Sintopiga kura yangu 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sintopiga kura yangu 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mokoyo, Sep 9, 2010.

 1. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Kwanza nianze kwa kusema kuwa mimi sio mwanachama wala mkereketwa wa chama chochote kile sio CCM, Chadema, CUF, TLP, NCCR-Mageuzi au chochote kingine.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya kusema hayo kwa kifupi tu sababu iliyonifanya kuamua kutokupiga kura yangu kwa mwaka huu wa 2010. Kimsingi naipenda nchi yangu na ningetamani siku moja iwe nchi yenye uchumi imara, amani na utulivu madhubuti na zaidi ya yote iwe na viongozi madhubuti ambao ndio chanzo cha hayo yote mema. Siku zote nimekuwa nikiwaza kuwa na viongozi wenye mawazo mbadala wa kubadilisha mwelekeo wa nchi hii. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kubadilisha kwangu msimamo wa kupiga kura mwaka huu kumetokana na kukosa wagombea wenye nia dhabiti ya kuibadilisha nchi hii itoke katika dimbwi la ufukara. Hakuna hasiyejua kuwa nchi yetu inakabiliwa na matatizo vyungu nzima kwenye kila sekta kuanzia elimu, barabara, kilimo, utalii, madini, afya n.k. Lakini jambo la kushangaza bado wagombea Urais tulio nao mwaka huu wamekuwa wagombea wale wale hapa nikiwa na maana ya wagombea wenye mawazo yaleyale mgando kuwa matatizo ya nchi hii yataondolewa kwa ahadi za kufanyia hiki na kile wakati wanajua kabisa kuwa hawawezi kutekeleza hata theluthi moja ya ahadi zao. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama Mtanzania nimekuwa nafuatilia kampeni za kila chama kwa vile vilivyokwishaanza kwa makini sana katika kujua ni kiongozi gani nimchague kwaajili ya uhai wa nchi yangu. Lakini mpaka hapa nilipo tayari kampeni hizi ZIMENIKIFU na KUNIKINAISHA kwa asilimia 100. Sababu kubwa ya kukinaishwa na kampeni hizi ni ahadi wanazotoa wagombea wote wa Urais kwanza na wale wa ubunge. Na kwa bahati mbaya sana wananchi tumekuwa kama vilema wa akili wenye utindio wa ubongo(samahanini kama hapa nimewakwaza ila ndio ukweli) kwani tumekuwa tunashangilia na kufurahia mpaka kusukuma magari ya wagombea hawa kwa nguvu zetu ambazo kwa akili yangu mimi ningezitumia kwenda kutafuta chakula cha watoto wangu wasiokuwa na maisha bora. Nina mifano kama hii hapa chini[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mgombea wa Urais chama cha 1:- Huyu kaahidi kununua meli kubwa za kimataifa kwenye maziwa mawili tofauti. Pia kaahidi kujenga international airport kwenye mikoa miwili. Pia kaahidi mambo mengine kibao kama mishahara, mashule, mahospitali, kusuluhisha migogoro ya ardhi n.k. Ebu tujiulize ni mikakati na mbinu gani zitafanya haya mbona hatupewi mikakati. Je mbona hizi ni ahadi za kawaida na hazishtui masikio ya walio makini katika kufuatilia uhai wa nchi yao. Zitatekelezekaje? Nani atafanya? Kwani hakufanya kipindi kilichopita?[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mgombea wa Urais chama cha 2:- Huyu kwanza kaahidi kuwa yeye sio rafiiki wa mafisadi, yeye atatoa elimu bure kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu, rasilimali za nchi zitatumika sawia kwa wananchi wote pasipo ubaguzi, huduma za afya zitaboreshwa hakuna tena kutumia machela kupeleka wagonjwa hospitali. Maswali ya kujiuliza anaoambatana nao ni wasafi kiasi gani mpaka yeye azungumze hivyo? Mbona hata mikakati yake haiku wazi na ina ukungu? Hiyo elimu bure itakujaje? Shule ziko wapi? Vyuo viko wapi? Waalimu wako wapi? Madaktari wako wapi? N.k[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mgombea wa Urais chama cha 3:- Huyu naye kama wengine kaahidi elimu ya bure bure kabisa, kaahidi ajira tele na kupandisha mshahara maradufu, kupunguza kodi kibao ili ziwe affordable, kaahidi umoja na ushirikiano, barabara safi kila mkoa na wilaya pia tarafa na kata. Lakini vile vile serikali ndogo isiyo na gharama kubwa. Huyu naye anatia shaka kwenye kuyatekeleza haya maana mengi ni maneno yasiyo na mikakati inayochambulika.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ahadi za wabunge ndio kabisa sitaki hata kuzichambua maana ni vichefuchefu vitupu.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]MATARAJIO YANGU:- Matarajio yangu yalikuwa ni kuwa na mgombea ambaye hasingekuwa na ahadi za uongo kiasi hiki ila awe mgombea ambaye angetoa mhutasari mzima wa matatizo ya nchi hii toka tumepata uhuru. Vilevile atoea mhutasari wa mafanikio ya nchi hii na mwisho aseme kuwa nipeni nchi nibadilishe mfumo mzima nchi inahitaji mapinduzi katika mifumo yote inahitaji watu wapya waadilifu na wenye kuelewa kuwa ubadhirifu wowote ni kosa la kunyongwa na kutupwa kwenye makaa ya mawe. Nchi yenye msimamo wa mabo yake ya ndani na nje, nchi yenye kuwasafisha kwanza viongozi wote waliowachafu waliokalia nyadhifa kwa kipindi na kujichotea railimali pasipo uhalali wowote. Tunahitaji viongozi wenye akili tofauti zinazowaza tofauti na kutenda tofauti kabisa. Si viongozi ahadi ambazo ukweli ni kuwa mwaka 2015 utafika hata robo yake hazijatekelezwa kwa asilimia 50.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Sipigi kura ingawa hapo awali nilipanga kufanyia hivyo. Sina wa kunishawishi vinginevyo [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mungu ibariki Tanzania[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mokoyo Jr[/FONT]
   
 2. b

  bobishimkali Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokupiga kura siyo suluhisho la kuondokana na matatizo yaliyopo nchini. Haya ni mawazo mgando yasiyofaa kuingia vichwani mwa watanzania.

  Wewe acha kupiga kura lakini sisi tutapiga kwani tunajua maana na umuhimu wa kupiga kura
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  So what? Mokoyo that your business usipopiga wengine watapiga na viongozi watapatikana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Hainiingii akilini kusikia mtu mzima kama wewe huoni umuhimu wa kupiga kura. Kutopiga kwako kura ni kuruhusu iongozi wabovu waendelee kuwa madarakani. Piga kura mkubwa kama ulijiandikisha!
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Kaka kapige tu kura. Wenzetu CCM wana genge lao la ulaji ambalo linataka watu wasipige kura ili watu wao wapite kiulaini.
   
 6. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  hamna sehemu nimeshawishi watu wengine wasipige kura, nimesema mimi, niache niendelee kuwa mimi na mawazo yangu, wewe ni wewe na fikra zako
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  its my business kweli, wengine wapige kura waweke viongozi walewale wasio na mwazo tofauti lakini mimi nitakuwa na amani kuwa si mshiriki wa kuangamiza nchi yangu!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hayuko bongo huyu, anatuzuga tu hapa na sentensi ndefu... waswahili wanasema hata "chongo ni mfalme katika vipofu", kwa msemo huo kati ya hao watatu mmoja ni chongo na wawili ni vipofu, basi nitampigia huyo chongo [kwa matazamo wangu

  I will vote na nasikitika kwamba hatuna means za kusaidia wapiganaji wetu walio nje kushiriki voting wakati hata mozambique majirani zetu wanaweza

  inshallah
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Sio lazima, nilijiandkisha kwa lengo la kupiga kura lakini nimesitisha, sio lazima kama sioni mabadiliko yoyote mapya
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Kutokuwa au kuwa bongo hakuondoi uhalali wa kupenda na kuthamini nchi yako

  Utaendelea kusikitika daima na kama ndio mpango wako huo wa kuchagua chongo
   
 11. Muacici

  Muacici JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mokoyo tupo pamoja hata mimi siwezi kupoteza muda wangu, hadi hapo nitakapoona hii nchi ni ya demokrasia. Kwani upende usipende wababe watachukua nchi hata kwa udi na uvumba. Hivyo sitaki kuihudhuinisha nafsi yangu. Hongera kwa uamuzi huo.
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  mimi sjashawishiwa na hilo genge na wala siwajui wapo upande gani wa hapa ninapoishi, ni maamuzi yangu binafsi
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kumbe ulikua unataka ligi... haya endelea nayo
   
 14. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mokoyo am afraid to say zati yua madi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  league iko wapi hapo? Au unataka ukiandika usijibiwe? Au na wewe mgombea ambaye unadanganya wananchi kuwa chongo lako sio tatizo? Pole bana mimi nimetoa msimamo wangu wewe ndio umeingia humu unajibiwa unakuwa mbogo, pole Acid
   
 16. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Dont be afraid Super Star ni mawazo yako, nayaheshimu as long as am not na unatumia haki yako ya kutoa maoni kama nilivyotumia ya kwangu
   
 17. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi sana hawana elimu ya uraia,
  Pole sana Mokoyo,kweli umeonyesha hisia zako za moyoni,ni kweli kwa Tanzania kama si wendawazimu huwezi kuishi kwa hali iliyopo.Mfanyakazi analipwa 135,000/= kama kima cha chini na bado anakula maisha sawa na mkurugenzi wa shirika binafsi au lecturer pale chuo kikuu.Kwenye Grocery(sitting room)zinajaa wakati wote jioni,sasa utajiuliza wanapata wapi pesa.na watoto wanaenda shule za Academy,
  Anajitokeza mpiganaji anayechukia umaskini huu anaitwa majina lukuki ya kifedhuli na watanzania wanakubali na kuamini na wengine kuahirisha kupiga kura kama ndugu yangu Mokoyo.
  Mpambanaji yeyote vitani lazma awe mstari wa mbele kupambana mpaka siku ya mwisho bila kutetemeka,ukizidiwa bora ujiue kama Chifu Mkwawa kule Iringa.Sishauri watu wajiue bali wapambane kiume hata wakishindwa washindwe kiakili si kijingajinga au kijanjajanda.
  Kupiga kura ni HIARI na si LAZIMA
  Huu ni mtizamo wangu Mokoyo na WanaJamii Tanzania,
  Hongera kwa JAMIIFORUM,Inapatikana kote ulimwenguni.CONGRATS
   
 18. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wewe ni mtapa maji tu. Unatakiwa ujue wajibu wako wa kupiga kura kama umejiandikisha. Kutokupiga kura si suluhisho ya matatizo. PIGa kura, mchague Dr Slaa
   
 19. matuse

  matuse Member

  #19
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kama ulikuwa na mpango wa kumpigia JK na Chichiem yake ni bora usipige tuachie sisi wapambanaji
   
 20. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mkakati wa kwanza ni kubalisha katiba ya nchi kwa siku 100 baada ya mgombea kuapishwa, wewe pia utashirikishwa na mambo yote ambayo umeolozesha hapo juu yatakuwa addressed humo.

  anyway, inaonekana huelewi mambo mengi, nafikiri pia unawakilisha wananchi wengi wasiokuwa na upeo, sasa jaribu kupitia mawazo ya wachangiaji watakusadia.

  Wakuu tusikate tamaa watu kama hawa wapo wengi na ndiyo wapiga kura wenyewe tuwasaidie kuwapanua mawazo.
   
Loading...