Salaam wakuu,
Wakati mikoa mingi nchini ikiendelea kupata mvua ya kutosha, kwa wengine imekuwa neema kwao kwani sasa wanaweza kuvuna maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na hata mazao.
Sasa kwa matumizi ya nyumbani ni pamoja na kuyatumia kwa kunywa bila kuyafanyia treatment yoyote. Tokea nakua kumekuwa na kasumba na kuaminishana kuwa maji ya mvua ni bora kwa kunywa. Mvua ikinyesha tumekuwa tukiyakinga na kunywa moja kwa moja bila kujua madhara yake
Pamoja na kubeba vimelea vingi na kila aina ya takataka, pia kuna aina ya madini maji hayo hukosa kwa ajili ya afya ya binadamu.
Pia kuna jamii zinaamini kuwa maji ya mvua yanatibu magonjwa mbalimbali.
Maji ya mvua yanaweza kuwa safi lakini siyo salama.

- Tunachokijua
- Maji ni kitu muhimu kwenye maisha ya viumbehai, na karibia 60% ya mwili wa binadamu huundwa kwayo.
Hivyo, mwili wa binadamu hutoa maji kupitia takamwili zake kama vile jasho na mkojo na kunywa maji ya kutosha kila siku husaidia kuboresha afya ya mwili pamoja na kufidia kiasi kingine kinachopotea.
Vyanzo vya maji
Vyanzo vya maji ni jumla ya maeneo yote ambayo maji huanzia hapo kabla ya kusafiri Kwenda sehemu nyinginezo. Kwa mfano Mito, Maziwa, Visima, Chemichemi, Mabwawa nk. Kimsingi maji ndio kiini cha uhai wa viumbe hai vyote vilivyopo duniani. Iwe ni Binadamu, Wanyama na Mimea, vyote haviwezi kuishi bila ya uwepo wa maji safi na salama.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaliwa aina tofauti tofauti za vyanzo vya maji, ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, nk. na huyatumia maji haya kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu pamoja na shughuli za kiuchumi.
Usalama wa maji ya mvua
Kukusanya na kutumia maji ya mvua inaweza kuwa njia nzuri ya kuhifadhi rasilimali. Watu wengine hutumia maji ya mvua kumwagilia mimea, kusafisha, kuoga, au kunywa. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa mfumo wa ukusanyaji maji ya mvua unadumishwa ipasavyo ili kutunza ubora wa maji kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa.
Ingawa ni muhimu kwa vitu vingi, maji ya mvua yanaweza yasiwe safi kama watu wengi wanavyofikiria, hivyo sio kila wakati hufaa kwa kunywa. Mvua inaweza kubeba aina tofauti za uchafu ndani ya maji unayokusanya (kwa mfano, kinyesi cha ndege kwenye paa lako kinaweza kuishia kwenye pipa lako la maji au tanki). Yanaweza kubeba bakteria, virusi pamoja na kemikali zingine zinazoweza kuwa hatari kwa afya yako.
Hatari ya kupata magonjwa kutokana na maji ya mvua inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo lako, ni mara ngapi mvua inanyesha, msimu na jinsi unavyokusanya na kuhifadhi maji ya mvua. Vumbi, moshi na chembechembe kutoka angani zinaweza kuchafua maji ya mvua kabla ya kutua juu ya paa lako.
Hivyo, madai ya kuwa sio kila maji ya mvua ni salama yana ukweli.
Jikinge na magonjwa
Ili kupunguza hatari ya kuugua, zingatia kutumia maji ya mvua kwa matumizi tu kama vile kumwagilia mimea au kuosha vitu ambavyo havitumiki kwa kupikia au kula. Epuka kutumia maji ya mvua kwa ajili ya kunywa, kupikia, kupiga mswaki, au kuosha au mimea ambayo unakusudia kula.
Ikiwa una mfumo wa kinga dhaifu, unapaswa kuwa mwangalifu hasa wakati wa kuchagua chanzo chako cha maji ya kunywa.
Hata hivyo, sio maji yote ya mvua ni mabaya. Ikiwa umejiridhisha kuwa maji husika ni masafi unaweza kuyatumia kwenye shughuli zote zinazokuhusu, ikiwemo kunywa.