Sio jambo zuri kumpiga Mwanamke ila muda mwingine Wanawake wanakera mno

Jana nimeshuhudia Jirani yangu kampiga mke wake kwa nyundo hadi kumjeruhi vubaya sana maeneo ya kichwani halafu kaondoka na kutuachia sisi tushughulikie matibabu. Sasa kama wanandoa mkishakuwa hamjishushi mtaishia kuuana au kupeana vilema. Mimi nimeshakuwa kwenye ndoa kwa mwaka wa saba hatujawahi pigana wala kurushiana matusi hii yote inatoka na kujishusha kwetu tunapokoseana na ni wepesi kuombana msamaha hata kama hujakosea ili mwenzio ajionje. Mwisho ushauri wangu ukiona mmeanza kupigana achaneni maana kifuatacho mmoja wenu atakuja kutumia shoka kuadhibu mwingine na baadaye itabaki kuwa hadithi

Kila mtu na aseme "Aameen"

Abusers hawa huanza pole pole. Leo kofi. Kesho ngumi, vichwa na mateke. Halafu fimbo. Baada ya hapo ni cho chote kilicho mbele yake iwe nyundo, msumeno, mapanga etc.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom