Chrizant Kibogoyo
Senior Member
- Aug 12, 2016
- 159
- 81
Kwa niaba ya Kamati ya Waathirika wa Bomoabomoa ya barabara ya Morogoro nachukua nafasi hii kuweka kumbukumbu sahihi dhidi ya upotoshaji mkubwa uliofanywa Na kikundi cha "CHADEMA IN BLOOD" kuwa Mhe John Mnyika Mbunge Jimbo ka Kibamba amefanikiwa kuwaokoa waathirika kupitia zuio la Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.
Ili kuweka kumbukumbu sahihi Kesi husika ilifunguliwa na baadhi ya waathirika wapatao 500 na zaidi kidogo siku nyingi hata kabla ya TANROADS kuanza kutoa notisi za ubomoaji. Mhe Mnyika amekuja kujua kuhusu kufunguliwa kwa shauri hili na tarehe ya kusikilizwa kwa maombi ya walalamikaji baada ya notisi kuanza kutolewa tar 2 Mei 2017. Hivyo sio sahihi hata kidogo kwa MTU mzima mwenye akili zake timamu kutoa madai kuwa Mbunge ndio amewaokoa waathirika hawa.
Hadi sasa waathirika waliofungua kesi wamepambana na changamoto kibao ikiwemo ukosefu wa raslimali za kufungua kesi husika. Lakini hatukuwahi kupata msaada wowote kufanikisha hatua hii ya ufunguaji kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutoka viongozi wa kuchaguliwa ikiwemo Mbunge, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa n.k wanaojifagilia kupitia kuwa mitandao ya kijamii kuwa ndio wakombozi.
Nichukue fursa hii kuwakumbusha wote wanaojifagilia kutusaidia kuwa hili suala ni la kijamii na si la kisiasa. Hivyo tunawaomba wanasiasa wote wasiokuwa na maadili mema wajiweke kando na shughuli zetu kama ambavyo walijiweka kando baada ya Mhe John Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi kumjibu Mhe John Mnyika kuwa "kama anataka barabara iwe na upana wa rula".
Kutokea hapo mbunge wetu alimuogopa Waziri wa Ujenzi Na akaamua kututekekeza waathirika wa bomoabomoa hii licha ya ukweli kwamba alikuwa na muda uwezo wa kutusaidia kupitia nafasi yake ya ubunge.
Niwatake wanasiasa wote wasiokuwa na utu wajiweke pembeni na mchakato huu wetu sasa kwa kuwa tuliwapatia nafasi ya kutosha kulishughulikia na wakashindwa.
Wanachofanya wanasiasa tuliowachagua ni kutumia mafuta yetu kutukaanga ili tutakapoiva washiriki kalamu ya kututafuna katika kualikwa uwekaji majiwe ya msingi, uzinduzi n.k
Sisi waathirika bado tuna imani na mhimili wa mahakama kutupatia haki yetu.
Aidha bado tuna imani Na wadau mbali mbali wenye nia njema ikiwemo vyama vya siasa vilivyoamua kuweka wazi mustakabali wake wa kujisahihisha na kujirekebisha na kuachana na utapeli wa kisiasa kama unaofanyika katika suala hili la bomoa bomo basdhi ya wsnasiada, kutaka kujipatia umaarufu wa kisiasa kupitia maafa, gharika Na shida za waathirika wa bomoa bomoa hii.
Kamati ya waathirika inachukua fursa hii kuwakumbusha wadau wote kuwa katika suala hili zitajitokeza athari kubwa sana za kijamii, kiuchumi n.k. Hivyo wadau wote wenye nia njema kutoa misaada ya ukweli wanaakikwa. Ikiwemo wale wanaojijua kuwa ndio walihusika kutunga na kuiagiza serikaki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekekekeza Operesheni Vijiji vya Ujamaa. Operesheni ambayo ndio chanzo cha hii bomoa bomoa.