Sinza yalipuka:...Abajalo yaichapa Mugabe FC na kutwaa seti ya jezi na zawadi nyingine... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sinza yalipuka:...Abajalo yaichapa Mugabe FC na kutwaa seti ya jezi na zawadi nyingine...

Discussion in 'Sports' started by Gang Chomba, Jul 18, 2011.

 1. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Klabu ya soka ya Abajalo ngilimaa ambayo ndio yenye mafanikio kuliko klabu yoyote ukanda wa Sinza, Ubungo, Mwenge na maeneo ya jirani wameweza kuwapa rrraha mashabiki wao na kukumbuka mafanikio ya kipindi kile cha kina Matokeo, Abeche, Adeba, Baba Dimu, Sagga, Modest, George Ngasongwa, Shomari, Raymond Ndunguru, Roberto Kalikawe, Kali Ongala na Baby Louis Mfede baada ya kukichapa goli 1-0 KILABU cha Mugabe FC iliokuwa umesheheni mapandikizi wa Ligi kuu kama Kijuso, Gumbo, Zahoro Pazi na wengine wengi huku wakiongozwa na striker wao Gaudence Mwaikimba aliyechemsha na kutolewa kipindi cha kwanza. Abajalo walifika fainali hii baada ya kuwatoa mahasimu wao timu ya Wakushi kwa sheria ya goli la ugenini. katika mchezo huo wa fainali dhidi ya Mugabe FC ya sinza Mugabe, Abajalo waliutawa mchezo huo kwa muda mwingi huku timu yao ikionekana kucheza kwa umoja na kujuana zaidi kutokana na kuwa na wachezaji wao wa siku zote na si wakuokoteza. Mechi hiyo iliyokuwa na mastaa wengi wa Sinza kama gang Chomba, Kwas Lee na wengine wengi ilikuwa ni ya amani na utulivu mkubwa tofauti na ilivyodhaniwa hapo awali. Abajalo wameendeleza furaha yangu iliyoanzishwa na AC Milan baada ya kuchukua ligi kuu ya Italia na kisha Yanga kuja kuchukua ligi ya hapa Bongo na kisha tena Yanga kuja kuchukua kombe la Kagame wiki ilopita...Forza Abajalo
   
Loading...