Sio sasa lakini Raisi ajaye atakuwa dikteta..

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Rasi ajaye atakuwa dikteta. Nchi yetu ikiendelea vizuri tusubiri Raisi ajaye ambaye atakuwa na nguvu za kuamua nani awe mbunge, kuteua na kuingilia mahakama, polisi ambayo iko juu ya madaraka na siyo ya wananchi. Biashara ndogondogo ambazo zitakuwa zinaenda kutokana na usifiaji wa serikali. Nchi ya watu waoga isiyo na uhuru wa vyombo vya habari. Kwa namna tunavyoenda hivi naomba kuwauliza watu wanaosifia sana bunge kutokuwa na nguvu na vyombo vya habari kutokuwa na uhuru.

Je tukipata Raisi ajaye mika iyajo ambaye si mzuri, mla rushwa, mkabila, mbinafsi na asije fanya vitu kwa manufaa ya nchi itakuwaje kama nguvu zote, vyombo vyote vya habari na wananchi wote hawana uhuru wa kuandamana, kutoa maoni tofauti, kukosoa, kwenda mahakamani na bunge duni? Hii ndiyo maana ni muhimu kuwa na system nzuri ya uongozi ambayo haitumii mtu. Tutaanza kuwa na Raisi wa maisha kama China! Wakati utamaduni wetu hauruhusu na unapenda demokrasia. China watu bilioni 1.3 wanachaguliwa wawe na watoto wangapi na serikali yaani mtu mmoja Raisi anauwezo wa kusema kuanzia kesho mnaweza kuwa na watoto au kama sasa hivi kulazimisha watu kutoa mimba bila kujali dini wala mila. Mnataka tuendehuko! Maana hiyo ni possibility kabisa sio kila dikteta atakuwa mzuri! Lakini mifumo ndiyo muhimu. Angalia US wana kichaa lakini nchi iko palepale
 
Back
Top Bottom