Sio kila ombaomba anahitaji msaada- be careful

tete'a'tete

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
472
62
Natumaini kwa uwezo wa Mungu mko wazima,

Leo kwenye misa ya asubuhi kanisani Azania Front mchungaji aliyekuwa anahubiri katufunulia siri nyingi sana za sheteni nakutupa shuhuda mbalimbali jinsi shetani anavyofanya kazi.

Moja ya ushuhuda wake ni kisa kilichotokea hivi karibuni hapa Dar es salaam. Napenda nikushirikishe ili uchukue hatua.

Pale salender Bridge ambapo anasimama trafiki akivuta magari, kuna mdada alikuwa ndani ya gari lake kwenye foleni akisubiri zamu yake ya kuruhusiwa na trafiki ifike apite. ndipo aliposogea kaka mmoja ombaomba, akasogea kwenye gari la yule dada na kuomba msaada.

Dada huyo kwa kumhurumia akamsaidia. Alipompa pesa tu mkono wa yule dada ukaota manyoya ya paka, akachanganyikiwa alipokuwa anaendelea kushangaa trafiki akawa anaruhusu magari ya upande wake yule dada akawa hawezi kuendesha gari, ndipo trafiki akamsogelea na kuuliza kulikoni?!

Yule dada akatoa mkono wake na kumuonyesha trafiki na kumsimulia kilichotokea na bahati nzuri yule kaka aliepewa pesa alikuwa mita chache pembeni anamuangalia yule dada. Ikabidi trafiki aende kumuuliza yule ombaomba kulikoni?

Ndipo yule ombaomba akamwambia trafiki kuwa yule dada akimbusu tu atapona mkono utarudi kawaida. Basi ikabidi yule dada atelemke aende kumbusu yule kaka, alivyombusu wakapotea wote palepale, gari ya yule dada ikabaki barabarani ndipo trafiki alipoita watu wakaanza kuisukuma ile gari na kuiweka pembeni.

Kuna dada mwingine alikuwepo leo kanisani baada ya ibada akawa anatusimulia, yeye alikuwa nyuma ya gari ya huyo dada alishuhudia hilo tukio anasema ni tukio la kweli kabisa ameshuhudia kwa macho yake.

Hivyo jamani nawatahadharisha ndugu zangu mlio na moyo wa huruma msipende kutoa pesa zenu hovyo sababu umekutana na maskini.

Biblia inasema maskini wapo na wataendelea kuwepo, mwombe Mungu kwanza kila unapotaka kutoa sadaka yako. Mwenye Masikio na Asikie
 
Mmmh hii kali.,na imekatishiwa patamu kweli, sasa walivyopotea walienda wapi?.,kwa kuwa ni ngumu sana kumtofautisha genuine ombaomba na huyo mzee wa busara nimeazimia kuanzia sasa sitoi tena senti zangu kwa ombaomba kudadadeki.
 
OMG!!!! we ndugu wewe simulizi hili umelisikia mwenyewe toka kwa shuhuda??

so scary!!
 
Amen,eeeeeh mbn naogopa jamani!plz it should be a joke au?duh inatisha jamani
 
Mhh! I don't believe it, mleta mada hebu tueleze ameshuhudia ibada ya wapi? I mean kanisa gani
 
yaani ndo uligungiwa na huyo mzenji mpaka leo!!! duh umefaidi

asante kwa kunipa pole na ile barabara sipit tena as of today

misd you Masa ......

Teh teh teh nilifikiri wewe ndo ulipotezwa na omba omba....nilisoma vibaya! bado nina hangover za Valentine
 
Sitashangaa kama hii habari ya kusadikika umesikia kwa Pastor Hammer pale ubungo kwa ufufuo wa misukule.
 
OMG!!!! we ndugu wewe simulizi hili umelisikia mwenyewe toka kwa shuhuda??

so scary!!
teh teh matonya akijua hii mada atajiunga hapa aje akanushe,huyu jamaa anawaharibia watu kula yao hapa.
 
Teh teh teh nilifikiri wewe ndo ulipotezwa na omba omba....nilisoma vibaya! bado nina hangover za Valentine

hahaaa jamani wewe hebu yanipishie mbali hayo madua yako mabaya, huyo ombaomba alikuwa anatafuta mwanamke huyo sio pesa......

kweli hizo ni hangover za Valentine day!!! hata ku aknoleji kadi nlokutumia??? mmh haya weee!!
 
hahaaa jamani wewe hebu yanipishie mbali hayo madua yako mabaya, huyo ombaomba alikuwa anatafuta mwanamke huyo sio pesa......

kweli hizo ni hangover za Valentine day!!! hata ku aknoleji kadi nlokutumia??? mmh haya weee!!

Hahaha hahahah nilipata nyingi bwana, nikiifikia ya kwako kwenye que nita acknowledge Kizenj!
 
Hahaha hahahah nilipata nyingi bwana, nikiifikia ya kwako kwenye que nita acknowledge Kizenj!

makubwa sas wa bi wadogo si tutakuwa wengi sana??

ngoja tukutafutuie dawa yako nawewe tukuoteshe manyoya ya sungura
 
Kama ni kweli si mchezo,vitu vya ajabu..Binafsi siamini!!
Mchungaji anaitwa nani huyo aliyeleta ushuhuda?
 
Back
Top Bottom