Sintopiga kura yangu 2010

Watanzania wengi sana hawana elimu ya uraia,
Pole sana Mokoyo,kweli umeonyesha hisia zako za moyoni,ni kweli kwa Tanzania kama si wendawazimu huwezi kuishi kwa hali iliyopo.Mfanyakazi analipwa 135,000/= kama kima cha chini na bado anakula maisha sawa na mkurugenzi wa shirika binafsi au lecturer pale chuo kikuu.Kwenye Grocery(sitting room)zinajaa wakati wote jioni,sasa utajiuliza wanapata wapi pesa.na watoto wanaenda shule za Academy,
Anajitokeza mpiganaji anayechukia umaskini huu anaitwa majina lukuki ya kifedhuli na watanzania wanakubali na kuamini na wengine kuahirisha kupiga kura kama ndugu yangu Mokoyo.
Mpambanaji yeyote vitani lazma awe mstari wa mbele kupambana mpaka siku ya mwisho bila kutetemeka,ukizidiwa bora ujiue kama Chifu Mkwawa kule Iringa.Sishauri watu wajiue bali wapambane kiume hata wakishindwa washindwe kiakili si kijingajinga au kijanjajanda.
Kupiga kura ni HIARI na si LAZIMA
Huu ni mtizamo wangu Mokoyo na WanaJamii Tanzania,
Hongera kwa JAMIIFORUM,Inapatikana kote ulimwenguni.CONGRATS
katumwa huyo dogo... si unajua tena akina mahimbo wako wengi tu, kila mmoja kwa namna yake!!

Kura zitapigwa na zitalindwa na tutakua tumetumia haki ya msingi!!! charity begins at home
 
Kuna mambo mengi sana huelewi, nafikiri pia unawakilisha wananchi wengi wasiokuwa na upeo, sasa jaribu kupitia mawazo ya wachangiaji watakusadia.

Wakuu tusikate tamaa watu kama hawa wapo wengi na ndiyo wapiga kura wenyewe tuwasaidie kuwapanua mawazo.
Unasema kweli kuwa watanzania hatuna elimu ya uraia lakini pia hata viongozi wetu hawana elimu ya uongozi ndio maana wamekalia kutudanganya na ukichanganya nao unaosema hawana upeo ndio haya yanatokea

hapo kwenye red zaidi ya Technician sijaona mchango mwingine wenye hoja nzito na za ushawishi
 
katumwa huyo dogo... si unajua tena akina mahimbo wako wengi tu, kila mmoja kwa namna yake!!

Kura zitapigwa na zitalindwa na tutakua tumetumia haki ya msingi!!! charity begins at home
Toa hoja basi ndugu yangu wacha utoto
 
Binafsi sijamuona mgombea wala chama kinachostahili kupata kura yangu ya uraisi, wagombea wote bado hawajavuka kwenye mstari wa kiwango cha chini kabisa cha ubora wa raisi nimtakaye.

Lakini nimemuona mgombea ubunge makini ambaye nitampigia kura yangu October 31.
 
katumwa huyo dogo... si unajua tena akina mahimbo wako wengi tu, kila mmoja kwa namna yake!!

Kura zitapigwa na zitalindwa na tutakua tumetumia haki ya msingi!!! charity begins at home

Kipindi kama hichi cha uchaguzi watu wana tumika ku diverge attenetion za mambo muhimu ya taifa na kupeleka kwenye mambo mepesi ambayo ingepaswa kuwa midahalo ya promaryy school tena standard three C. Badala mtu kutumia muda wake kuelimisha watu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi na kutumia haki yake ya msingi katika mambo kama haya yeye anatua 2 page za A4 kuelezea kiasi alivyokata tamaa. Hao ndio contemporary great sinker wetu
 
Hakika kama wapiga kura ndio baadhi ya wachangiaji hapa basi Tanzania tuna safari ndefu sana kuelekea katika ukombozi sahihi. Na hapa ndio nakubaliana na muandika makala mmoja aliyesema KIZAZI CHA MABADILIKO TANZANIA BADO HAKIJAZALIWA NA KAMA KIPO NDIO KWANZA WANA MIAKA MIWILI. Watu wanaongozwa na ushabiki husio na fikra zao wenyewe kwa kuoanisha na uhalisia wa maisha tunayoishi. Sasa kwa mfano huyu anayesema akina Mahimbo sijui na nani na nani ni hana hata sababu ya kusikiliza sera za wagombea wake ameshaandaa kura yake kwa ushabiki. Mimi nimetoa msimamo wangu wachangiaji wangenichallenge kwa kunieleza umuhimu wa kupiga kura na kunieleza uzuri wa wagombea kwa yale nisiyoyajua sasa kuniita mad, mwendawazimu, nimetumwa haina maana zaidi ya kuendelea kunipa nguvu kwenye hoja msimamo wangu wa awali. Asante Technician kwa mchango mzuri otherwise I better concentrate na kazi zangu maana hapa ni vijembe kama kampeni za wagombea wenyewe
 
Kipindi kama hichi cha uchaguzi watu wana tumika ku diverge attenetion za mambo muhimu ya taifa na kupeleka kwenye mambo mepesi ambayo ingepaswa kuwa midahalo ya promaryy school tena standard three C. Badala mtu kutumia muda wake kuelimisha watu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi na kutumia haki yake ya msingi katika mambo kama haya yeye anatua 2 page za A4 kuelezea kiasi alivyokata tamaa. Hao ndio contemporary great sinker wetu
ebu muone na huyu naye ni mpiga kura jamani, duh
 
Hakika kama wapiga kura ndio baadhi ya wachangiaji hapa basi Tanzania tuna safari ndefu sana kuelekea katika ukombozi sahihi. Na hapa ndio nakubaliana na muandika makala mmoja aliyesema KIZAZI CHA MABADILIKO TANZANIA BADO HAKIJAZALIWA NA KAMA KIPO NDIO KWANZA WANA MIAKA MIWILI. Watu wanaongozwa na ushabiki husio na fikra zao wenyewe kwa kuoanisha na uhalisia wa maisha tunayoishi.

Raisi wao alishasema 75% ya wananchi wake ni wafuata upepo tu, safari bado ni ndefu sana!!
 
Hainiingii akilini kusikia mtu mzima kama wewe huoni umuhimu wa kutopiga kura. Kutopiga kwako kura ni kuruhusu iongozi wabovu waendelee kuwa madarakani. Piga kura mkubwa kama ulijiandikisha!

Kama umempata kiongozi mwenye sifa unazozitaka ni vyema ukapige kura lakini si busara kupiga tu kura ata pale ambapo hakuna mgombea aliyetimiza sifa mama katika mizani yako ya kiongozi umtakaye, tuna matarajio tofauti sana...iangalie nafsi yako.

Ni usaliti mkubwa kwa nchi yako pale ambapo kura yako itamuwezesha kiongozi mbovu kuchukua madaraka, nafsi yangu haitaniruhu kushiriki katika hilo.
 
Msisumbuke na huyu layman upeo mdogo wa kufikiri!
Mmoja anakwambia atajenga flyovers na viwanja vya ndege tena kigoma, atahakikisha shule za secondary kila mwanafunzi atapata computer wakati hata umeme wenyewe hauna dalili ya kufika maeneo hayo.

Mwingine anakwambia sio rafiki wa mafisadina hilo liko proven (nani asiyejua kile ufisadi unaifanyia nchi hii) , kuandika upya katiba, elimu bora, utaratibu mpya wa upadaji mishahara amabao unazingatia hali halisi ya maisha (sio ataongeza mishahara) ambao hata asipokuwepo yeye taratibu bado utaendelea kusimamiwa, utaratibu mpya wa kulipa pension kwa wazee wanaostaafu.

Kama unshindwa kuchagua jibu sahihi kwenye hiyo multiple choice utaweza kuthamini umuhimu wa kura yako? Kura yako ndio mstakabari wa nchi, ni darasa bora, ufisadi free, matibabu bora. Kinachokusumbua wewe ni ubinafsi kujiona wewe ndio mwisho, hujui hapo nyuma ya kura yako kuna watoto wako, shangazi na wajomba

Endelea kubeba box. Nchi hii itajengwa na wenye moyo
 
Mkuu hapa umeongea jambo lililogusa moyo wangu na jinsi ninavyoithamini nchi yangu napata tabu sana kuona wananchi wanachagua viongozi wabovu huku wakifahamu kabisa. Hakika nami sitashiriki uovu huu
 
Msisumbuke na huyu layman upeo mdogo wa kufikiri!
Mmoja anakwambia atajenga flyovers na viwanja vya ndege tena kigoma, atahakikisha shule za secondary kila mwanafunzi atapata computer wakati hata umeme wenyewe hauna dalili ya kufika maeneo hayo.

Mwingine anakwambia sio rafiki wa mafisadina hilo liko proven (nani asiyejua kile ufisadi unaifanyia nchi hii) , kuandika upya katiba, elimu bora, utaratibu mpya wa upadaji mishahara amabao unazingatia hali halisi ya maisha (sio ataongeza mishahara) ambao hata asipokuwepo yeye taratibu bado utaendelea kusimamiwa, utaratibu mpya wa kulipa pension kwa wazee wanaostaafu.

Kama unshindwa kuchagua jibu sahihi kwenye hiyo multiple choice utaweza kuthamini umuhimu wa kura yako? Kura yako ndio mstakabari wa nchi, ni darasa bora, ufisadi free, matibabu bora. Kinachokusumbua wewe ni ubinafsi kujiona wewe ndio mwisho, hujui hapo nyuma ya kura yako kuna watoto wako, shangazi na wajomba

Endelea kubeba box. Nchi hii itajengwa na wenye moyo
Asante kwa uchambuzi wako unaweza kuwa na hoja za ushawishi lakini bado una jazba kama wagombea wako
 
Siku zote usiongozwe na hisia!Fanya lililo jema hata kama matokeo yake ni baada ya miaka 50. Wamarekani hao hao waliokuwa wanamwabudu Obama miezi michache iliyopita leo hii job approval yake iko below 50. Why? Output! Tusimnyime kura Mzee wa watu ambaye ame-fight sana na ame-sacrifice mengi. Tutampima kwa output yake na ikiwa haendi sawasawa tutamhukumu pia kwa kipimo kile kile kama wanacho hukumiwa wengine!
 
Pamoja na kuwa nakubali kwamba kupiga au kutopiga kura ni haki ya kila mtu mwenye sifa za kufanya hivyo, naamini kabisa kuwa kupiga kura ni jambo jema kama kweli mtu ana nia njema na nchi yake.

Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna wagombea zaidi ya watatu walioorodheshwa na mtoa mada. Kama hao watatu hawatoshi kumshawishi awachague, basi napendekeza aangalie na hao wengine waliobaki ili afanye maamuzi yenye manufaa zaidi.

Kwa mtazamo wangu, wachangiaji wengi wa thread hii wameamua kumshambulia mtoa mada bila kumsaidia kwa lipi linaloweza kumfanya ashirikiane na watanzania wenzake katika uchaguzi wa mgombea bora zaidi. Mimi naomba nijaribu kumshawishi ndugu Mokoyo na wengine wengi ambao kwa sababu moja au nyingine hawaoni umuhimu wa kutumia muda wao kushiriki katika kuchagua viongozi October 31. Nitajaribu kufanya hivyo kwa kuanza na yale aliyoyaainisha kuwa yanamchefua.
Mgombea wa Urais chama cha 1:- Huyu kaahidi kununua meli kubwa za kimataifa kwenye maziwa mawili tofauti. Pia kaahidi kujenga international airport kwenye mikoa miwili. Pia kaahidi mambo mengine kibao kama mishahara, mashule, mahospitali, kusuluhisha migogoro ya ardhi n.k. Ebu tujiulize ni mikakati na mbinu gani zitafanya haya mbona hatupewi mikakati. Je mbona hizi ni ahadi za kawaida na hazishtui masikio ya walio makini katika kufuatilia uhai wa nchi yao. Zitatekelezekaje? Nani atafanya? Kwani hakufanya kipindi kilichopita?
Mimi pia nashindwa kuelewa uwezo uliopo katika kutoa ahadi hizi kubwa, hasa ukizingatia kuwa mgombea huyu anajua vyema hali ya uchumi wa nchi yetu na miundombinu yake. Kununua meli mbili kwa ajili ya kila bandari si jambo baya. Ni jambo jema. Ila yeye huyu huyu amekuwa akitumia pesa kwa mambo yasiyo ya kimaendeleo zaidi na kudai kudai kuwa serikali yake haina pesa za kutosha kiasi cha hata bajeti iliyopita kujitengea pesa za kujenga barabara sehemu chache kwa kujipendelea. Sioni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaiwezesha serikali yake kutimiza ahadi hizo mpya, hasa kabla hajatimiza zile alizozitoa mwaka 2005.

Huyu sina imani nae kabisa.
Mgombea wa Urais chama cha 2:- Huyu kwanza kaahidi kuwa yeye sio rafiiki wa mafisadi, yeye atatoa elimu bure kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu, rasilimali za nchi zitatumika sawia kwa wananchi wote pasipo ubaguzi, huduma za afya zitaboreshwa hakuna tena kutumia machela kupeleka wagonjwa hospitali. Maswali ya kujiuliza anaoambatana nao ni wasafi kiasi gani mpaka yeye azungumze hivyo? Mbona hata mikakati yake haiku wazi na ina ukungu? Hiyo elimu bure itakujaje? Shule ziko wapi? Vyuo viko wapi? Waalimu wako wapi? Madaktari wako wapi? N.k
Pamoja na kuwa ahadi alizotoa zinahitaji pesa nyingi. Naona kuwa ni ahadi ambazo ni muhimu sana kwa ustawi wa Taifa changa (sijui litaendelea kuwa changa hadi lini). Elimu ndio msingi wa maendeleo ya kweli kwa jamii ya kisasa. Nchi yoyote na hasa yenye rasilimali kama tulizonazo, inaweza kuhakikisha kiasi kikubwa cha watu wake wanapata elimu bora na kwa ukamilifu. NI mikakati tu ndio ambayo inahitajika kuhakikisha hili linafanikiwa. Lakini mikakati yoyote ni lazima ianzie kwenye nia.
Usawa katika matumizi ya rasilimali ni jambo la kisera, na linaweza kufanikiwa kwa kushirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa katika uamuzi wa maendeleo yao na ushirikishwaji katika kutekeleza sera mbalimbali za ustawi wa maisha yao.
Ubora wa hospitali na huduma zake, ubora wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama, ubora wa miundombinu yetu ni vitu vinavyohitaji kufanyiwa mabadiliko ya haraka ili kujenga taifa lenye afya na maendeleo ya haraka. Haiwezekani serikali kujivunia maendeleo bila kuhakikisha kuwa watu wake wako hai, salama na wana nguvu za kuyashiriki maendeleo hayo. Hili ni jambo linalowezekana kama nia ipo.

Mimi naamini zaidi ahadi za mgombea huyu, zinaonekana kuwa objective, achievable na measurable.
Mgombea wa Urais chama cha 3:- Huyu naye kama wengine kaahidi elimu ya bure bure kabisa, kaahidi ajira tele na kupandisha mshahara maradufu, kupunguza kodi kibao ili ziwe affordable, kaahidi umoja na ushirikiano, barabara safi kila mkoa na wilaya pia tarafa na kata. Lakini vile vile serikali ndogo isiyo na gharama kubwa. Huyu naye anatia shaka kwenye kuyatekeleza haya maana mengi ni maneno yasiyo na mikakati inayochambulika.
Kama zilivyo ahadi za mgombea wa pili hapo juu, naamini pia kuwa ahadi za mgombea huyu zinatekelezeka kwa urahisi kama serikali itakayoundwa itakuwa na nia ya kuzitekeleza. Ni masuala ya kisera zaidi.

Tatizo pekee nililonalo na mgombea huyu ni ufahamu wake katika utekelezaji wa sera na ushiriki katika mipango ya ukuaji wa ustawi wa jamii na utungaji wa sheria. Hajawahi kushiriki katika uongozi wowote wa umma kama waliotangulia hapo juu. Hii inanipa shida ya kujua uwezo wake wa kuhudumia umma.
MATARAJIO YANGU:- Matarajio yangu yalikuwa ni kuwa na mgombea ambaye hasingekuwa na ahadi za uongo kiasi hiki ila awe mgombea ambaye angetoa mhutasari mzima wa matatizo ya nchi hii toka tumepata uhuru. Vilevile atoea mhutasari wa mafanikio ya nchi hii na mwisho aseme kuwa nipeni nchi nibadilishe mfumo mzima nchi inahitaji mapinduzi katika mifumo yote inahitaji watu wapya waadilifu na wenye kuelewa kuwa ubadhirifu wowote ni kosa la kunyongwa na kutupwa kwenye makaa ya mawe. Nchi yenye msimamo wa mabo yake ya ndani na nje, nchi yenye kuwasafisha kwanza viongozi wote waliowachafu waliokalia nyadhifa kwa kipindi na kujichotea railimali pasipo uhalali wowote. Tunahitaji viongozi wenye akili tofauti zinazowaza tofauti na kutenda tofauti kabisa. Si viongozi ahadi ambazo ukweli ni kuwa mwaka 2015 utafika hata robo yake hazijatekelezwa kwa asilimia 50.

Mkuu, kampeni ni kujaribu kutafuta ushawishi ili uweze kupata kura zaidi ya wale unaoshindana nao. Katika kampeni, kila mgombea anatakiwa kusema anayoweza kuyatekeleza katika kipindi atakachokuwa kiongozi na mara nyingi huzidisha chumvi kidogo ili kuvuta ushawishi zaidi. Ni vyema kutambua ukweli huu na cha msingi zaidi kuangalia utashi wa ndani wa kila mgombea. Kipindi hiki hakuna mgombea anaekuwa bora zaidi kama hakuwa bora siku za nyuma. Ni kipindi cha kujitambulisha, kuelezea na kushawishi kuwa, kati ya wote wanaoomba nafasi hiyo, yeye ni bora zaidi.

Ukweli ni kuwa hakuna hata mmoja asie na mapungufu. Ni mapungufu hayo ndio yanayoweza kuwafanya wananchi kuamua wanaeweza kumvumilia kwa kipindi chote cha uongozi unaokuja.

Ushauri wangu ni kushirikiana na wananchi wenzako kuamua japokuwa huridhiki kwa kiasi kikubwa, nani atakaekuwa kiongozi wako ili asiefaa asipate nafasi ya kuongoza kutokana na watu wengi kukata tamaa ya kushiriki uchaguzi. Nakuomba ushirikiane nasi sote kuchagua kiongozi bora kwa Taifa letu na vizazi vijavyo.
 
Pamoja na kuwa nakubali kwamba kupiga au kutopiga kura ni haki ya kila mtu mwenye sifa za kufanya hivyo, naamini kabisa kuwa kupiga kura ni jambo jema kama kweli mtu ana nia njema na nchi yake.

Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna wagombea zaidi ya watatu walioorodheshwa na mtoa mada. Kama hao watatu hawatoshi kumshawishi awachague, basi napendekeza aangalie na hao wengine waliobaki ili afanye maamuzi yenye manufaa zaidi.

Kwa mtazamo wangu, wachangiaji wengi wa thread hii wameamua kumshambulia mtoa mada bila kumsaidia kwa lipi linaloweza kumfanya ashirikiane na watanzania wenzake katika uchaguzi wa mgombea bora zaidi. Mimi naomba nijaribu kumshawishi ndugu Mokoyo na wengine wengi ambao kwa sababu moja au nyingine hawaoni umuhimu wa kutumia muda wao kushiriki katika kuchagua viongozi October 31. Nitajaribu kufanya hivyo kwa kuanza na yale aliyoyaainisha kuwa yanamchefua.
Mimi pia nashindwa kuelewa uwezo uliopo katika kutoa ahadi hizi kubwa, hasa ukizingatia kuwa mgombea huyu anajua vyema hali ya uchumi wa nchi yetu na miundombinu yake. Kununua meli mbili kwa ajili ya kila bandari si jambo baya. Ni jambo jema. Ila yeye huyu huyu amekuwa akitumia pesa kwa mambo yasiyo ya kimaendeleo zaidi na kudai kudai kuwa serikali yake haina pesa za kutosha kiasi cha hata bajeti iliyopita kujitengea pesa za kujenga barabara sehemu chache kwa kujipendelea. Sioni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaiwezesha serikali yake kutimiza ahadi hizo mpya, hasa kabla hajatimiza zile alizozitoa mwaka 2005.

Huyu sina imani nae kabisa.
Pamoja na kuwa ahadi alizotoa zinahitaji pesa nyingi. Naona kuwa ni ahadi ambazo ni muhimu sana kwa ustawi wa Taifa changa (sijui litaendelea kuwa changa hadi lini). Elimu ndio msingi wa maendeleo ya kweli kwa jamii ya kisasa. Nchi yoyote na hasa yenye rasilimali kama tulizonazo, inaweza kuhakikisha kiasi kikubwa cha watu wake wanapata elimu bora na kwa ukamilifu. NI mikakati tu ndio ambayo inahitajika kuhakikisha hili linafanikiwa. Lakini mikakati yoyote ni lazima ianzie kwenye nia.
Usawa katika matumizi ya rasilimali ni jambo la kisera, na linaweza kufanikiwa kwa kushirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa katika uamuzi wa maendeleo yao na ushirikishwaji katika kutekeleza sera mbalimbali za ustawi wa maisha yao.
Ubora wa hospitali na huduma zake, ubora wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama, ubora wa miundombinu yetu ni vitu vinavyohitaji kufanyiwa mabadiliko ya haraka ili kujenga taifa lenye afya na maendeleo ya haraka. Haiwezekani serikali kujivunia maendeleo bila kuhakikisha kuwa watu wake wako hai, salama na wana nguvu za kuyashiriki maendeleo hayo. Hili ni jambo linalowezekana kama nia ipo.

Mimi naamini zaidi ahadi za mgombea huyu, zinaonekana kuwa objective, achievable na measurable.
Kama zilivyo ahadi za mgombea wa pili hapo juu, naamini pia kuwa ahadi za mgombea huyu zinatekelezeka kwa urahisi kama serikali itakayoundwa itakuwa na nia ya kuzitekeleza. Ni masuala ya kisera zaidi.

Tatizo pekee nililonalo na mgombea huyu ni ufahamu wake katika utekelezaji wa sera na ushiriki katika mipango ya ukuaji wa ustawi wa jamii na utungaji wa sheria. Hajawahi kushiriki katika uongozi wowote wa umma kama waliotangulia hapo juu. Hii inanipa shida ya kujua uwezo wake wa kuhudumia umma.

Mkuu, kampeni ni kujaribu kutafuta ushawishi ili uweze kupata kura zaidi ya wale unaoshindana nao. Katika kampeni, kila mgombea anatakiwa kusema anayoweza kuyatekeleza katika kipindi atakachokuwa kiongozi na mara nyingi huzidisha chumvi kidogo ili kuvuta ushawishi zaidi. Ni vyema kutambua ukweli huu na cha msingi zaidi kuangalia utashi wa ndani wa kila mgombea. Kipindi hiki hakuna mgombea anaekuwa bora zaidi kama hakuwa bora siku za nyuma. Ni kipindi cha kujitambulisha, kuelezea na kushawishi kuwa, kati ya wote wanaoomba nafasi hiyo, yeye ni bora zaidi.

Ukweli ni kuwa hakuna hata mmoja asie na mapungufu. Ni mapungufu hayo ndio yanayoweza kuwafanya wananchi kuamua wanaeweza kumvumilia kwa kipindi chote cha uongozi unaokuja.

Ushauri wangu ni kushirikiana na wananchi wenzako kuamua japokuwa huridhiki kwa kiasi kikubwa, nani atakaekuwa kiongozi wako ili asiefaa asipate nafasi ya kuongoza kutokana na watu wengi kukata tamaa ya kushiriki uchaguzi. Nakuomba ushirikiane nasi sote kuchagua kiongozi bora kwa Taifa letu na vizazi vijavyo.
Recta I wish wewe ndie ungekuwa mgombea maana unajua kuchambua fikra na mahitaji ya wananchi wako. Umezungumza jambo moja kubwa na la msingi kuwa kampeni si wakati wa kumtafuta aliye bora ila ubora wa mgombea unatakiwa uonekane toka mwanzo nyakati za nyuma. Kwa hili nakuunga mkono lakini piaukazungumzia kuwa kampeni ni sehemu ya kufanyia ushawishi ili mgombea auzike kwa wapiga kura ni kweli kabisa lakini wasitake tuwanunue kwa uongo wao ila kwa facts zao. Unajua kujua kuongea sio kujua kutenda ingawa kuna maana kubwa sana unapojua kuongea na kujua kutenda pia

Pia nashukuru kwa kujaribu kuona baadhi ya ahadi za wagombea niliowachambua hapo juu kuwa ni za uongo na uzandiki wa hali ya juu.

Mwisho niseme kuwa tunahitaji kiongozi mwanamapinduzi mwenye itikadi ambayo hata wananchi wenyewe wataiona kama kulamba sumu vile lakini matokeo yake baadaye yawe ya kusherehekea na siyo kiongozi ambaye maneno yake na misimamo yake ni kama kulamba asali lakini matokeo yake yawe kilio na kusaga meno.

Kuambiwa elimu bure kila siku sio jambo la kushangilia tunataka serikali ambayo itahahakikisha kuwa wananchi wanaweza kutumia akili zao na rasilimali zilizopo kama vile madini, misitu, ardhi na nyinginezo kujikwamua kimaisha ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wao kwa kulipa karo ya shule. Leo hii siwezi kushangilia elimu ya bure kwa sababu ina maana tutaendelea kuibiwa na viongozi wachache kwa sababu hiyo hiyo.
 
Unasema kweli kuwa watanzania hatuna elimu ya uraia lakini pia hata viongozi wetu hawana elimu ya uongozi ndio maana wamekalia kutudanganya na ukichanganya nao unaosema hawana upeo ndio haya yanatokea
Mabadiliko yanaanzia kwako. Nakuomba ukapige kura ili uingie ktk historia mpya ya waliochangia Mabadiliko. Taifa linahitaji kubadilika sasa na wa kubadili ni mimina wewe na wote wenye mapenzi mema. Kwa Pamoja Tutafika.
 
Binafsi sijamuona mgombea wala chama kinachostahili kupata kura yangu ya uraisi, wagombea wote bado hawajavuka kwenye mstari wa kiwango cha chini kabisa cha ubora wa raisi nimtakaye.

Lakini nimemuona mgombea ubunge makini ambaye nitampigia kura yangu October 31.
Please! kuwa serious japo kidogo,hatuja test the difference,make it happen! We porojo si umezizoea? Tunataka kuachana nazo sasa.
 
unanikumbusha maneno ya jenerali:

"Tunachagua kama vipofu, kisha tunalalama kama vichaa. Sasa tuamue: ama tuchague viongozi wetu kwa makini, au tukae kimya wakati wakitunyanyasa. Wachagua hovyo wasiwe wasema hovyo wakitendewa hovyo."

source: Raia Mwema
 
Back
Top Bottom