Sinunui tena hivi viwanja vya million moja moja ni kero tupu

Msemajiwao

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
638
1,531
Nimekubali ule msemo Wa ndege wafananao huruka pamoja!
Mwenzenu nilinunua Kiwanja cha million moja huko majoe ndani ndani!
Madalali waliniambia kwamba nisiwe na wasiwasi njia ipo, lakini cha ajabu baada ya kujenga na kuhamia, kuna jamaa mbele yangu kaja kujenga hadi kamaliza njia kiasi kwamba hata toroli halipiti!
Tumejaribu kumsihi jamaa atupatie njia hata Kwa kumpoza kagoma kuacha njia wakati upande Wa pili ana eneo kubwa tu kaliacha.
Wakati naendelea na mazungmzo upande Wa pili napo nimeshuhudia majilani zangu wakigombana kupeana nafasi ya kuweka Nguzo za umeme kiasi kwamba wenye maeneo ya mbele wamegoma kupitisha umeme kwenye vichochoro vyao.
Mwenzenu nimetafakali nikagundua kosa kubwa nililofanya nikukubali kununua viwanja vya bei ndogo! Kiasi kwamba nimezungukwa na roho za umasikini tupu!
Nataka nihame nikatafte hata Kiwanja cha million 10 ili nikae na wenye akili kuriko hapa kila siku migogoro! Naombeni ushauri wadau .
 
Mkuu ulivyowaza ndio ufanye hivyo .

Nina nyumba yangu ipo chamazi huko kiwanja nilinunua milioni mbili nusu nikajiona nipata bingo sasa hivi hata baiskeli haufiki nayo. Nimeweka wapangaji nyumba nzima mwenyewe nimehamia kwa wastaarabu wenzangu bora ununue kiwanja kwa gharama kubwa kuliko bei poa ukaanza kugimbana na waswahili wasiokuwa hata na wazo la kuja kumiliki gari huko mbeleni.
 
Ndiyo maana tunashauri mnapo nunua kiwanja lazima kuwashirikisha watu wa serikali ya mtaa inakuwa rahisi mwisho wa siku kupata ufumbuzi wa changamoto inapojitokeza eg, barabara na mipaka,
 
Mkuu ustaarab ulipaswa uanze nao mwenyewe. Kuna uwezekano mkubwa huna mahusiano mazuri na hao jirani zako kutokana na vile mfumo wako wa kuishi na watu na mazingira uliyopo hayaendani nao.
Mtu hukaribishi wageni ukirudi kwenye mihangaiko yako au siku za weekend hupiti kuwasabahi majirani na kucheka nao kidogo, uswahili hatuishi hivyo.
Portray image nzuri kwa majirani hata kama unawazidi kipato.
Halafu haijakaa njema hii ya kuwaita majirani zako eti "hawana akili".
Halafu ni umasikini wako ndo ulikufanya ununue kijiuwanja kifinyu kwenye makazi disorganized.

Hata utakako enda jijengee tabia ya ustaarabu utapendwa na kila mtu na kupewa ushirikiano wakutosha.
 
Mmmh kweli mjini kugumu

Yaani weekend ajipitishepitishe kuchekacheka na majirani??????
 
Mkuu ustaarab ulipaswa uanze nao mwenyewe. Kuna uwezekano mkubwa huna mahusiano mazuri na hao jirani zako kutokana na vile mfumo wako wa kuishi na watu na mazingira uliyopo hayaendani nao.
Mtu hukaribishi wageni ukirudi kwenye mihangaiko yako au siku za weekend hupiti kuwasabahi majirani na kucheka nao kidogo, uswahili hatuishi hivyo.
Portray image nzuri kwa majirani hata kama unawazidi kipato.
Halafu haijakaa njema hii ya kuwaita majirani zako eti "hawana akili".
Halafu ni umasikini wako ndo ulikufanya ununue kijiuwanja kifinyu kwenye makazi disorganized.

Hata utakako enda jijengee tabia ya ustaarabu utapendwa na kila mtu na kupewa ushirikiano wakutosha.

Mzee kuna maeneo ni pasua kichwa, yaani unazungukwa na kenge, yaani kitendo cha wewe kufanya mabidiriko yoyote kama kuweka plasta tayari uadui, ndio hayo ya kuzibiana njia, yaani ujinga kwa kwenda mbele.
 
Pole sana mkuu, mimi sikutaka rudia makosa ya wazazi wangu. walijenga eneo flan wakati tunahamia tulikua wachache tu na gari linafika mpaka home, dooh miaka kadhaa mbele balaa, jamaa wakajenga yani hovyo hovyo tu, mbele ya nyumba yetu kuna mtu kajenga choo yani noma sana. Mpaka wazee wakaiacha nyumba wakapangisha wakahamia mkoa,
 
Nimekubali ule msemo Wa ndege wafananao huruka pamoja!
Mwenzenu nilinunua Kiwanja cha million moja huko majoe ndani ndani!
Madalali waliniambia kwamba nisiwe na wasiwasi njia ipo, lakini cha ajabu baada ya kujenga na kuhamia, kuna jamaa mbele yangu kaja kujenga hadi kamaliza njia kiasi kwamba hata toroli halipiti!
Tumejaribu kumsihi jamaa atupatie njia hata Kwa kumpoza kagoma kuacha njia wakati upande Wa pili ana eneo kubwa tu kaliacha.
Wakati naendelea na mazungmzo upande Wa pili napo nimeshuhudia majilani zangu wakigombana kupeana nafasi ya kuweka Nguzo za umeme kiasi kwamba wenye maeneo ya mbele wamegoma kupitisha umeme kwenye vichochoro vyao.
Mwenzenu nimetafakali nikagundua kosa kubwa nililofanya nikukubali kununua viwanja vya bei ndogo! Kiasi kwamba nimezungukwa na roho za umasikini tupu!
Nataka nihame nikatafte hata Kiwanja cha million 10 ili nikae na wenye akili kuriko hapa kila siku migogoro! Naombeni ushauri wadau .
Mtu mwenye mawazo ya million moja hawezi kukaa na mwenye mawazo ya milioni hamsini
 
Back
Top Bottom