Sio LAZIMA CCM ITAWALE, Ni vita ya ukombozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio LAZIMA CCM ITAWALE, Ni vita ya ukombozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jun 25, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kuna watu kila mara wanapopata fursa ya kufikiria wao hufikiria namna watakavyoshindwa kufikiri. Hali hii imetusababishia kushindwa na kushindwa kwenye sekta mbalimbali, leo hii mtanzania anaweza jisifu kwenye sekta ipi? uchumi mfumko wa bei 20%, utamaduni ndo umetushinda kabisa, uwekezaji-upi kwa fedha kidogo ya kitanzania hii, michezo aibu na kashfa visingizio kila kona-msumbiji tumetolewa, simba licha ya 3-0 wakatolewa, twiga pamoja na mazuri ugenini wakapigwa home, yanga ndo imekufa siku mingi sana kimataifa.

  Siasa ndo za maji taka -ukisema ukweli kwenye siasa utajutia, siasa tume ya uchaguzi inateuliwa na mgombea mmojawapo ambaye ni dhaifu, refa anateuliwa na mchezaji mmojawapo harafu anashangilia ushindi wakati wenzake wanalalamika mipira mingi inapigwa kifaulo faulo hivi, anatabasamu naendelea na kugombea, siasa bila maendeleo, utulivu na amani vimekuwa kitu kimoja, umasikini sio adui tena wa maendeleo ni nyenzo muhimu kwa mafsaidi kutuibia rasilimali za nchi, elimu duni hadi aibu, shule za kata ni taka za leshu, vyuoni ni vituko tupu, hebu chukulia SAUT & CBE hadi utawala unatoa agizo ni marufuku wasichana/wanawake kuvaa nguzo fupi inayovuka magoti, suruali za kubana n.k,

  Je hawa wamama wanafuata taaluma au kitu kingine? Hivi mwanafunzi wa chuo kikuu anahitaji kuambiwa kuhusu mavazi ndio ajirekebishe? Ndo maana mababu zetu walisema kumpeleka mtoto wa kike shule kunaambatana na kumfaunza umalaya!!!! badala ya kuwaprove wrong, sasa tunawaprove correct!!! watoto class7 hawajui kusoma wala kuandika, wala kuhesabu. TUMESHINDWA KILA SEKTA.

  Nyerere alipotoka madarakani alionesha kwa vitendo kuwa serikali bila yeye itakuwepo, alipotoka kwenye uongozi wa CCM alionesha kwa vitendo bila yeye CCM itakuwepo, kwanini CCM isioneshe kwa vitendo bila ccm Tanzania
  itakuwepo??

  Siasa ya vyama vingi bila kubadilisha vyama kwenye uongozi wa nchi ni hatari sana, ni hatari kuliko siasa ya chama kimoja. Kama demokrasia inaishia kwenye kupigia kura zaidi ya mtu mmoja bila kubadilisha watawala demokrasia hiyo sio angavu wala haina tija kwa mwananchi. Si mnaona enzi za chama kimoja angalau kulikuweko na kina G55 Njeru Kasaka etc, ina maana hawa kina njeru siku hizi hawapo ndani ya CCM, au demokrasia imezima nyota hizi kung'ara??

  Vitu vingi tumevikosea kwa kudhani bila CCM nchi hatakuwepo, uchumi na siasa zitakoma, hapana hata kidogo. CCM sharti ipite ili mapambazuko mapya yaonekane. Tusifikirie kushindwa kwa upinzani kuongoza serikali mara baada ya kuingia serikalini, la hata kidogo, tufikirie maendeleo na uchumi kwa mtanzania utakavyopata mawazo na masukumo mpya. Hebu firkiria nyerere na TANU ya miaka 7 tu alipata uhuru, leo CDM, CUF au NCCR mageuzi washindwe kuongoza nchi kwa misingi ipi? udhaifu wa kutpkuweza kufikiria nje ya CCM utatuangamiza, mbaya zaidi sisi na wajukuu wetu.

  Deni la taifa linakuwa bila maelezo kuwa tunakopa ili kufanya nini? Mtu anatuambia tusiogope deni kukua mama meghji na wenzake, sijui kama bado wanaakili za kuongoza watanzania. suala sio deni yes, lakini suala ni tulikopa kufanya nini? USA kama deni ni kubwa unaona walichokifanya duniani hapa, Japani na wengine hakika unaona deni lilifanya nini.

  Je Watanzania Trilioni 22, zimekopwa kiasi gani wakati wa Kikwete?? zaidi ya trilion 15, ambayo kwa msingi ni bajeti ya taifa, sasa kama tumekopa mafedha yote hayo tumefanya nini??? mbona shirika la ndge limekufa, mbona reli hakuna, mbona meli hatuna, mbona barabara hatuna, mbona nyumba bora hatuna, mbona elimu bora hatuna, mbona siasa safi hatuna, mbona kila kitu hatuna???? NAOMBA KUPITIA hoja hii deni la taifa liainishwe lini na wapi na nani kakopa, kafanya nini? kwa faida ya nani?

  Vinginevyo CCM tuseme basi, Kikwete ni vema kupumzika kwa amani huko msoga, kama utamind mwanza, kapumzike lakini hali ni mbaya kila mtanzania hata mawaziri wako wanalalamika japo kila siku mko wote kwenye vikao, wabunge wanalalamika, diwani wanalalamika, wanaCCM ndo wako hoi maana wamezoea siasa za kura rushwa ndo wajenge wanunue magari, mgombea asipojitambulisha kwa wajumbe imekula kwake.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Unadhani CCM hilo wanalielewa ni wewe na mimi tutakapo amuwa kwamba wanaweza kukaa benchi na nchi ikabaki kama ilivyo na ikawa na maendeleo zaidi
   
Loading...