Sio lazima iwe miaka kumi hata mitano inatosha

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Ifike mahala watanzania tuwe na mitazamo ya kuona mbali, ikiwa ndani ya miaka mitano hali Ni mbaya kwa kiwango hiki vipi kama itakuja mingine Kama hii?

Tunaambiwa kuwa uchumi wetu unazidi kupanda lakini kiukweli sivyo, hebu tutizame hali ya wananchi ilivyo imefikia kuwa katika familia nyingi Sana hapa nchini wengi wanaishi kwa kula mlo mmoja kutwa.

Biashara ndogo ndogo zilizokuwa zikiwasaidia hawa wanyonge sasa haziendi kutwa nzima akina mama wanazunguka na mabeseni ya mboga mboga, matunda, nyanya na hakuna hata mnunuzi, hii inaonyesha wazi kuwa mizunguko wa hela haupo Tena kwa wananchi.

Hebu angalia mishahara kwa watumishi haijaongezwa kwa miaka mitano na ukweli ni kwamba ndani ya hiyo miaka mitano familia hizo nazo zimeongezeka hivyo kupelekea matumizi ndani ya familia kuongezeka.

Unawezaje kujisifu kuwa uchumi ni mzuri wakati unazidi kuwapa wananchi umaskini kwa kiwango Cha Hali ya juu?

Ajira hakuna watoto Wana maliza masomo iwe ni sekondari hata vyuo wanarudi Tena kwa wazazi wao ambao walitumia hela zao nyingi kuwasomesha.

Yako mengi ambayo tukiyatazama kwa jicho la tatu, tutaamua kwa pamoja kwamba hii mitano inatosha kwa CCM, iondoke na waje wengine huwenda tukapata Neema.
 
Kama maamuzi ya wapiga kura yangekuwa yanapewa uzito kwenye sanduku la kura hilo la miaka mitano lingewezekana kabisa, tatizo maamuzi ya wapiga kura nchi hii hayaheshimiwi, ukimchagua mwingine wao watamuweka wanaemtaka wao kwa wizi wa kura.
 
Back
Top Bottom