Sio kila baya linalokutokea lina lengo la kukuumiza

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
Hadithi Hadithiii..

Kulikuwa na mvuvi mmoja kwa bahati mbaya akiwa kwenye kazi yake ya kuvua basi boti yake ilizama. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kuogelea na kufika kwenye kisiwa kimoja kilicho kuwa karibu na sehemu ambapo boti yake ilizama.

Basi siku zikazidi kwenda na kwa bahati mbaya hakuna mtu aliyejua kuwa yupo kwenye hiko kisiwa. Akawa amejizoelea maisha yake na akafanikiwa kujijengea kibanda chake.

Baada ya miezi kupita, msimu wa baridi ukaanza, akawa amewasha moto wake ili apate joto. Kwa bahati mbaya ule moto ukatapakaa na kuunguza kibanda chake.

Yule mvuvi alisikitika sana, na kumlaumu Mungu kwanini anampitisha kwenye shida. Kulikuwa na meli inapita, ikaona moshi mkubwa, basi wakaamini kutakuwa na uwepo wa binadamu katika kisiwa hiko na kwa bahati nzuri ikamkuta na kumrudisha nyumbani kwake.

Point of the story ni kwamba.

Kuna muda unaweza pitia tabu flani bila kujua kuwa mapito yako ndio yatakayokuletea neema katika maisha.

Usiwe mwepesi kulaumu, kulalamika, jitahidi kushukuru kwa kila jambo.

Karibuni kutoa mifano kuhusu changamoto ambazo umepitia kwenye maisha ambazo mwisho wake ukawa mzuri kwako.

#lifechallenges #changamotozamaisha #swahili
 
Tunaleteana stori za uongo na ukweli hapo umezungumzia matatizo ambayo yamesababishwa na nature kidogo unaweza ukasema mh.
Lakn ambayo yanasababishwa na binadamu wanaotuzunguka kwa makusudi napo unataka utaje jina la Mungu au ww unaonaje hapo
 
Kuna watu kunyimwa connection za kazi na ndugu zao ndio zimewasababisha wao kuwa wafanyabiashara wakubwa sana leo hii
 
Kwa hiyo Mungu ndio alisababisha wanyimwe connection ili wawe wafanyabiashara wakubwa
hahahhaa point ni kwamba tujifunze tu kushukuru mbeleni everything might make sense, japo ilo swala la watu kuwa na roho mbayAa lipo tu ni kama ndugu zake Yusuph
 
hahahhaa point ni kwamba tujifunze tu kushukuru mbeleni everything might make sense, japo ilo swala la watu kuwa na roho mbayAa lipo tu ni kama ndugu zake Yusuph
Acha uzwazwa wewe kwa hiyo kwa sababu Yusuph ndugu zake walikuwa na roho mbaya ndo watu wawe na roho mbaya.... mm ninachoona hamna cha kushukuru hapo yaani mtu akikufanyia ubaya na wewe unamfanyia zaidi.....acheni kuitumia Biblia vibaya kwa uelewa mdogo
 
Nahisi kuna watu hawajaelewa huu uzi, sijasema kuwa watu wawe na roho mbaya au tu embrace watu kufanya ubaya.
Sema kwenye msafara wa mamba basi na kenge nao hawawezi kukosekana.
Nimeongelea swala la situation kwenye maisha wakati zinakukuta zilikuweka kwenye situation mbaya ukawa stressed, depressed. ukahisi bora hata ufe or something similar lakini miaka mbeleni kutokana na ile situation ikabadilisha maisha yako na kuwa jambo jema. Wanasema what does not kill you makes you stronger, point ni tu encourage each other ambao wanapitia situation mbaya wajue ipo siku yatapita, wajitahidi kuwa na positive attitude ili ku overcome what ever they are going through.
Kulaumu, kuwa mkatili, kulipa ubaya haisaidii, ila ku walk away na kuamua kuwaza nje ya box itakusaidia kuona nuru .
Mfano mdogo, kuna wadada nilisoma nao walishindwa kuendelea na shule kwasababu ya kupata ujauzito wakiwa shule, kwa mda ule walihisi aibu, kufeli maisha nk lakini wakakubaliana wakabahatika kujifungua salama, wakapambana na biashara zao, sasahivi watoto wao ni wakubwa, wameoelewa, wana biashara zao na wapo proud kwa vitu walivyo accomplish.
Simaanishi tu support watoto wakike kupata mimba wakiwa wadogo, ila point yangu ni kwamba this too shall pass and tomorrow is a beautiful day. Kuliko kumkatisha mtu tamaa, na kumfaya ajisikie kama failure au mpaka afikie kujiua.
Wenye akili, hekima na busara naamini watanielewa na wamenielewa.
 
Back
Top Bottom