Magufuli akisoma barua ya Sophia Simba

KWELI CCM INAZIDI KUIMARIKA.
 
=> CCM ni chama ambacho mimi kama kijana sioni aibu kujihusisha nacho

=> Kipindi cha nyuma watu walikuwa wanaona aibu kusema wako CCM lakini sasa hivi ni ufahari.

=> CCM iliahidi kupapamba na ufisadi na rushwa na sasa hivi tunaona watu wanavyoshughulikiwa. Zamani taarifa zilikuwa zikitolewa watu hata hawafikishi polisi.

=> Nidhamu ya kazi imerudi pamoja na uwajibikaji na kila mtu natekeleza majukumu yake.

=> Ni mtu ambaye ni punguani ndio anaweza kupinga jitihada zinazofanyika.
 
CCM imesajili washambuliaji makini leo ambapo mbele ya mkutano wa NEC ya chama hicho waliokuwa viongozi wakubwa kabisa wa vyama vya upinzani wamejiunga CCM, nao ni Samson Mwigamba aliyekuwa katibu mkuu wa ACT, Kitila mkumbo aliyekuwa mshauri mkuu wa ACT na kabla ya hapo mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Yumo Albert Msando mwanasheria mkuu wa ACT na mshauri wa sheria wa chama hicho. pia Lau masha kada wa CHADEMA.

KWELI CCM INAZIDI KUIMARIKA
hakuna mwanachadema hata mmoja apo
 
Back
Top Bottom