Sintofahamu yazidi mradi wa umeme wa Kinyerezi II

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,533
3,186
  1. SINTOFAHAMU YAZIDI MRADI WA UMEME KINYEREZI II.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameomba kuliagiza shirika la umeme Tanesco kuangalia upya mkataba wa ujenzi na uendelezaji wa mradi wa umeme wa Kinyerezi II unaotarajiwa kuanza hivi karibuni huku kukiwa na sintofahamu za kila namna.

Sintofahamu hiyo imeendana sambamba na taharuki na hamaki za kisiasa huku baadhi ya wabunge wakiazimia kulipigania suala hilo na kumtaka rais asitishe utekelezaji wa mradi huo mpaka pale taifa litakapojiridhisha kuwa hautazalisha hasara kama inavyodaiwa na vyanzo mbalimbali.

Hilo limetokea mara baada ya kinachodaiwa kufichuka kwa siri kubwa juu ya mradi huo wa umeme wa Kinyerezi 11, ambao unatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwa mradi huo unatariwa kuligharimu taifa zaidi ya sh. trioni 1 mpaka kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo wa kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.

Mradi huo, ambao taarifa zake zimekuwa zikifanywa kwa usiri mkubwa kiasi cha kupelekea wanasiasa na wadau wengine wa maendeleo kuanza kupaza sauti na ‘kupiga kelele’ kuhofia upotevu wa fedha nyingi kwenye mradi huo kama ilivyozoeleka kwenye miradi mingine mingi ya umeme iliyowahi kuripotiwa hapa nchini ikiwemo Richmond, IPTL na Symbion,

Taarifa za uhakika zinasema kwamba tayari serikali imewekeana mkataba na kampuni ya Sumitomo Corporation ya kutoka Japan na kwamba taarifa zinasema mkataba huo utaipelekea Tanzania kulipa fedha nyingi katika mradi huo kulinganisha na miradi mingine inayoshabihiana na huo wa KinyereziII.

Mradi huo unapangwa kugharamiwa kwa uwiano wa asilimia 85 kwa 15 zinazotakiwa kuchangiwa na serikali ya Tanzania ili mradi uanze ambapo taarifa zinasema tayari serikali ya Tanzania imeshatoa sehemu yake..

Mradi wa KinyereziII , ambao unatarajia kuzalisha megawati 240, ambapo mitambo hiyo itakuwa inatumia gesi asilia kutoka Mtwara, ambapo awali watu mbalimbali walikuwa wanapinga ujenzi huo kwa kuwa unaigharimu serikali na nchi kwa ujumla kulinganisha na miradi mingine.

Taarifa ya serikali iliyotolewa na Mkuu wa Mawasiliamo wa wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud inasema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote na kwamba mkataba huo ni halali na umesainiwa kwa kufuata kanuni na taratibu zote za kibiashara tena zenye kulisaidia taifa.

‘’Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Japan ya Mkopo wa masharti nafuu wa dola za marekani milioni 292 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Megawat 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO ya Japan kama Mkandarasi na sio kama Mbia’’. Ilisema taarifa ya Badra

Badra alisema ‘’Mradi huu unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia Tanesco na hakuna mwekezaji mwengine katika mradi huu’’.

Taarifa hii ya Serikali imekuja baada ya kuibuka kwa taarifa za mkanganyiko wa gharama za mradi huo ambapo zipo taarifa zinasema mradi utagharimu dola za marekani milioni 459 sawa na Shilingi Trilioni moja ya kitanzania ikijumuisha gharama za ujenzi, uendeshaji na gharama za dharula.

‘’Rais anatakiwa auzuie huu mradi maana ukitekelezwa kama hivi ulivyo hautakuwa na tija kwa taifa zaidi ya kututia hasara zaidi ya ile ya ESCROW’’. Alisikika akisema mmoja wa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Volkswagen_Audi_gas_to_power_plant_Wertle_Volkswagen.jpg
 
hivi ni nini kinachofanya hio mikataba isiwe open kwa general public sababu sisi ndio serikali na ndio wenye umiliki na sio magufuli wala kikwete kwa nini hio mikataba isiwe open kwa wizara husika kwa yeyote mwenye doubt anawezakwenda kupitia, second hio mikataba ingekua available ingetumika kufundishia wanafunzi wa sheria na course nyingine zinazoendana na hapo elimu yetu ingekua imevuka levels kutoka nadhalia kwenda kwenye realit tafadhali viongozi wa hii nchi mikataba iwe wazi sio tu tanesco hata ile ya Gesi na Madini na ninaamini wzira husika wangepata na michango toka kwa wananch wenye weledi wa hizo sector badala ya kufichaficha

Note: kwa MEDIA mnauwezo wa kufatilia na kuweka wazi hio mikataba badala ya kufatilia habari za kina sepetu ambazo hazina tija
 
Mara nyengine Jazba ya umimi na uzawa na hali hamna kitu mnachoweza kufanya wenyewe utalirudisha hil taifa nyuma. Sio muwe mnapinga tu kila kitu serikali inakifanya au sababu mradi hawakupewa MECO na akina Mengi. Hela yenyewe ya mkopo wenye masharti na legal binders. Mnatakiwa muwe weledi wa kiufundi katika mikataba ya mikopo na biashara, muwe weledi wa commercial laws muwe weledi katika Infrastructure projects managment na kadhalika na kadhalika. Utashi na ubishi wa kisiasa uwekwe pembeni kwa maslahi ya nchi katika kutatua uoza wa ikosefu wa mahitaji muhimu ya msingi kwa wananchi wote.
CCM na vyama vyengine vyote muache ku siasia (politicizing) katika mambo ya mahitaji ya msingi ya wananchi. Maana na hata huo mkopo viongozi wa CCM mnajiringia eti juhudi yenu hata pale nchi inapo kopeshwa kwa makusudi na wafadhili wetu wanapo ona nchi na wananchi wake wana shida kwa siasa mbovu na ufisadi eti nyinyi mnageuza ni kete yenu kisiasa ndio maana hamuaminiki hata mkifanya la maana. Mnapopewa mikopo ya makusudi au sadaka (grants) haina maana siasa zenu zekubalika na wafadhili.
Ni kuwa wanajuwa kuwa hata mkiondoka madarakani basi wanaoluja kushika nchi watabaki na makubaliano ya serikali zilopita na watalipa au kuenzi mgao waliopewa na kuzitumia hela katika mradi uliokusudiwa bila ya ubabaishaji. Nanyi wadau kama ni wapinzani juu yenu ni kumulika na kuchukuwa vielelezo vyovyote venye viashiria vya ufisadi na kufuatilia mahesabu kila mwisho wa mwaka au muhula (phase) wa mradi lakini sio kuzuia mradi ambao utatunufaisha sote. Mnadhani wafadhili wakizuia hizo hela na matajuri ya nchi yetu ni matupu wapi atatokea mtu akatupa hizo hela kwa haraka haraka kama hivyo. Muwe waangalifu katika mambo yanayotugusa sote.
Ila si vibaya kuwasitua mapema.
 
  1. SINTOFAHAMU YAZIDI MRADI WA UMEME KINYEREZI II.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameomba kuliagiza shirika la umeme Tanesco kuangalia upya mkataba wa ujenzi na uendelezaji wa mradi wa umeme wa Kinyerezi II unaotarajiwa kuanza hivi karibuni huku kukiwa na sintofahamu za kila namna.

Sintofahamu hiyo imeendana sambamba na taharuki na hamaki za kisiasa huku baadhi ya wabunge wakiazimia kulipigania suala hilo na kumtaka rais asitishe utekelezaji wa mradi huo mpaka pale taifa litakapojiridhisha kuwa hautazalisha hasara kama inavyodaiwa na vyanzo mbalimbali.

Hilo limetokea mara baada ya kinachodaiwa kufichuka kwa siri kubwa juu ya mradi huo wa umeme wa Kinyerezi 11, ambao unatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwa mradi huo unatariwa kuligharimu taifa zaidi ya sh. trioni 1 mpaka kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo wa kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.

Mradi huo, ambao taarifa zake zimekuwa zikifanywa kwa usiri mkubwa kiasi cha kupelekea wanasiasa na wadau wengine wa maendeleo kuanza kupaza sauti na ‘kupiga kelele’ kuhofia upotevu wa fedha nyingi kwenye mradi huo kama ilivyozoeleka kwenye miradi mingine mingi ya umeme iliyowahi kuripotiwa hapa nchini ikiwemo Richmond, IPTL na Symbion,

Taarifa za uhakika zinasema kwamba tayari serikali imewekeana mkataba na kampuni ya Sumitomo Corporation ya kutoka Japan na kwamba taarifa zinasema mkataba huo utaipelekea Tanzania kulipa fedha nyingi katika mradi huo kulinganisha na miradi mingine inayoshabihiana na huo wa KinyereziII.

Mradi huo unapangwa kugharamiwa kwa uwiano wa asilimia 85 kwa 15 zinazotakiwa kuchangiwa na serikali ya Tanzania ili mradi uanze ambapo taarifa zinasema tayari serikali ya Tanzania imeshatoa sehemu yake..

Mradi wa KinyereziII , ambao unatarajia kuzalisha megawati 240, ambapo mitambo hiyo itakuwa inatumia gesi asilia kutoka Mtwara, ambapo awali watu mbalimbali walikuwa wanapinga ujenzi huo kwa kuwa unaigharimu serikali na nchi kwa ujumla kulinganisha na miradi mingine.

Taarifa ya serikali iliyotolewa na Mkuu wa Mawasiliamo wa wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud inasema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote na kwamba mkataba huo ni halali na umesainiwa kwa kufuata kanuni na taratibu zote za kibiashara tena zenye kulisaidia taifa.

‘’Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Japan ya Mkopo wa masharti nafuu wa dola za marekani milioni 292 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Megawat 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO ya Japan kama Mkandarasi na sio kama Mbia’’. Ilisema taarifa ya Badra

Badra alisema ‘’Mradi huu unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia Tanesco na hakuna mwekezaji mwengine katika mradi huu’’.

Taarifa hii ya Serikali imekuja baada ya kuibuka kwa taarifa za mkanganyiko wa gharama za mradi huo ambapo zipo taarifa zinasema mradi utagharimu dola za marekani milioni 459 sawa na Shilingi Trilioni moja ya kitanzania ikijumuisha gharama za ujenzi, uendeshaji na gharama za dharula.

‘’Rais anatakiwa auzuie huu mradi maana ukitekelezwa kama hivi ulivyo hautakuwa na tija kwa taifa zaidi ya kututia hasara zaidi ya ile ya ESCROW’’. Alisikika akisema mmoja wa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 317633
WanaJF, hebu naomba tulinganishe gharama hizi za ujenzi wa bomba la gesi
International Average Cost
*12- inch pipeline costs about $ 300,000 per 1 mile
*42- inch pipeline costs about $ 1.5 Million per 1 mile.

Tanzania average cost
*36- inch pipeline costs about $ 2.3 million per 1 km. Na bado inaonekana kuna sehemu litawekwa bomba lenye inch 24.

Serikali inasema, Mpango huu wa bomba la gesi unahusisha ujenzi wa bomba la inchi 36 kwa umbali wa kilomita 487 na bomba la inchi 24 kwa umbali wa kilomita 24, likiunganisha bara hadi kwenye chanzo cha gesi iliyoko Somanga Fungu, kisiwa kidogo katika Bahari Hindi. Bomba hilo lenye urefu wa km 512 (wengine wanasema km 532) litajengwa kwa Gharama ya $ 1.2 bn, ambayo ukifanya mahesabu utapata gharama kwa km 1

Japokuwa Pipeline Economics zinaonyesha kuwa Gharama hizo za kimataifa zinaweza kuongezeka, kulingana na ukubwa wa bomba husika, bado hali halisi inaonyesha kuwa hili linalojengwa Tanzania litakuwa la inch 36 na na lingine nchi 24. Sasa ni kwa nini gharama hizo ziwe kuwa inflated kwa kiwango kikubwa namna hii? Je ni nani anafaidika? Tafakari

Updates
Mradi kama huu wa kwetu unafanyika Pakistan, ( Iran Pakistan Gas Pipeline Project) lakini cha kushangaza ni kwamba kwa upande wa Pakistani bomba lenye urefu wa 785km litajengwa kwa gharama ileile ya $ 1.2 bn, lakin bomba lao litakuwa la 42 inch (now do the math)
 
Mara nyengine Jazba ya umimi na uzawa na hali hamna kitu mnachoweza kufanya wenyewe utalirudisha hil taifa nyuma. Sio muwe mnapinga tu kila kitu serikali inakifanya au sababu mradi hawakupewa MECO na akina Mengi. Hela yenyewe ya mkopo wenye masharti na legal binders. Mnatakiwa muwe weledi wa kiufundi katika mikataba ya mikopo na biashara, muwe weledi wa commercial laws muwe weledi katika Infrastructure projects managment na kadhalika na kadhalika. Utashi na ubishi wa kisiasa uwekwe pembeni kwa maslahi ya nchi katika kutatua uoza wa ikosefu wa mahitaji muhimu ya msingi kwa wananchi wote.
CCM na vyama vyengine vyote muache ku siasia (politicizing) katika mambo ya mahitaji ya msingi ya wananchi. Maana na hata huo mkopo viongozi wa CCM mnajiringia eti juhudi yenu hata pale nchi inapo kopeshwa kwa makusudi na wafadhili wetu wanapo ona nchi na wananchi wake wana shida kwa siasa mbovu na ufisadi eti nyinyi mnageuza ni kete yenu kisiasa ndio maana hamuaminiki hata mkifanya la maana. Mnapopewa mikopo ya makusudi au sadaka (grants) haina maana siasa zenu zekubalika na wafadhili.
Ni kuwa wanajuwa kuwa hata mkiondoka madarakani basi wanaoluja kushika nchi watabaki na makubaliano ya serikali zilopita na watalipa au kuenzi mgao waliopewa na kuzitumia hela katika mradi uliokusudiwa bila ya ubabaishaji. Nanyi wadau kama ni wapinzani juu yenu ni kumulika na kuchukuwa vielelezo vyovyote venye viashiria vya ufisadi na kufuatilia mahesabu kila mwisho wa mwaka au muhula (phase) wa mradi lakini sio kuzuia mradi ambao utatunufaisha sote. Mnadhani wafadhili wakizuia hizo hela na matajuri ya nchi yetu ni matupu wapi atatokea mtu akatupa hizo hela kwa haraka haraka kama hivyo. Muwe waangalifu katika mambo yanayotugusa sote.
Ila si vibaya kuwasitua mapema.
WanaJF, hebu naomba tulinganishe gharama hizi za ujenzi wa bomba la gesi
International Average Cost
*12- inch pipeline costs about $ 300,000 per 1 mile
*42- inch pipeline costs about $ 1.5 Million per 1 mile.

Tanzania average cost
*36- inch pipeline costs about $ 2.3 million per 1 km. Na bado inaonekana kuna sehemu litawekwa bomba lenye inch 24.

Serikali inasema, Mpango huu wa bomba la gesi unahusisha ujenzi wa bomba la inchi 36 kwa umbali wa kilomita 487 na bomba la inchi 24 kwa umbali wa kilomita 24, likiunganisha bara hadi kwenye chanzo cha gesi iliyoko Somanga Fungu, kisiwa kidogo katika Bahari Hindi. Bomba hilo lenye urefu wa km 512 (wengine wanasema km 532) litajengwa kwa Gharama ya $ 1.2 bn, ambayo ukifanya mahesabu utapata gharama kwa km 1

Japokuwa Pipeline Economics zinaonyesha kuwa Gharama hizo za kimataifa zinaweza kuongezeka, kulingana na ukubwa wa bomba husika, bado hali halisi inaonyesha kuwa hili linalojengwa Tanzania litakuwa la inch 36 na na lingine nchi 24. Sasa ni kwa nini gharama hizo ziwe kuwa inflated kwa kiwango kikubwa namna hii? Je ni nani anafaidika? Tafakari

Updates
Mradi kama huu wa kwetu unafanyika Pakistan, ( Iran Pakistan Gas Pipeline Project) lakini cha kushangaza ni kwamba kwa upande wa Pakistani bomba lenye urefu wa 785km litajengwa kwa gharama ileile ya $ 1.2 bn, lakin bomba lao litakuwa la 42 inch (now do the math)
 
Ivi ni wapi nchi hii ni pasafi? kila sehemu kunaharufu ya ufisadi

Back
Top Bottom