Sio haki suala la Muungano kujadiliwa na watu 2 wa chama kimoja na mmoja kujifanya Bosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio haki suala la Muungano kujadiliwa na watu 2 wa chama kimoja na mmoja kujifanya Bosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Nov 13, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Wz,bar tukatae Masuala ya Muungano kuamuliwa na watu 2 tu,Jk na Shein huku Shein akiwa Jk ni Bosi wake na mwenyekiti wake wa chama.[/h]Written by amini // 13/11/2011 // Habari // No comments

  [​IMG][​IMG]WAZIRI NA RAISI WAKE(MWENYEKITI WAKE WA CHAMA)

  Ndugu zangu wana wa Zanzibar kuna hatari kubwa mbeleni kama hatukukakamaa na kukataa hivi vitimbi wanavyo tufanyia watanganyika wakishirikiana na Wanafiki(walafi0 wasio wazalendo Zanzibar kuitowa Zanzibar kwa mlongo wa nyuma.
  katika katiba mpya Wzanzibar tusitegemee lolote lenye baraka na Zanzibar, hali imeshaonekana kuwa Tanganyika wamepewa uhuru wakufanya watakavyo na viongozi wa SMz kimya bila cheche zozote kutoka ccm/smz wala cuf tulio zowea kuwa ndio watetezi wetu?.
  Hakuna mtu asio fahamu kuwa kila kitu kuhusu katiba ya Muungano hivi sasa kinabangwa na kupanguliwa na Watanganyika akina Rais Kikwete no 1 Waziri wa sheria Celina Komba no 2 na waziri mkuu no 3 sisi sisi Wzanzibar wetu wamo lakini imetafutwa ile mijitu milafi isio na elimu hata ya kisomo cha watu wazima wamesindikwa tu kuwemo ili kusaidia kumezwa Zanzibar.
  Mumeona Wzanzibar Tume ya Samuel Sitte na watu wake walio bobea Sheria na mumeona Wabambe wetu walio kuwemo kwenye tume, nivifuu vitupu hamuna hata mwana sheria moja niwatu wasio kuwa na upeo wa kujuwa vipengele vyovyote vya sheria wanaweza kuibiwa hivi hivi.
  Hii yote nimbinu tunazo fanyiwa halafu visokomezwe vipengele vyakutumiza na kuambiwa kuwa watu wetu walikuwemo ktk mchakato wa katiba kumbe ilio pelekwa ni midudu vifuu.
  Jengine baya zaidi nikuwa vipi suala kubwa kama hili la Muungano tukaambiwa kuwa Rais wa Tanganyika ijitayo Tanzania atashauriana na Raisi wa Zanzibar lakini mashauri hayo sio kama tufikiriavyo kuwa nguvu za Uraisi zitakuwa moja na mashauriano yatakuwa ya Raisi na Raisi no.
  Uhakika nikuwa Rahisi wa Zanzibar Dr Shene atashauriwa na Boss wake Kikwete na Mwenyekiti wake wa Chama kuwa nilivyo amua ni hivi na hivi ndivyo nitakavyo na wewe ni kutekeleza, hivyo ndivyo ukweli ulivyo.
  Sasa Wzanzibar ikiwa juzi dulishuhudia Rahisi wetu anapishwa rasmi kuwa Waziri ktk baraza la mawaziri na huku kikwete akiwa ndio rais na baraza lake la mawaziri jee Muungano wa nchi mbili kweli utakuwa na usawa wa nchi na nchi?
  Mimi nahisi viongozi wa smz tayari wameshaiuza Zanzibar na kuwa watifu mbele ya Kikwete na ndugu zake wakitanganyika.
  Ikiwa leo suala kumbwa kama hili la katiba ya Muungano ambalo linamkusa kila Mzanzibar leo tunambiwa mambo yote yako Bara na Rais wa Zanzibar atashauriwa? vipi rahisi huyu aweze kuwa na say wakati Kikwete kajifanya Super power na yeye ndio Boss kuliko Shein na ni kiongozi wake wa chama na kama tunavyo juwa kuwa ubovu wa ccm/smz ni kuwa watifu mno mbele ya chama?.
  Hapa Wzanzibar hatuna letu nikusubiri kukangwa kwa Katiba ya Muungano na sikweli wanavyosema Cuf(Maalim Seif) kuwa Wzanzibar subirini katiba mutowe maoni yenu no, nikusubiri wimbi kutuzamisha?.
  Haya nimaneno yalozoweleka kwa Maalim Seif kusema kila siku, kwani kila chaguzi ccm hutuibia na wakati pabavu tunapajuwa kuwa ni tume ya ccm ZEC na kuletewa Jeshi lakini mpaka leo cuf wameshindwa kupapatia dawa?.
  Kilichobaki nikuambiwa na cuf kuwa subirini mara hii mutakiano huku Wzanzibar wakawaida kuawa na kuteswa mateso ya kila aina.
  Mimi nasema ccm watatawala maisha kama tume haija badilishwa na kuwa independence na kuhusu kero za Muungano kama hawaja shauriwa Wzanzibar wenyewe kwa kura ya maoni isio simamiwa na ZEC basi kero za Muungano zitaendelea na kuzidi mpaka pale watakapo hakikisha kuwa Watanganyika wamechakuwa wengi Zanzibar na Wzanzibar wameshafunikwa hapo ndio kero za Muungano zitakisha kivipi?
  Nikuwa itapigwa kura ya maoni wapi wanataka Muungano na wapi hawataki kwa hio Wzanzibar milioni 1 watasema hawataki too late lakini Watanganyika milioni 3 kutoka mkowa wa Murogoro walokwishakuwa na uzanzibar powa watapitisha kwa kura zote kuwa Muungano tunautaka, hapo ndipo yalaitani.
  Hii ndio shabaha ya wenzetu wana focus ya mbali na ndio ukaona kila pembe ya madaraka hujichomeka Zanzibar bada tu ya msajili wa vitambulisho Juma Ame kuwapa vipande wageni na kuwanyima Wazawa kwaitikadi tu za chama huku akiihalalicha Zanzibar kuiuza kwa wageni wasio wa Zanzibar.
  Hivi sasa kuna ajira nyingi za kazi ndani ya Zanzibar basi wazanzibar hawapewi wanapewa wageni niaibu, eti tu utawaona viongozi wa smz wanasema wazanzibar niwavivu nna uislamu umewazidi iti hawawezi kutandika vitanda na kukamata nguruwe na ulevi.
  Hii sio kweli nikuwa ccm/smz wanaiuza nchi yetu kwa machogo na badae kutafuta visingizio vya unafiki na uongo.
  Kama wzanzibar hawawezi kutandika vitanda na kushika pombe? basi hata Bank ya watu wa Tanzania ilioko Zanzibar na sio Tanganyika ilioko Zanzibar Malindi hakuna Mzanzibar hata moja wote chogo, sasa tuseme mule munauzwa Bia na kutandika vitanda?
  Suala hili la Bank liliulizwa kwa waziri wa Fedha Bara na alilojibu nikuwa wazanzibar hawana qualification kazi zao kubwa nikupika chai na kufagia ndio kazi tulio tengewa ktk Bank ile.
  Sasa ikiwa tumefika hadi kuzalilishwa na kuzarauliwa jee kuna haja gani viongozi wetu wa ccm/smz kuwa na Muungano?.
  Au ndio biashara zenu na vijumba vyenu vilivyoko bara Mutanyaganywa ndio muiuze nchi ilio rasilimali ya Wzanzibar wenyewe?.
  Kama hatukujikaza Wzanzibar basi tusubiri shene atuuze na badae akimbilie kwao Bara alikokwisha kujipangia maicha yake ya Dunia na kusahau ya Ahera.
  wzanzibar tusimuamini ccm/smz yoyote yule hawa watu nikama lana mana mambo yote wanayo tufanyia vitimbi wtanganyika wao ndio wachangiaji wakubwa kwa vile wamekuwa hawaoni hawasikii kwa itikadi za chama na ukereketwa huku wakiacha uzalendo na utu wa nchi yao.
  Mungu kibariki kizazi shetu cha Zanzibar.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  <<<Hii sio kweli nikuwa ccm/smz wanaiuza nchi yetu kwa machogo na badae kutafuta visingizio vya unafiki na uongo.
  Kama wzanzibar hawawezi kutandika vitanda na kushika pombe? basi hata Bank ya watu wa Tanzania ilioko Zanzibar na sio Tanganyika ilioko Zanzibar Malindi hakuna Mzanzibar hata moja wote chogo, sasa tuseme mule munauzwa Bia na kutandika vitanda>>>

  Kumbe tatizo ni ubaguzi? Hivi ukilinganisha waZanzibari walioko bara na WaTanganyika walioko Zanzibar ni wapi wengi zaidi? Mbona humuwaiti ndugu zenu warudi kwenye dhiki yenu na akili finyu. Wewe mwandishi kwa unavyoandika kama vile ni cassette iliyorekodiwa hata ukipewewa kazi utaweza kweli? Na Uislamu unaingiaje? Njoo bara uone waislamu wanavyopiga mzigo. Au waZanzibari ndiyo waislamu wa kweli? Utalalamika mpaka kiama. Kama una uhakika unachokisema ndiyo msimamo wa wengi kwa nini msiipigie serikali yenu kura ya kutokuwa na imani nayo. Kelele kila siku, la! Muafaka mmepata lakini bado tu. Aliyekuwa nabii mkombozi wenu (Maalim) sasa ameishakuwa shetani!!!!
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  wazanzibar mmechelewa sana kuvunja muungano, nashangaa rais wenu anachaguliwa dodoma
   
Loading...