Sio kila mfanyabiashara ni Mfanyabiashara,Chagua mtu sahihi wa kumshirikisha mawazo yako

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,935
22,919
Unajua kuna watu huwa nawakutaga wanasema mimi mpira wa BONGO siangaliii kabisa,ukimuuliza kwanini haangaliii Atakupa sababu za ajabu ajabu tena za kijinga jinga zisizo hata na maana yeyote Huwa nawambia watu wa namna hiyo kuwa "nyie mpira sio fani yenu na wala haupo kwenye damu" hivyo visingizio vyenu ni blah blah tu ambazo kamwe siwezi zielewa maana ukitaka

Kujua wapenda mpira wa ukweli wale wenye mpira wao kwenye damu,ukimkata na wembe damu yke inachuruzika vimipira vidogo vidogo Yeye hata iwe ndondo cup,asikie watoto wa mtaani, asikie mbuzi cup,asikie chochote kinachohusiana na mpira Utampiga utamuua ila lazima Aende kushangaaa na kuangalia haijalishi mpira unachezewa juu ya mawe,haijalishi mpira ni wa makaratasi,haijalishi refayupoje,ilimradi huo mchezo unaitwa "Mpira wa Miguuu" lazima utamuona eneo la tukio.Wael wengine wapenda premier League sjui laliga (tuachane nao)

Nimeanza na mfano mrefu kidogo ila sasa point yangu iko hapa,katika biashara Kuna wafanyabiashara dam dam na kuna wafanyabiashara Fata upepo,kuna wale wafanyabiashara yeye anafanya biashara kwasababu baba/mama/ndugu anafanya biashara au kwasababu ana mtaji tu wa biashara,Hawa wafanya biashara kisa wana mitaji tu ya biashara flani kwa sasa hivi ndio tunao wengi ktk jamiii kuliko wale wafanya biashara Dam Dam.

Hawa wafanyabiashara wenye mitaji ndio ma ninja/komandoo wa kukatisha wengine tamaa kuhusu biashara flani au kitu flani walichowahi kukifanya kabla halafu kikawabumia au wakatoka kapa bila kuambulia faida yyte.Wafanyabiashara hawa kwa kua biashara si asili yao wao wapo kwenye biashara kupata FaidA TU LKN HAWAFANYI BIASHARA KAMA passion iliyo ndani mwao.

Inapotokea sasa kafungua/anzisha biashara halafu ika dead kifo cha mende,Baadae ukaenda mfata ukamuomba ushauri kuhusu biashara ile ile aliyo feli asee atakuvunja moyo,maini,firigisi yani atakusaga saga kama lile limashine la kushindilia udongo huko road,kamwe hatoruhusu uifanye hiyo biashara.

Yeye ktk biashara yeyote anaamini "PESA" ndio kila kitu,ikatokea ukamwambia nataka nifungue Mama ntilie,nina mtaji wa laki 3 Kwanza kabla hajakwambia kitu atakuuliza mara mbili mbili hivi umesema una laki 3 au milioni 3? maana yake hiyo laki 3 yko kwa hesabu zake ni hela ya Vijiko TU yani yeye mawazo yake ukimwambia mama ntilie "anavuta picha haraka haraka ya classic mama ntilie anaemjua town"

Hata siku moja hanaga Kumpa moyo mtu mwenye mtaji mdogo afanye kile alichokitaka kwa mtaji wake ule ule,Hawa ni wazee wapeperusha mawazo ya wenzao.Hawa hata siku moja hatokaa akwambie kwanini yeye anakwambia usifanye biashara flani,yeye alifeli wapi? Muulize yeye alipofeli Hatokaa akwambie hata siku 1 n wazee wakujiekea self defence eneo hilo point atakazokushukia yani huwezi kukumbuka hata kumuuliza hilo swali wanajiita ma EXPERT wa hiyo business unayotaka kuifanya wewe sasa hivi.

Umeshawahi kukutana na ninja/komando anakwambia "Mimi kilimo sifanyi bora niokote makopo" tena nilime nyanya mimi au mpunga,nk nk,Yule mwingine anakwambia yani mimi Biashara ya Pesa sjui tigo pesa/mpesa/takataka za namna hiyo kuliko nifanye hiyo biashara bora nikagawe hela yangu au

Ushawahi kukutana na mtu anakwambia Mimi Forex shubaaamit sifanyi huo upupu Nishaifanya sana utaniambia nn kuhusu forex mimi, au Kuna wale wengine anakwambia mimi kuku wa kisasa kufuga sifanyi huo ujinga huniambii kitu kuhusu kuku wa kisasa, au mwingine anakwambia kuliko ununue Boda Boda umpe mtu alete hesabu Bora hela yako ukanunue TOTOZ upge one night stand.

Utamsikia mtu anakwambia Mimi biashara za ONLINE sifanyi n bora nilale nipate Afya nijue moja,nknk yani Hawa ma ninja/komando wana list nyingi sana za biashara ambazo wamezifanya zikawapiga kubung kabang,sasa usijiloge ukawaomba ushauri kuhusu hizo biashara,Utajuta. Kasoro yao 1 kubwa "hawa kwa kua pesa wanazo,ni mabingwa wa kuiga idea za wengine.Kuwa makini nao.

Halafu Upande huu mwingine sasa Kuna wale wafanya biashara wengine ambao ukimkata damu yake,damu inayotoka ni majina ya biashara tu,kuuza mishkaki,mahindi,pweza,duka la nguo,showrooms,nk nk yani hawa watu bwana biashara ndio uwanja wao wa nyumbani "msamiati wa Kushindwa hawana" kama unataka kuanza biashara au kuwa na rafiki mfanya biashara nakushauri tafuta aina ya wafanyabiashara kama hawa,ukitaka ushauri wafate hawa

Ukitaka kujua chakufanya wafate hawa na ukitaka wajua hawa n rahisi sana,Unaweza ukawa unataka ushauri wa biashara ambayo yeye aliifanya akafeli,Ukimfata huyu mfanyabiashara tuseme unataka kununua boda boda yeye alishanunuaga zikaibiwa zote,ila wakati anakushauri kwanza utamsikia akikupongeza kwa kuweza kujua Hela Ilipo,kisha utaanza msikia akikwambia Nini ufanye ili upate faida ili usiibiwe boda boda zako

Yani ataangalia loop holes zake huko nyuma halafu atakwambia wewe ili utakapoingia isitokee ukaanguka kama yeye,na mara nyingi hawa watu wakati mnapga story utamskia akikwambia,Yani ikatokea mtu akanipa 5M ntaenda kutungua BOXER mbili zote nawapa mkataba watu,yani anakwambia hvyo kukuonyesha hata yeye soon akipata pesa

Atakuja kufanya tena hiyo biashara pamoja na kwamba alifeli/alifelishwa,hawa n wafanyabiashara ambae akikwambia Kitu flani usifanye kweli usifanye,na mara nyingi ya vitu ambavyo hawawezi kukushauri ufanye ni Biashara Haramu tu,hawa wafanyabiashara hamna biashara atakwambia eti usifanye,labda tu hatokushauri ufanye kutokana na hali yako/familia yako/majukumu yako/nk nk

Chagua Mtu sahihi wa kumuomba ushauri ktk kile unachotaka/tamani kukifanya ktk biashara,sio kila mfanyabiashara ni Mfanyabiashara wengine wanafanya biashara kwasababu wana pesa za kufanya hizo biashara.
 
Ulichokisema ni sahihi kabisa.

Kuna wengine ni roho mbaya tu za kiswahili na ubinafsi.

Kuna jamaa huku analima sana UFUTA ( Na huwa anapata sana ), basi akikuona na wewe unataka kulima - anaponda sana kilimo.

Atakwambia, Kilimo hiki hakifai, ni kazi mbaya sana na haina maslahi kabisa.

Wakati huo huo yeye HAACHI na analima kila MWAKA.
 
Mtu anakwambia kilimo ni upumbavu siwezi kupoteza mda wangu kwenye kilimo kisa alilima msimu mmoja akapata hasara,
Alafu ukigeuka nyuma unaona kuna mamia ya watu wametoboa kupitia kilimo
 
Watu hawapendi wengine wafanikiwe mkuu yani kuna

mijitu hii dunia ina roho flani hata ya shetan afadhali.
 
Mtu anakwambia kilimo ni upumbavu siwezi kupoteza mda wangu kwenye kilimo kisa alilima msimu mmoja akapata hasara,
Alafu ukigeuka nyuma unaona kuna mamia ya watu wametoboa kupitia kilimo
Mkuu tena usiombe ukakutana na mtu wa namna hiyo,ningekua naweza

mtag hapa ningekutagia mmoja,yupo humu namfahamu Ukimtajia kilimo tu

utamsikia u expert wake sekta hiyo,yani ukimaliza mskiliza Na ukaweza kuingia

ktk kilimo basi wewe utakua ni shindikana wa mwisho mjini,anajua katsha watu tamaa sjawah ona.
 
Humu jf Kuna mmama mmoja hivi anapenda sana kukatisha watu tamaa anajifanyaga kuponda kila biashara
 
Simply:
Research ni hatua kuelekea kufanya biashara. Unapokutana na MTU akakueleza negative za ile biashara note,then endelea kukusanya data utakutana wengine wakueleze positive za hiyo biashara.
Then utapitia research yako uamue kufanya au kutokufanya.

Kila MTU anachokieleza huwa ni sahihi. Kwan kila biashara wapo waliofanikiwa kupitia hiyo biashara. Na wapo waliofeli kupitia hiyo biashara.

Tatizo LA watu wengi wanaotafuta ushauri wa Biashara. Akiona MTU amefanikiwa, akili yake inaamini ni ile biashara anayoifanya ndo imempatia mafanikio. Unapompatia ushauri tofauti na matarajio yake anaona hautaki afanikiwe.

Unawezaje kumwambia MTU biashara ni nzuri wakati imekupatia hasara zaidi ya Mara 2/3?. Means you have experienced the negative side of that business.

Contradiction
Mzungumzaji anaamini anasema ukweli
Msikilizaji anaamini anadanganywa.

MTU akifuata ushauri mwambie kama umeona inalipa kafanye full stop

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tena usiombe ukakutana na mtu wa namna hiyo,ningekua naweza

mtag hapa ningekutagia mmoja,yupo humu namfahamu Ukimtajia kilimo tu

utamsikia u expert wake sekta hiyo,yani ukimaliza mskiliza Na ukaweza kuingia

ktk kilimo basi wewe utakua ni shindikana wa mwisho mjini,anajua katsha watu tamaa sjawah ona.
mtaje mkuu tumjue
 
Simply:
Research ni hatua kuelekea kufanya biashara. Unapokutana na MTU akakueleza negative za ile biashara note,then endelea kukusanya data utakutana wengine wakueleze positive za hiyo biashara.
Then utapitia research yako uamue kufanya au kutokufanya.

Kila MTU anachokieleza huwa ni sahihi. Kwan kila biashara wapo waliofanikiwa kupitia hiyo biashara. Na wapo waliofeli kupitia hiyo biashara.

Tatizo LA watu wengi wanaotafuta ushauri wa Biashara. Akiona MTU amefanikiwa, akili yake inaamini ni ile biashara anayoifanya ndo imempatia mafanikio. Unapompatia ushauri tofauti na matarajio yake anaona hautaki afanikiwe.

Unawezaje kumwambia MTU biashara ni nzuri wakati imekupatia hasara zaidi ya Mara 2/3. Means you have experienced the negative side of that business.

Contradiction
Mzungumzaji anaamini anasema ukweli
Msikilizaji anaamini anadanganywa.

MTU akifuata ushauri mwambie kama umeona inalipa kafanye full stop

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemaliza kila kitu hapo ndio unakuja ule usemi "Akili za kuambiwa changanya na zako"
 
Umemaliza kila kitu hapo ndio unakuja ule usemi "Akili za kuambiwa changanya na zako"
Haujawahi kuambiwa kitu na mtu hadi ukaona akili zako

hazifai kuzichanganya na zile ulizoambiwa maana za kuambiwa

ni tamu na nzuri mara laki 5 ya akili zako,haijawahi kuku kuta hyo eh?
 
Back
Top Bottom