Sio CCM, Chadema wala CUF vinafaa kuongoza tanzania , tunahitaji chama mbadala. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio CCM, Chadema wala CUF vinafaa kuongoza tanzania , tunahitaji chama mbadala.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CANCER, Jul 16, 2012.

 1. C

  CANCER Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Kwa maovu ya CCM hivi sasa imepoteza uhalali wa kuongoza mfano ufisadi,manyanyaso kwa wananchi , kuuza rasilimali za nchi kwa wazungu na kukuza makundi.

  Vile vile CHADEMA haina wema wa kutawala wala wa kusema kuwa kinatetea masilahi ya wanyonge ukitazama ukabila unaoendelea mfano chacha wangwe alinyanyaswa , zito n.k, vitu maalumu ni vya kujua wamejaa watoto wa vigogo na wake zao, CHADEMA na udini.

  Maoni yangu watu waadilifu kama slaa, magufuli, sita, lisu, zito, mwakyembe, waungane na kuunda chama kisichokuwa na sula ya ukanda ufisadi, ukabila kama uchaga, ubabe kama wa Mbowe na umutandao kama lowasa.
   
 2. C

  Cartoons Senior Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Tatizo lako unasahau kuwa Tanzania ina zaidi ya vyama 10.
  Km CDM & CCM vimeshindwa kwa mawazo yako,vp kuhusu CUF,TLP,SAU,UDP,NCCR MAGEUZI n.k.?

  Tanzania haitaj chama kipya,vilivyopo vinatosha.
   
 3. C

  CANCER Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Tatizo ni muunganiko wa watu waadilifu vyama ulivyotaja ni vya waganga njaa havina nia na kuchukua dola
   
 4. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  na hicho chama kiingine unafikiri wanachama watatoka katika vyama vipi? si watameguka humo humo au una point gani ya maana mkuu labda ungesema wajerumani warudi, tatizo sio chama ni watu mkuu funguka
   
 5. b

  bdo JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Kwenye Red ... haiwezekani na ndio maana wako tofauti na hawako chama kimoja, ila kwa kuwa haujasema chochote kuhusu CUF, ngoja nikusaidie CUF wanaweza kuendelea kudumisha muungano wao na kuwa chama kimoja ili wazidi kushidwa na kusiwe na CCM A na CCM B
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Umekua mchanga mno ktk si ha sa, na post yako inakutambulisha ulivomwathirika wa ukosefu wa akili na uzoefu ktk si ha sa, vyama vipo kibao unajiunga kwa mtizamo wako na si kwa kuazima akili ya mtu mwingine kama Lusinde na mdogo wake Mwigulu machemba, ukisikia udini mtu kausema hana shule, ukisikia mtu anazungumzia ukanda hana shule, ufukara wa akili unamsumbua, hakuna chama kisichokuwa na viongozi wanao amini dini na ukanda.

  Mfano: CCM ndo chama kilicho jaza watumishi wa kanda fulani kuliko chama kingine chochote, ccm ndicho kinachotumia misikiti na mashehe, makanisa na maaskofu ktk kujipatia madaraka Mfano, jk ni chaguo la Mungu Askof Kilaini, viti, vifaa vya matangazo ya mikutano ya ccm Gwajima, Msichague CDM mashehe Igunga, angalia BOT, HAZINA, W ya Fedha, TRA, Vyuo vya veta vya mikoa, Wahadhili kwenye vyuo vikuu, Ma DC, Wabunge, majaji, Mahakimu, Angalia mikoa yenye shule na vyuo vikuu vingi, wafanyabiashara Kariakoo, angalia wagombea wa urais, anaglia viongozi wa vyama vyote.

  Nina uhakika kama una akili utajua ni nani wapo kila mahala na wanaongoza maeneo mengi, angalia hata bajeti za mikoa mwaka huu mikoa inayoongoza kwa kupewa fungu kubwa ni ile ile yenye mafanikio makubwa zaidi
   
 7. R

  Robson Mulabwa Senior Member

  #7
  Dec 21, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukitafakari mwenendo wa mambo ulivyo ndani ya upinzani ni wazi hakuna chama mbadala wa CCM na kwa hakika mpaka 2015 tutakuwa na vipande vya vyama tu na CCM kama kawa itashika hatamu sipendi ubishi mwenye akili anatambua ninachosema.
   
 8. jerrytz

  jerrytz JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 5,693
  Likes Received: 3,114
  Trophy Points: 280
  Hoja ni nzuri japo sikubaliani na wewe kwamba hakuna chama mbadala kwa ccm;moja yanayotokea upinzani ni mambo ya kawaida katika ulimwengu wa siasa tofauti tu ni namna wanasiasa wetu wanavyopambana na hoja wanazopambania; Pili sioni kama hawa wanaopambana wana potential za kuvuruga cdm; tatu mimi sio mwanachama wa cdm lakini naamini kuwa wana cdm watamaliza hili kwa kuwatoa wote wenye tuhuma hasa hawa vijana na hapo cdm itabaki salama
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwani umetumwa au unajituma? Mbona huongelei mitandao ya kimaslahi kwenye CCM? CCM sijua wala hewa. Itaondoka kama ilivyokuja.
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Njaa ndio inasumbua kila mtu Tanzania. Watu hawataki kufanya kazi wanakalia sihasa na "wanatengeneza" pesa kupita pesa chafu ya sihasa. CCM inacheza vizuri huu mchezo mchafu ndio maana wameishatahadharisha kuwa CHADEMA kwishney 2014! Kwani wanawatu wao wanaohakikisha baada ya uchaguzi wa CHADEMA, kinavunjika vipande vipande vingi vingi....CHAUMA, CHAUSTA, ADA, ADF, CHAMIMI, n.k.
   
 11. R

  Robson Mulabwa Senior Member

  #11
  Dec 21, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani kuelezea fikra lazima utumwe? hivi tunajenga jamii ya aina gani?? kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake sasa linakujaje suala la kutumwa??? hao mnaowatetea wamewatuma?? mkuu unanitisha kwa swali lako inaonesha huko uhuru wa mawazo ni usaliti tujipange jamani.
   
 12. R

  Robson Mulabwa Senior Member

  #12
  Dec 21, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu sina njaa kama unavyodhani na kamwe siwezi kuuza utu wangu kwa watu ni mtazamo wangu si kama nachumia tumbo sina shida hiyo mkuu.
   
 13. d

  dada jane JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nipambanuavyo mimi ni kwamba ukombozi wa kweli kwa Tanzania umefika. Na Mungu mwenzewe ndie atakae ratibu ukombozi huo. Kama imefika Akina Tuntemeke ni akina Festo Sanga.
   
 14. R

  Robson Mulabwa Senior Member

  #14
  Dec 21, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukombozi upo sawa lakin pia unaweza kupitia huko huko ccm tofauti na mnavyozani
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160

  Huo ndio ukweli, na hapa si upinzani kutoshinda pekee, bali ni ishara kuwa hawana uwezo wa kuongoza nchi na hata kama ikitokea wakashinda kwa bahati mbaya tunaweza kurudi nyuma kimaendelea badala ya kusonga mbele.
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Na hapa ndo upeo wetu wa kupambanua mambo unaonekana mdogo, iweje hali kama hiyo ikitokea ndani ya CCM tunakuja na mapambizo kuwa sasa mwisho wao umefika , lakini ikitokea ndania ya CDM iwe hali ya kawaida? Tusijifanye wachambuzi wa mambo ya siasa kwa kushabikia tu badala ya kusimama katika ukweli. Hakuna mgogoro wowote unaojenga sio kwenye siasa tu hata katika familia, katika michezo na kwingineko.
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Yap, ukombozi siyo lazima kubadili chama tawala, bali kubadili tabia za watawala ili kuwa wazalendo.
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Acha jazba CCM imesemwa sana kuhusiana na makundi iliyonayo na hayo yalionekana kama sababu ya kupoteza mvuto kwa wananchi, sasa sijui unaona tabu gani hayo hayo yanayotokea ndani ya CDM kuongelewa ili waweze kujirekebisha? Ni hatari sana kwa chama kichanga kama CDM, CCM kisiki cha mpingo kile, wanavutana lakini mwisho wa siku suluhu inapatikana tena kwa hoja. CDM ni hatari sana kwa vile migogoro yao ikizidi itachochewa sana na dhana nyingi zinazokitawala kama vile Ukabila, Udini n,k
   
 19. S

  Sumu JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 6,233
  Likes Received: 3,218
  Trophy Points: 280
  Chama mbadala kipo ila siyo hivi tunavyoviona sasa. CHADEMA walikuwa wameshanipa matumaini ila kadri 2015 inavyokaribia hali ya hewa ndo inavyozidi kuchafuka. Na kitu kitakachotuharibia kabisa CHADEMA ni hili swala la nani agombee uraisi kupitia chama chetu cha CHADEMA.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 20. R

  Robson Mulabwa Senior Member

  #20
  Dec 21, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wayahui walizani yesu angekuja na utukufu mwingi cha kushangaza akazaliwa katika familia maskini tena kwenye holi na ng'ombe so tufikirie juu ya ukombozi na ukombozi huo hauletwi na wanasiasa ni sisi wenyewe kufanya kazi za kuijenga nchi.
   
Loading...