Sio Muhimbili na Mloganzila tu, hospitali zote za umma zimulikwe

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Habari iwe nanyi!

Nashukuru wazalendo wa taifa hili walioleta kero za hospitali zetu hasa MNH-Mloganzila, kwa kweli kuona tatizo kubwa kama hilo na kulisema ndiyo uzalendo wenyewe. Kukaa kimya huku mambo yanaharibikia tena ya kupoteza wapendwa wetu ni sawa na uhaini.
 
Naunga mkono kuwa tatizo ni kubwa sana kwenye hospitali za umma. Hakuna manpower ya kutosha. Unakuta kituo cha afya kina robo ya nguvu kazi inayotakiwa
 
kindikwili kwa sasa hicho sio kipaumbele chetu siasa ndio inayoharibu kila sekta nchi hii wanasiasa wanataka kupata sifa na unashangaa wananchi wenyewe wanashangilia juzi hapa yule mkuu wa kituo cha Afya huko Geita anaambiwa apige magoti, unawaza kwa utaratibu upi mtumishi apige magoti?Juzi hapa mwalimu anachapwa viboko watu wanashangilia hivi wanajua athari zake?

Leo sakata la Mloganzila limekuwa moto sababu watu wa JF wamekwenda kutibiwa hapo lakini ukweli ni kuwa WANASIASA KUTAKA SIFA ZA KUPATA UDIWANI, UBUNGE NA URAIS Leo wanafunzi wakipata alama C wanasiasa wanakuambia weka msawazo kwa kila mwanafunzi AAB au BBB ili tuwafurahishe wananchi huku ukweli ukiwa ni DDD au EEE matokeo yake ndio hayo tunayoyaona leo

Hizo Hospitali zote za serikali huduma ndio hizo hizo uwe Mwanza, Mtwara, Mbeya, Rukwa hapo suluhu ni kuwapeleka watu wakasomee nje ya nchi huo utaalamu wa hivyo vitendea kazi, pia maslahi ya watumishi wa serikali wote yaboreshwe huku mtaani tunaambiwa sasa ni mwaka wa sita hakuna nyongeza hakuna lolote zaidi ya watumishi kuwa watumwa kwenye nchi yao, lakini nachelea kusema Nani anaweza kuthubutu kuwajali watumishi?

Jibu naona ni kiza kinene,( kama hutaki kazi acha kazi haya ni majibu ya watanzania ambao wanataka MLONGANZILA iwe hai)
 
Sorry thread imejipost kabla sijamaliza ila , mimi ni shuhuda wa majibu ya hovyo ya madaktari na manasi wetu kwenye hospitali zetu za umma. Mwaka jana mke wangu akiwa na ujauzito wa miezi nane alipatwa na tatizo la kutokwa na damu akakimbizwa hospitalini nikiwa kazini muda huo (sitataja hospitali maana nitakuwa nimeji-expose sana) alipofikishwa madaktari waliokuwa zamu walimpokea vizuri sana na kwakweli akahudumiwa kwa haraka . Walimpiga ultrasound wakasema mtoto yuko hai ila kwenye zile process za kutaka kumuokoa mama na mtoto , bahati mbaya mtoto akafia tumboni.

Nilipofika tu nikaambiwa mama yupo ila kwa hali yake siwezi kumuona ila nikafuate vitenge na nguo halafu nifanye mpango wa kuchukua kile kiumbe. Nikaenda nyumbani ,kurudi nikawauliza kama naweza kupata huduma ya kumzika kile kiumbe pale hospitalini wakasema wao hawana makaburi lazima nichukue , hapo inakaribia saa kumi na mbili jioni. Nikamwambia nesi wa zamu kuwa anipe kipaumbele kuchukua kile kiumbe ili nikazike kabla jua jalijazama (maana mimi sijawahi kuona bindamu akizikwa usiku). Nesi akaniambia bado niko busy najaza fomu za wagonjwa wengine . Nikakaa nusu saa hapo ni saa 12 na nusu nikashindwa kuvumilia nikamuwakia akanipa kiumbe nikatoka.

Nilikaa siku MBILI sijamuona mke wangu kwamba siwezi kumuona maana yuko kwenye wodi ya wamama na hawezi kutembea kutoka nje. Wakati huo wazazi na ndugu zake na wazazi wangu wanapiga simu cha kuwajibu sina manesi hawataki nimuone. Siku ya tatu akafanikiwa kutoka nje, dah mke wangu alikuwa amevimba mwili mzima. Nilipomuuliza nesi kwanini amevimba vile ,nesi akanijibu unashangaa mkeo kuvimba hushangai abiria wanaosafiri kwenye magari wakivimba miguu. Nikamwambia huyu hajavimba miguu bali mwili mzima akaniambia kuvimba ni kawaida.

Nikaenda kwa madaktari kuwauliza kwanini amevimba vile mwili mzima na kwanini waliita ambulance kumpeleka hospitali nyingine kubwa baadaye wakasitisha. Yule dokta akaniambia kwanza wewe una elimu gani, nikamwambia darasa la saba akasema ungekuwa na degree ya udaktari ningekueleza. kwavile naishi shamba nilikuwa sionekani kama mtumishi au mtu mwenye elimu. Nikamwabia kwahiyo sisi la saba hatuna haki ya kujua shida za wagonjwa wetu ? akajibu kamtafute ndugu yako daktari nije nimpe maelezo ili akakuelezee huko ila mimi sina muda maana najua hutanielewa. Namshukuru Mungu alipona na nawashukuru madaktari na manesi wale wenye moyo kumpigania kwenye hatua za mwanzo Mungu awabariki sana

Dharau na uzembe wa baadhi ya madaktari huharibu sifa nzuri ya madaktari wengine na hospitali kwa ujumla. Mfano bila wale madaktari wa mwanzo huenda ningepoteza mke na mtoto ila kwa jitihada zao nilibaki na mke. Ila majibu ya madaktari na nesi niliowakuta baadaye na kunipa majibu hayo yalinivunja moyo sana. Serikali itambue kuwa watu wanasema haya hawana lengo la kukosoa juhudi za awamu ya tano au kukashifu haspitali zetu bali kuwahimiza wazidishe usimamizi na uendeshaji bora wa hospitali , jamani kumpoteza mke , mtoto, mume , baba ,mama au ndugu inauma sana ila hata kama anayefariki humjui ni lazima ikuume maana naye ni mtu na anategemewa na familia yake.
 
Habari iwe nanyi!

Nashukuru wazalendo wa taifa hili walioleta kero za hospitali zetu hasa MNH-Mloganzila, kwakweli kuona tatizo kubwa kama hilo na kulisema ndiyo uzalendo wenyewe. Kukaa kimya huku mambo yanaharibikia tena ya kupoteza wapendwa wetu ni sawa na uhaini.
Baada ya hapo achunguzwe waziri maana sizani kama ni dokta by profession, then tuhamie kwa rais mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hapa naandika ninikiwa na huzuni.Mdogo wangu amepoteza maisha Leo asubuhi huko mbeya et kwa tatizo la kuhara tu.Kaanza Jana kuumwa akapelekwa hospital ya mkoa Leo asubuhi wanaenda kumwona wakakuta amefariki.INASIKITISHA.

Sasa kuna mawili,
1.Huduma mbovu na kutojali wagonjwa.

2.Hakuna health facilities (Dawa) ktk hospitals zetu.
Lakini kuna kikundi cha watu kina ongea uongo kuwa kuna Dawa na Huduma ni nzuri na kuwa wanajali watumishi kwa kuwapa maslahi bora.

Mungu yupo tu atalipa.

Hainiingi akilini kimasihara tu dogo ametangulia mbele ya haki.lazima kuna tatizo lililotokea hospital.

R I P GLORY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAKI na MASLAHI ya mtumishi ni kitu MUHIMU sn.Watu wanakufa,watu wanajufa.Halafu haya maccm yanasema Tupo vizur, uwajibikaji mkubwa. Ni wapuuzi na anayewaongoza.Kuna watu wa kutowachezea
1.Madaktar

2.Walimu

Chunga sana.

Serikali haijajua tu mioyo ya hawa watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Inasikitisha sana! Imefikia hatua sasa hivi ukisikia mgonjwa kapelekwa Muloganzira ujue hatorudi akiwa hai.. mifano ninayo kwa ndugu, rafiki na majirani zangu.
 
Habari iwe nanyi!

Nashukuru wazalendo wa taifa hili walioleta kero za hospitali zetu hasa MNH-Mloganzila, kwa kweli kuona tatizo kubwa kama hilo na kulisema ndiyo uzalendo wenyewe. Kukaa kimya huku mambo yanaharibikia tena ya kupoteza wapendwa wetu ni sawa na uhaini.
Hata ndege tunazonunua tutakuja kulia tuu baadaye. Wakati Mlonganzila inajengwa na hata sasa design yake ni nzuri sana na imegharimu mabilioni kujenga. Lakini angalia UENDESHAJI wake sasa. Hospitali imegeuka kuwa KERO badala ya kuwa FARAJA kwa watu. Ndivyo ilivyo miradi mingi mikubwa ya nchi hii.
 
Huko iringa
Screenshot_20200107-151628~01.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hapa naandika ninikiwa na huzuni.Mdogo wangu amepoteza maisha Leo asubuhi huko mbeya et kwa tatizo la kuhara tu.Kaanza Jana kuumwa akapelekwa hospital ya mkoa Leo asubuhi wanaenda kumwona wakakuta amefariki.INASIKITISHA.

Sasa kuna mawili,
1.Huduma mbovu na kutojali wagonjwa.

2.Hakuna health facilities (Dawa) ktk hospitals zetu.
Lakini kuna kikundi cha watu kina ongea uongo kuwa kuna Dawa na Huduma ni nzuri na kuwa wanajali watumishi kwa kuwapa maslahi bora.

Mungu yupo tu atalipa.

Hainiingi akilini kimasihara tu dogo ametangulia mbele ya haki.lazima kuna tatizo lililotokea hospital.

R I P GLORY

Sent using Jamii Forums mobile app

Poleni sana kaka, ndoto za mdogo wetu umepotezwa na ugonjwa dhaifu sana hospitalini kama kuhara, kama kuhara kunamuua mtu hospitalini vipi magonjwa mengine? Inauma sana familia kumpoteza bini aliyekuwa na ndoto lukuki
 
kindikwili kwa sasa hicho sio kipaumbele chetu siasa ndio inayoharibu kila sekta nchi hii wanasiasa wanataka kupata sifa na unashangaa wananchi wenyewe wanashangilia juzi hapa yule mkuu wa kituo cha Afya huko Geita anaambiwa apige magoti, unawaza kwa utaratibu upi mtumishi apige magoti?Juzi hapa mwalimu anachapwa viboko watu wanashangilia hivi wanajua athari zake?

Leo sakata la Mloganzila limekuwa moto sababu watu wa JF wamekwenda kutibiwa hapo lakini ukweli ni kuwa WANASIASA KUTAKA SIFA ZA KUPATA UDIWANI, UBUNGE NA URAIS Leo wanafunzi wakipata alama C wanasiasa wanakuambia weka msawazo kwa kila mwanafunzi AAB au BBB ili tuwafurahishe wananchi huku ukweli ukiwa ni DDD au EEE matokeo yake ndio hayo tunayoyaona leo

Hizo Hospitali zote za serikali huduma ndio hizo hizo uwe Mwanza, Mtwara, Mbeya, Rukwa hapo suluhu ni kuwapeleka watu wakasomee nje ya nchi huo utaalamu wa hivyo vitendea kazi, pia maslahi ya watumishi wa serikali wote yaboreshwe huku mtaani tunaambiwa sasa ni mwaka wa sita hakuna nyongeza hakuna lolote zaidi ya watumishi kuwa watumwa kwenye nchi yao, lakini nachelea kusema Nani anaweza kuthubutu kuwajali watumishi?

Jibu naona ni kiza kinene,( kama hutaki kazi acha kazi haya ni majibu ya watanzania ambao wanataka MLONGANZILA iwe hai)
Hapa kazi tu . Mafanikio yanaonekana waziwazi, ndege, barabara stiglers gorge , hospitali za wilaya zaidi ya 60 vituo vya afya zaidi ya 250 n.k mnataka nini watanzania. tumuunge mkono raisi wetu hata ikibidi kufa tufe kwa ajili yake hata ikibidi kuzama baharini tuzame nae. Mbere kwa mbere. Nahisi nchi nzima tuna mtindio wa ubongo kwaa yanayoendelea
 
  • Thanks
Reactions: PNC
basi hao waliopo tuone wako serious. hospitali nyingi za serikali utawakuta wanapiga soga na kuchezea simu tu wakati kuna dharura.
Naunga mkono kuwa tatizo ni kubwa sana kwenye hospitali za umma. Hakuna manpower ya kutosha. Unakuta kituo cha afya kina robo ya nguvu kazi inayotakiwa
 
Poleni sana kaka, ndoto za mdogo wetu umepotezwa na ugonjwa dhaifu sana hospitalini kama kuhara, kama kuhara kunamuua mtu hospitalini vipi magonjwa mengine? Inauma sana familia kumpoteza bini aliyekuwa na ndoto lukuki
Pole Sana inaumiza mno
 
Duh!Umeandika kwa unyenyekevu sana.Mungu akubariki mkuu
Sorry thread imejipost kabla sijamaliza ila , mimi ni shuhuda wa majibu ya hovyo ya madaktari na manasi wetu kwenye hospitali zetu za umma. Mwaka jana mke wangu akiwa na ujauzito wa miezi nane alipatwa na tatizo la kutokwa na damu akakimbizwa hospitalini nikiwa kazini muda huo (sitataja hospitali maana nitakuwa nimeji-expose sana) alipofikishwa madaktari waliokuwa zamu walimpokea vizuri sana na kwakweli akahudumiwa kwa haraka . Walimpiga ultrasound wakasema mtoto yuko hai ila kwenye zile process za kutaka kumuokoa mama na mtoto , bahati mbaya mtoto akafia tumboni.

Nilipofika tu nikaambiwa mama yupo ila kwa hali yake siwezi kumuona ila nikafuate vitenge na nguo halafu nifanye mpango wa kuchukua kile kiumbe. Nikaenda nyumbani ,kurudi nikawauliza kama naweza kupata huduma ya kumzika kile kiumbe pale hospitalini wakasema wao hawana makaburi lazima nichukue , hapo inakaribia saa kumi na mbili jioni. Nikamwambia nesi wa zamu kuwa anipe kipaumbele kuchukua kile kiumbe ili nikazike kabla jua jalijazama (maana mimi sijawahi kuona bindamu akizikwa usiku). Nesi akaniambia bado niko busy najaza fomu za wagonjwa wengine . Nikakaa nusu saa hapo ni saa 12 na nusu nikashindwa kuvumilia nikamuwakia akanipa kiumbe nikatoka.

Nilikaa siku MBILI sijamuona mke wangu kwamba siwezi kumuona maana yuko kwenye wodi ya wamama na hawezi kutembea kutoka nje. Wakati huo wazazi na ndugu zake na wazazi wangu wanapiga simu cha kuwajibu sina manesi hawataki nimuone. Siku ya tatu akafanikiwa kutoka nje, dah mke wangu alikuwa amevimba mwili mzima. Nilipomuuliza nesi kwanini amevimba vile ,nesi akanijibu unashangaa mkeo kuvimba hushangai abiria wanaosafiri kwenye magari wakivimba miguu. Nikamwambia huyu hajavimba miguu bali mwili mzima akaniambia kuvimba ni kawaida.

Nikaenda kwa madaktari kuwauliza kwanini amevimba vile mwili mzima na kwanini waliita ambulance kumpeleka hospitali nyingine kubwa baadaye wakasitisha. Yule dokta akaniambia kwanza wewe una elimu gani, nikamwambia darasa la saba akasema ungekuwa na degree ya udaktari ningekueleza. kwavile naishi shamba nilikuwa sionekani kama mtumishi au mtu mwenye elimu. Nikamwabia kwahiyo sisi la saba hatuna haki ya kujua shida za wagonjwa wetu ? akajibu kamtafute ndugu yako daktari nije nimpe maelezo ili akakuelezee huko ila mimi sina muda maana najua hutanielewa. Namshukuru Mungu alipona na nawashukuru madaktari na manesi wale wenye moyo kumpigania kwenye hatua za mwanzo Mungu awabariki sana

Dharau na uzembe wa baadhi ya madaktari huharibu sifa nzuri ya madaktari wengine na hospitali kwa ujumla. Mfano bila wale madaktari wa mwanzo huenda ningepoteza mke na mtoto ila kwa jitihada zao nilibaki na mke. Ila majibu ya madaktari na nesi niliowakuta baadaye na kunipa majibu hayo yalinivunja moyo sana. Serikali itambue kuwa watu wanasema haya hawana lengo la kukosoa juhudi za awamu ya tano au kukashifu haspitali zetu bali kuwahimiza wazidishe usimamizi na uendeshaji bora wa hospitali , jamani kumpoteza mke , mtoto, mume , baba ,mama au ndugu inauma sana ila hata kama anayefariki humjui ni lazima ikuume maana naye ni mtu na anategemewa na familia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna uzembe mkubwa hospital za umma unaweza kuleta mgonjwa daktari akakimbia akabaki kuhudumiwa na nesi mgonjwa akishafariki daktari ndio anajitokeza kuandika ripoti hii fani inaelekea imevamiwa ni vema zoezi la uhakiki lianze kwa hawa watu na wajue walikuwa wanapata maksi gani sio kubebwa kwa sababu sasa hivi tuna vyuo vingi vya kusomea udaktari wanapewa udokta
 
basi hao waliopo tuone wako serious. hospitali nyingi za serikali utawakuta wanapiga soga na kuchezea simu tu wakati kuna dharura.
Kama mzigo wa kazi ni mkubwa na maslahi duni unategemea nini mkuu, sina uhakika ule mgomo mkubwa wa madaktari changamoto zao zilishughulikiwa
 
Back
Top Bottom