Sio kila mabadiliko ni maendeleo, Watanzania tunaenda kuwa masikini kwa pamoja - collective poverty!

unapoilinganisha USA na Tz huon kama unatukosea sana?unaijua per capita ya mu USA na mtz?think big
No siyo kweli;

Nimi nilipomaliza form six ajira yangu ya kwanza za kwenye kampuni ya kibrazili ya Cears (sikumbuki jina sawasawa) iliyokuwa inajenga barabara ya lami kutoka Morogoro kwenda Dodoma tukiwa pale Dumila- Nimesoma kuwa Brazili wametusamehe deni la ujenzi wa barabara ile. Kwa vile tulikuwa tunaishi nje ya mji, kila weekend tulikuwa tunakwenda either Mororogo au Dodoma kwenda kutumia pesa zetu ambazo zilikuwa zinaingia kwenye uchumi. Baada ya kutoka Dumila nilihamia Morogoro kwenye kampuni ya kikanada iliyokuwa inajenga Mindu Dam (nayo sikumbuki jina lake leo). Mwishoni nikaishia kufanya kazi kwenye kampuni iliyokuwa inajenga kiwanda cha magunia hapo Morogoro kwenye ile Industrial park ya Morogoro wakati huo kabla sijaenda "Varsity." Hiyo miradi ilisababisha mji wa Morogogo uwe vibrant economically kwani wafanyakazi wa makapuni hayo walikuwa wanaingiza pesa nyingi sana mitaani, na wale akina mama waliokuwa wanatupikia lunch (mama ntilie) walikuwa na stable income siku zote, na siwezi kujua nao walikuwa wanasupport familia za ukubwa gani nyuma yao.

Hiyo ndiyo maana ya miradi ya miundombunu kwenye uchumi wa taifa. Usitegemee kuwa serikali itatoa pesa kuwapa watu kama mgao wa bure. Hata marekani wanaposema kujenga miundo mbinu ingawa miundo mbinu yao ni mizuri sana kuliko yetu, nia yao ni kuweka pesa kwenye mzunguko kiuchumi cha njia hiyo,.
 
Nani kakwambia kuwa wanataka kukawiwa chakula na serikali, serikali inatakiwa itengeneneze mazingira ili mwananchi atafute chakula akipate
Kama haikutengeneza hayo mazingira?
 
Pole sana...
Unajaribu kutabiri...
Umeona mahali naiomba serikali iniwekee pesa mfukoni ndio unaijibia bila shaka!!
Nilitumbuliwa ukiwa unashuhudia bila shaka, usijipe kazi ya kupiga ramli ukahisi kila unaemdhania ni mpiga porojo kama ulivyo, niletee wanao niwaajiri ujifunze kuheshimu usiowafahamu wakati mwingine.....
Chapa kazi wewe wacha porojo. Hakuna serukali itakueekea pesa mfukoni.

Mliotumbuliwa mnajionesha wazi wazi.
 
Miradi mingi mikubwa haikwepeki. Angeiahirisha JPM huyo mwingine anayefuata angelazimika kuitekeleza.

Sasa ndiyo tunaishi ile theory ya opportunity cost, unayo mfukoni noti ya shilingi elfu kumi, ni maamuzi yake uinywe bia yote au ukishinde kiu chako ili hiyo noti ikufae.
 
Unamzungumzia anaefanya kazi tena ofisi ina water dispenser kuwa vyuma vimemkazia?
Sijaelewa hapa nyumbu mie
Ile water dispenser ipo pale imewekwa na kampuni? Kwani gharama ya kununua maji makubwa ya elfu 6 kila baada ya siku 2 au 3,kwa kampuni yenye ofisi Samora avenue wewe unaona ni big deal? Hata kampuni yangu ya kuchomelea huku mkoani nimeweka water dispenser, tena kuna sukari na kahawa wakihitaji!
 
Analipwa mshahara kama alivokuwa akilipwa hapo kando halafu vyuma vimemkazia anapiga pasi ndefu?
Kuna tatizo mahali
Kisha jifunze kuelewa kabla hujakurupuka....
 
Awamu hii ya uongozi imejitahidi kugusa kila mfumo katika maisha ya jamii kwa jamii za aina zote kwa nia tu ya kutaka mabadiliko wakiamini kila mabadiliko ni maendeleo.

Hivyo mzunguko wa fedha umepunguzwa, kilimo kimeguswa, biashara zimeguswa, ajira zimeguswa,CAG ameguswa, deni la taifa limeguswq n.k
Ukiangalia vyote vilivyoguswa lengo limekuwa moja tu, kufyonza chochote kitakachoonekana ili kutekeleza miradi inayoitwa 'ya maendeleo'.

Matokeo yake ni kuwa jamii imejikuta na mifumo ya maisha ambayo sio rafiki kwao na mzunguko kidogo sana wa fedha kwenye uchumi usiotosheleza biashara nyingi kujiendesha kwa 'kujikimu'.

Wazoefu wa biashara wameamua kufunga biashara na kuhifadhi mtaji kidogo uliobaki mpaka mawimbi yatakapotulia.
Ambao hawana njia mbadala wamelaimika kuendelea na biashara huku wakila mtaji kidogo kidogo maana hamna namna!

Ukiangalia jamii kwa jicho la uerevu utaona maisha tuliyozoea yanaenda kukwama kwa wakati mmoja.
Serikali inatekeleza miradi mingi isiyokuwa na hakika ya kufanikiwa na hata ile yenye dalili za kufanikiwa sio ya kuleta matunda yanayoonekana katika kizazi hichi, siongelei kijacho maana sijui hata kama kitazaliwa!

Jamii kubwa imekosa matumaini. Hakuna hatari kama jamii kukosa matumaini. Jamii inayokosa matumaini haijaribu tena, haioni fursa, haijali, haifanyi kwa maslahi maana haioni kesho yake!

Sijui kama kuna mtu mmoja kwenye Serikali hii anajua tofauti ya mabadiliko na maendeleo. Sijui kama kuna mtu anaejua kuwa hata hayo mabadiliko yanahitaji maandalizi ya hatua kwa hatua!
Pumba tupu...
Mibavicha inatokota kwenye mafuta
 
Nalisha tumbo langu na familia yangu jamaa na rafiki kwa kiasi chake
Wengine wote nitawatumia kufikia lengo mama hata wewe ukijipendekeza nitakunyonya sana tu .
Hata Mo na Bahresa wanafanya hivo
Yes! Kila binadam anafanya chochote kwa maslahi yake kwanza
 
Kwenye basic needs wewe unatumia hierarchy ya nani?
Unachagua daraja badala ya chakula halafu unaita practice ya opportunity cost.
Kwako wewe scale of preference ni concept inayoeleweka kweli?
Unajua juu ya marginal propensity to spend?

Wewe ni mchumi wa wapi kwanza?
Miradi mingi mikubwa haikwepeki. Angeiahirisha JPM huyo mwingine anayefuata angelazimika kuitekeleza.

Sasa ndiyo tunaishi ile theory ya opportunity cost, unayo mfukoni noti ya shilingi elfu kumi, ni maamuzi yake uinywe bia yote au ukishinde kiu chako ili hiyo noti ikufae.
 
Mkuu kama kila mabadiliko sio maendeleo, ningependa kujua kati ya mabadiliko yote mnayoyahubiri wapinzani yapi ni maendeleo na yapi sio, au yote mnayoyahubiri ni maendeleo??
 
Ukitaka kuongelea mabadiliko wanayohubiri wapinzani, fungua uzi wake tuyaongelee!
Mimi naongelea uchumi unaoenda kukwama!

Kawaida, miradi ya maendeleo inategemea ukuaji wa uchumi kama factor mojawapo.
Sasa ukuaji wa uchumi haupo ila inayosemekana ni miradi ya maendeleo ndio inayoshika kasi!
Maana yake ni kuwa, fedha ambazo zingetumika kama kichocheo cha kukuza ajira ndizo zinazonunua ndege na fedha ambazo zingetumika kuongeza mzunguko wa fedha ndio zinazojenga reli.

Jamii zinashindwa kukidhi mahitaji ya msingi. Ng'ombe ambayo ingeuzwa buchani siku moja inauzwa siku tatu. Maana yake ni kuwa ;kodi ya bucha, mpimaji, mahitaji ya kujikimu, umeme, n.k yanakuwa mara tatu kwa ng'ombe yule yule mmoja.
Hapo hauoni mtaji unakufa?

Mara hii umeshasahau hata kichwa Cha mada yako.

Basi tusaidie, hayo mabadiliko mnayoyasema nyie wapinzani ni katika nini hasa???

Au nyie hamtafanya miradi ya miundombinu?? Mtaajiri tu, maana hapa umezungumzia ajira pekee??
 
Kwenye basic needs wewe unatumia hierarchy ya nani?
Unachagua daraja badala ya chakula halafu unaita practice ya opportunity cost.
Kwako wewe scale of preference ni concept inayoeleweka kweli?
Unajua juu ya marginal propensity to spend?

Wewe ni mchumi wa wapi kwanza?
Mapovu hayasaidii mkuu. Usikariri maisha, nenda na uhalisia wa dunia.

Obama alipokuja Afrika alitushauri tufanye biashara sisi kwa sisi.

Utafanyaje biashara na nchi zinazokunguka bila ya kuwa na miundo mbinu rafiki kwa biashara?.
 
Back
Top Bottom