Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

"....Wakati mambo yanaenda kombo kuna wajinga wa chama tawala ikiwemo watangazaji, viongozi wa dini na wazee wenye ushawishi walikuwa wanaitangazia dunia kupitia redio Rwanda ipo salama hakuna chochote kibaya kinachoendelea kwani amani imetawala kabisa....."

Sentensi hiyo inafikirisha kweli kweli.
 
"....Wakati mambo yanaenda kombo kuna wajinga wa chama tawala ikiwemo watangazaji, viongozi wa dini na wazee wenye ushawishi walikuwa wanaitangazia dunia kupitia redio Rwanda ipo salama hakuna chochote kibaya kinachoendelea kwani amani imetawala kabisa....."

Sentensi hiyo inafikirisha kweli kweli.
Umezifananisha na kauli za Chama Chetu?
 
Ndiyo yanayoendelea kwa sasa huku
"....Wakati mambo yanaenda kombo kuna wajinga wa chama tawala ikiwemo watangazaji, viongozi wa dini na wazee wenye ushawishi walikuwa wanaitangazia dunia kupitia redio Rwanda ipo salama hakuna chochote kibaya kinachoendelea kwani amani imetawala kabisa....."

Sentensi hiyo inafikirisha kweli kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea.......

Sasa hapa ntaelezea tukio ambalo lilitokea hapa hapa ubalozini tukiwa kazini hatuna hili wala lile tena siku yenyewe j3, ni hivi kwanza naombanizungumzie jambo la kikazi kidogo unajua balozi ni mtu mwenye mambo mengi sanaa ya siri na ya wazi ndo maana nchii nyingi zilizoendelea hupenda kuwapeleka mabalozi ambao ni watu ambao ni mawaziri na wanadiplomasia kweli kweli wengine huwa ni watu wazito jeshini, au wameshawahi kukaa kwenye vitengo vya usalama wa nchii ,sasa ipo hivi unaweza ukawa unafanya kazi ubalozini ukawa unamuona balozi kama mara mbili hivi kwa week au hata mara tatu kwa mwezi si kwamba hayupo anakuwepo ila anakuwa na mambo mengine sanaa.

Sasa huyu mama kama nilivyosema awali ni mwanamama mweupe ila shupavu aise sijawahi ona ntaelezea matukio mawili aliyoyafanya humu hadi nikamvulia kofia , wala si mwongeaji sanaa sasa siku hiyo alikuwepo ofisini tukiwa tunaendelea na majukumu yetu kama kawaida ghafla tukasikia kelele kwa mbali kama kuna watu wamekimbizwa kelele nyingi sanaa kundi kubwa la watu wakawa wanakuja usawa wa ubalozi wetu, ubalozi ulikuwa imeangaliana na ubalozi wa malawi kama sio mozambique kuna Askali alikuwa analinda pale wa nchi yao ila kwetu walikuwa wanalinda walinzi wa kampuni za pale pale kigali ,watu wakawa wazidi kusogea sasa, ubalozi wetu ulikuwa na geti fupi la kama futi sita hivi, sisi tukawa tumejitokeza uwani kuangalia kulikoni ghafla tukaona watu wanaruka kuingia ubalozi wa jirani na akina dada wawili wanaruka kuingia ubalozi wetu na muonekano wao ulikuwa wakitusi mpaka hapo tukaelewa nini kinachoendelea na kwanini wanakimbizwa wauawe si vinginevyo sasa hapo ndo niliposhuhudia ujasiri ambao sijawahi uona kwa mwanamke yeyote toka nizaliwe

Wakati wale watu wanatishia kuingia ubalozini, Balozi akatokea ofisini kwake akawa anawaangalia tu bila kuongea chochote huku kushikilia redio call na ndo mara ya kwanza kumuona balozi ameshikilia redio call ikawa wanaangaliana balozi anawaangalia na wao wanamuangalia sisi wanaume kwa mabinti tumeshakimbia tupo gereje ndogo tunachungulia madirishani ila
Tunachungulia nakusikia kinachoendelea nje, sasa wao wanaimba na kupiga kelele za kutaka balozi awatoe hao mabinti balozi yeye akawa anaongea na redio call ,hebu vuta picha kibaka kakimbilia kwako halafu wananchi wanazunguka nyumba yako wanakwambia wanakupa dakika 4 uwe umewatoa la sivyo wanarushs magrouneti humo sasa hali ilikuwa kama ilivyo kuwa siku hiyo vurugu na makelele yakawa yanaendelea ubalozi mzima tumezungukwa ghafla akaruka njemba moja imejazia kweli kweli na panga lake, ikawa inamfuata balozi wala mama hukukimbia kurudi ndani alisimama hapo hapo, nilichosikia aliapokuwa anaongea kwenye redio call upande wa pili kwamba sasa mmeamua kuichokozaa tanzania kwa makusudi na umewatuma watu wako waje kuwaua watanzania ila tusilaumiane ila alikuwa anaongea kwa kinyarwanda balozi alikuwa anabonga kinyarwanda kama chake vile, ile njemba ikawa inazidi kumfuata ikafanya kama inatanyanyua panga kumkata shingoni, ndo akawa badala ya kujali kinachoendelea pale ndo akawa anazidi kulumbana na alikuwa anaongea nae na alikuwa kwenye redio call, njemba ikashusha panga taratibu ikawa inaisugua panga lake kwenye matiti yake yule mama (balozi) akalivuta lile panga akalitupa nje ya fensi aisee ile njemba ili kasirika ikawa inatukana kwa kinyarwanda vibaya ila kumpiga haimpigi ghafla ilipigwa filimbi yule njemba akarudi nyuma akapanda geti ikarukia njee na wenzake wakawa wanaimba tutarudi tanzania tunaficha ing'otanyi yani Watusi. Mara balozi dakika hiyo hiyo akawasha gari akafunguliwa geri akaondoka alikoelekea hatujui sasa ikawa kimbembe kwa tuliobaki mle na wale akina dada.uongo mbaya wale akina dada walikuwa visu hatariii ila Mbele ya kifo sikukumbuka hilo .

Jioni ikafika kila mtu akaondoka tukawa tumewaacha wale akina dada na mlinzi mle ubalozini mimi nikawahi geto kwangu mapema sikutaka siku hiyo kuzunguka mitaani nikalala bila hata kula, hamu unaotoa wapi ya kula wakati mchana umeponea chupuchupu .asubuhi tuliporudi tulikuta balozi amewachukua na ameondoka nao alipowapeleka hatujui mpaka leo huwa najiuliza aliwapeleke wapi mji ule uliojaa damu za watu.

Naomba swala matokio niishie hapa kwani matokeo madogomadogo mengi yalikuwa mengi sanaa sasa tutaendelea na hatua ya mwanzoni mwa mwaka 1993 ....sasa tunaingia katika hali ya hatari kuwahi kushuhudia katika maisha yangu yote.

Itaendeleaaaaaa.......... Usiku.



Sent using Jamii Forums mobile app
Balozi wenu alikuwa akijiendesha mwenyewe au ana dereva?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea........

Haya sasa maisha ya matukio madogo madogo ya uhalifu kama wizi, kutekana na kupotesana yakawa yanaendelea kiaina watu wanauawa maisha yanaendelea ,kwa mara ya kwanza nikajuta kuwepo nchini rwanda kikazi nikawa nimekinai matukio hayo
Nikaanza kuwaza je? Siku itokee nchi yetu Tanzania uwaudhi hawa jamaa si tutachinjwa kama kuku, ikabidi nipunguze matembezi ya usiku, rafiki yangu mkubwa akawa demu wangu.
Sasa hali ikawa inaendelea ila nikumbushie kitu demu wangu mamake alikuwa mtusi ila yeye alikuwa kama mchanganyiko hivi ila babake sikuwahi kumjua wala kumuona ila stori za mtaani ni kwamba alikuwa jera amefungwa kifungo cha mda mrefu sababu sijui wala sikuwahi kumuuliza hilo swala mpenzi wangu huyo. Sasa kuna kitu kikawa kinanishangaza nikiwa nae ananipigisha stori za kuhamia Tanzania ,yani anataka tuhame tanzania na mimi tuishi wote tena akawa yupo serious kabisa nikimuuliza unawaachaje ndugu zako anasema nisijali wao watabaki tu hakuna shida nahisi alishahisi kuna hatari inakuja mbeleniii.

Kama mnakumbuka nilisema , hapo mwanzoni nimesema ukiona vikundi vya ulinzi vya kisiasa vinaanza kubeba silaha hadharani jua sasa hali ya hatari inagonga hodi.
Sasa turukie kwenye dalili ya pili ambayo sasa ukiona hiyo jua nchii inaelekea shimoni dalili yenyewe ni pale unapoona unaenda dukani muuzaji anakwambia labda unaulizia unga yeye anakwambia hataki hela kama una sukari mpe sukari yeye akupe unga yani kwa wale wazee wa histori kule west Afrika walikuwa wanaita barter trade karne ya 16 unanipa kitu nakupa kitu ,hela haina Thamani tena kwa binadamu watu wanaangalia kitu sio pesa ukionahivyo juasasa nchi inaingia shimoni muda si mrefu yani imebaki miezi michache tu kama sio siku nchii isambaratike vipande ,sasa ikawa hivyo wahindi, Wasomali wenye hoteli mjini wakaanza kusepa moja moja unakaa unashangaa duka halifunguliwi kumbe wenyewe waeshaondoka maisha yakaanza kuwa magumu mjini. Bidhaa hazipatikani sasa njaa ikaanza. ikabidi balozi awasiliane na makao makuu Dar kuomba ushauri nini afanye uturudishe nyumbani au ubalozi ufungwe au makao makuji Dar wakagoma jibu likaja tusubiri kwanza.

Kuna upumbavu ulikuwa unaendelea nchini rwanda ,ndo maana nikasema hapo juu usimwamini mnyarwanda .unajua ni upumbavu gani yani sijui ni teknolojia ya chini kipindi hicho ,wakati mambo yanaenda kombo kuna wajinga wa chama tawala ikiwemo watangazaji viongozi wa dini na wazee wenye ushawishi walikuwa wanaitangazia dunia kupitia redio rwanda ipo salama hakuna chochote kibaya kinachoendelea kwani amani imetawala kabisa aise ukawa unapigwa wimbo flani wa chama kwenye redio rwanda kuhamasisha Wahutu wajilinde na chama chao popote walipo na wahakikishe maeneo yapo salama hakuna mchanganyiko wa damu yani wawe wao tu bila Watusi tafsiri yake wamalize Watusi wote, ila katika hili wanajeshi wengi hawakushiriki katika kuua kikatili Watusi walihamishiwa nje mji na mipakani kulinda na kupigana na RPF kazi ya kumaliza Watusi ilikuwa kazi ya interahamwe maisha yakawa magumu watu wakaanza kuikimbia kigali kwa siri yani unaamka asubuhi unakuta mlango wa jirani yako uko wazi amechukua vijavyobebeka kasepa japo sasa nami nikaanza kufikiri kurudi kuishi ibalozini swala narudi je sasa? Daahh demu wangu nimwachie nani nguvu ya penzi ikawa kubwa ,mtaani kwetu tukabaki watu wakuhesabika maisha yanazidi kuwa magumu.

Sasa njiani tukaanza kuwa tunapishana na wanajeshi wa ubelgiji wako kwenye mstari na bunduki za kivita nzito nzito kuuliza eti wamekuja kulinda ndugu zao na mali zao mambo yakawa magumu tukawa tunaelekea mwezi wa kumi na moja, sasa ikawa redioni ni propaganda tupu za vita ,Paulo kagame amechachama huko na jeshi lake mapambano yamepamba moto jeshi la rwanda li kawa kama limezidiwa ila propaganda za redio rwanda ni vita inaendelea jeshi limewapiga RPF limewarudisha msituni hali ikawa inaendelea hivyo uvamizi mipakani Ukawa ni report ya kila siku redioni plus propaganda za kupeana moyo nchi inazidi kuzama taratibu, hela haina Thamani tena, chakula hamna watu hawaelewi wafanyei nini nchi ikawa gizani..

Naomba leo niishie hapa......... Itaendelea kesho kutaja dalili ya mwisho nchii kuu ingia gizani rasmi na wingu la roho ya mauti linatanda angani hapo kinachobaki mtu anapambania nafsi yake

Usiku mwema itaendelea kesho.............

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu.
Sipati picha siku ya kwanza kufanikiwa kurudi Tanzania ulijisikiaje!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee unatudanganya.

Ulikumbana na mawasiliano magumu wakati umesoma chuo kikuu kwa hiyo na kiingereza hawajui hujui?

Kule mwanzo unesema unesoma chuo Kule Kule rwanda halafu wakati unaoata ajira unaenda kuripoti unasema Ni Mara yako ya kwanza kwenda nje ya nchi??


CHAIII HII

Sent using Jamii Forums mobile app
Matatizo yenu mnahamishia kwa mleta uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom