Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,240
- 9,527
Awamu hii ya uongozi imejitahidi kugusa kila mfumo katika maisha ya jamii kwa jamii za aina zote kwa nia tu ya kutaka mabadiliko wakiamini kila mabadiliko ni maendeleo.
Hivyo mzunguko wa fedha umepunguzwa, kilimo kimeguswa, biashara zimeguswa, ajira zimeguswa,CAG ameguswa, deni la taifa limeguswq n.k
Ukiangalia vyote vilivyoguswa lengo limekuwa moja tu, kufyonza chochote kitakachoonekana ili kutekeleza miradi inayoitwa 'ya maendeleo'.
Matokeo yake ni kuwa jamii imejikuta na mifumo ya maisha ambayo sio rafiki kwao na mzunguko kidogo sana wa fedha kwenye uchumi usiotosheleza biashara nyingi kujiendesha kwa 'kujikimu'.
Wazoefu wa biashara wameamua kufunga biashara na kuhifadhi mtaji kidogo uliobaki mpaka mawimbi yatakapotulia.
Ambao hawana njia mbadala wamelaimika kuendelea na biashara huku wakila mtaji kidogo kidogo maana hamna namna!
Ukiangalia jamii kwa jicho la uerevu utaona maisha tuliyozoea yanaenda kukwama kwa wakati mmoja.
Serikali inatekeleza miradi mingi isiyokuwa na hakika ya kufanikiwa na hata ile yenye dalili za kufanikiwa sio ya kuleta matunda yanayoonekana katika kizazi hichi, siongelei kijacho maana sijui hata kama kitazaliwa!
Jamii kubwa imekosa matumaini. Hakuna hatari kama jamii kukosa matumaini. Jamii inayokosa matumaini haijaribu tena, haioni fursa, haijali, haifanyi kwa maslahi maana haioni kesho yake!
Sijui kama kuna mtu mmoja kwenye Serikali hii anajua tofauti ya mabadiliko na maendeleo. Sijui kama kuna mtu anaejua kuwa hata hayo mabadiliko yanahitaji maandalizi ya hatua kwa hatua!