Sio mabasi ya mwendokasi ni daladala tu, maana yanapanga foleni

G-ManiaX

Member
Jan 8, 2017
14
2
Haina maana kuita Mabasi ya MwendoKasi hali ya kua hayapewi kipaumbele katika junction za barabara.

Unakuta mabasi ya MwendoKasi 10 yamepanga foleni yanasubiri askari usalama aruhusu magari mengine kwanza yapite kisha ndo mruhusiwe nyinyi.

Haina maana sasa ya kulipia 650 bora upande daladala kwa 400 ambayo inakwenda mahala hapo hapo inapokwenda mabasi ya mwendo kasi na itawahi kufika hiyo daladala. Lengo la mwendo kasi linapuuziwa kabisa.
 
Kwahiyo sisi wenye magari yetu tusiruhusiwe kwasababu umelipa hiyo 650 yako?

Unajua mafuta tunayotumia kwenda kwenye shughuli zetu sisi wenye magari binafsi?

Ni zamu kwa zamu. Kama unaharaka sana amka mapema au panda bodaboda huwa hazikai foleni.
 
Safi sana kwa michango yenu kumbuka hili ni jukwa huru la kutoa michango ya mawazo. Kama gari hata mimi ninalo ninapaki ferry nikivuka naingia MwendoKasi. Kwanza napunguza msongamano pia na-save. So issue is not kua na gari issue ni uhalisia wa BRT
 
mwendokasi yakiwa kumi yanasubiri kuachiwa katika junction yatapita yote haraka,lakini kwa msongamano wa barabara ya kawaida wenye zaidi ya madari 50 gari ako ikiwa nyuma sana utasubiri sana mana unaweza uchukue dakika kadhaa mpaka itakapofika zamu yako kuweza kupita lets say kama ni pale mataa ubungo.
 
Mkuu hoja yako nimeielewa. Ila point ni ile priority, mfano mzuri ntakupa katika junction ya Morogoro rd na Samora Ave, hua kuna askari akiyaona anazuia magari mara moja, likipita anaendelea kuyaruhusu magari kama kawaida. Hata dk haiishi kuliacha Bus kupita. Na hata kama taa hakuna utaratibu ile bus ipite kabla we hujaingia barabarani. Kuna makutano mengine ya barabara askari anayalundika mabasi yake huku na kule ukiyahesabu 10 yanafika. Maono yangu mimi ukiyaacha yapita hata dakika 1 haziishi kwani hayana foleni kuyazuia mpaka yazibe barabara kama magari mengine unayaruhusu mpaka huko yanapoenda hayaendi tena na kubakia msongamano. Ndo hapo unakuta lengo sio Kasi tu bali kupunguza msongamano mjini, hata pia kuokoa nishati, muda pia kutunza.
 
mi nadhani kwa baadhi ya sehemu kama hiyo uloitaja possible,ila sehemu kama mataa ubungo pale huwezi kusimamisha gari za barabara ya kawaida ghafla ili kuruhusu mwendoksi apite,ni vigumu kwa sababu huwa yanakuwa mengi na kwa speed kubwa.so kuna baadhi ya sehemu na wao pia wanakuwa kama daladala tuu.
 
Kwahiyo sisi wenye magari yetu tusiruhusiwe kwasababu umelipa hiyo 650 yako?

Unajua mafuta tunayotumia kwenda kwenye shughuli zetu sisi wenye magari binafsi?

Ni zamu kwa zamu. Kama unaharaka sana amka mapema au panda bodaboda huwa hazikai foleni.
Sikutegemea kukuta umeandika hivyo ila mwenyenguvu mpishe mimi nimekupisha wewe MWENYE GARI.
 
Umeona mkuu, watu labda wanafikiri wanaopanda mwendokasi hawajielewi au hawana funguo. Utakuta gari kumi za watu binafsi zimepanga foleni kila gari ina mtu mmoja moja yani dereva halafu bus moja watu zaidi ya 60 kwani hao wehu mpaka wote kujumuika wanakoenda mahala pamoja. Mfano mzuri wa kuchukua kama watu wanajitambua vzr, mnaweza mkawa wote mnamagari na mnaishi katika sehemu mmoja, mnaweza mkaji-organize wote mnachangia mafuta kwa gari mojawapo inayobeba watu wengi mnakuja nayo mjini inawaacha kisha jioni mnakusanyana mnarudi majumbani kwenu. Huku magari yenu mmeyaacha majumbani. Same concept applies for BRT
 
Back
Top Bottom