Sintofahamu yatanda kwa walimu wa sanaa katika shule za sekondari hapa nchini juu ya kuhamishiwa shule za msingi (IKAMA)

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
Toka mwaka huu uanze; walimu wa sanaa katika shule za sekondari hapa nchini wamegubikwa na simanzi ikiambatana na Msononeko juu ya Hii operation inayotekelezwa nchi nzima ya kuwahamishia shule za msingi.

Waraka uliotolewa unadai kuwa Walimu wa sanaa katika shule za sekondari ni wengi sana hadi imekuwa kero huku waraka huo huo ukibainisha wazi kuwa "Kuna uhaba wa walimu wa science na hisabati katika shule za sekondari na msingi".

Hivo basi serikali imeamua mara moja kuwapunguza walimu wa sanaa waliojazana katika shule za sekondari mikoa yote kwenda kufundisha shule za msingi.

Serikali imebainisha kuwa utaratibu huu hautoathiri mishahara yao na stahiki nyingine zote ambazo mwalimu alipaswa kuzipata akiwa sekondari.

Kwa sasa walimu wa sanaa katika mashule wamejawa na pressure za kupanda na wengine za kushuka kwani hakuna hata mmoja anaejua kuwa yeye atabakizwa au atashushwa!

Hakuna mwalimu hata mmoja wa sekondari ambaye amefurahishwa na agizo hili kwani wanaona kuwa wamepewa demotion na kuwa wataathirika kisaikolojia na watadharaulika mitaani.

Malalamiko yao:

1. Wanahoji kuwa iweje leo wapelekwe kufundisha shule ya msingi ilihali wao hawakujifunza saikolojia ya kumlea mtoto wa shule ya msingi?

Walimu wengi wana shahada walizozipata katika vyuo mbalimbali. Na kwenye vyuo hivo hawakuandaliwa kwenda kufundisha shule za msingi! Waliandaliwa kwenda kufundisha sekondari. Kwa maana hii basi wanaona kuwa itawawia ngumu.

Walimu wanadai kama serikali imegundua kuwepo na uhaba wa walimu wa science katika shule za Sekondari na Msingi kwa nini isiajiri walimu hao ilihali kuna wahitimu kibao mitaani wa masomo ya science?

Pia wanadai; Je mwalimu huyu wa sanaa anaeshushwa kwenda shule ya msingi ndio yeye anaeenda kufundisha masomo hayo ya science huko? Je ataweza nawakati yeye hakusomea science.

2. Mwalimu mmoja kuwa na idadi ya vipindi 24 kwa wiki.

Hili nalo limekuwa lalamiko kweli kweli. Wanadai kuwa kama kila mwalimu anatakiwa kuwa na vipindi 24 kwa wiki inamana kwamba Kwa somo moja litatakiwa kuwa na walimu 2 tu.

Kwa hali hiyo sasa ya wingi wa vipindi itamfanya mwalimu huyo kushindwa kutekeleza majukumu mengine ya kikazi kama: Mwalimu wa taaluma, mwalimu wa nidhamu, mwalimu wa Darasa; mwalimu wa mazingira; mwalimu wa Zamu; mwalimu wa miradi, mwalimu wa michezo n.k.


Matokeo ya huu mkakati wa IKAMA.

1. Kushuka kwa Morali ya kazi.

Walimu watakaoshushwa kwenda kufundisha shule za msingi watakaa taklibani mwezi mzima wanauguza vidonda vyao vya kushushwa na hapo morali ya kazi itapungua kwani muda wote watakuwa wanaona kuwa si mahala pao pa kazi. Mpaka waje waizowee hiyo hali itawachukuwa muda mwingi sana.

Pia na walimu watakaobahatika kubaki huko sekondali watakuwa na Overwork. Watakuwa wachache sana na watalazimika pia kugawana majukumu mengine kama kushika zamu ya wiki na majukumu mengine nje ya darasani. Kwa maana hii basi watakosa molari ya kazi na mambo hayatoenda kama ilivokuwa hapo awali.

2. Ufaulu kushuka.

Ifahamike kuwa miaka yote masomo ya sanaa ndio huwa yanaongoza kwa kufaulisha kuliko masomo ya science na hisabati na huu ndo ukweli halisi ambao hautilii shaka.

Walio wazazi wengi tumezoea kuona mwanafunzi kapasua sana masomo ya sanaa kwa kupata alama za A, B na pengine kapata alama D masomo ya science na pengine ka alama C kamoja katika mojawapo ya masomo hayo ya science na mwanafunzi huu kuchaguliwa kwenda kusoma Mchepuo wa Science. Hii ni kutikana na Sera ya serikali ya awamu hii ya tano kutilia mkazo sana kwenye masomo ya Science!

Kuwepo kwa walimu wa kutosha wa sanaa ni mojawapo ya ufaulu huo kwani wanafunzi walikuwa wakipata huduma yakutosha. Ratio ya walimu na wanafunzi ilikuwa sawa kwa 100%

Kwa nini masomo ya science hayafanyi vizuri? Hii ni kwa sababu ya uhaba wa walimu katika mashule hivo basi kupelekea matokeo mabaya. Ukijaribu kucheki ratio ya waafunzi na walimu wa science katika mashule hauko sawa. Walimu ni haba hivo basi kupelekea kufeli kwa namna hiyo.

3. Kuwepo tena kwa uhaba wa walimu.

Hii itakuja kwa namna hii:

- Likizo ya Uzazi. ( Maternity Leave)

Chukulia kwa mfano hii likizo ya uzazi kwa akina mama ambayo ni haki yao. Sasa chukulia kwamba IKAMA imebalance kwenye shule fulani na walimu wamebaki hao wawili kwenye hilo somo fulani. Maana yake mmoja atafundisha kidato cha kwanza hadi cha pili na mwingine kidato cha 3 hadi cha 4. Sasa hapa mmoja wapo amejifungua na kapata Maternity leave ambayo ni miezi 3; Je serikali haioni kuwa itasababusha upungufu wa walimu muda huo maana atakuwa hayupo kazini?Je hayo madarasa yake nani atakuwa akiyafundisha kwa muda huo ambao atakuwa hayupo?

- Kustaafu.
Pia hii italeta uhaba wa walimu kwani itafika kipindi tu kwenye shule fulani mwalimu astaafu. Je kwenye idara yake ( maana wako wawili tu) nani atakava nafasi yake?

- Kifo

Kama tujuwavyo kila nafsi itapata umauti. Sasa kwa mfano kwenye shule fulani mwalimu amefariki na kwenye idara yake walikuwa 2 au 3 je hapo si dhahiri shahiri kuwa kutakuwa na shida ya mwalimu mwingine?

- Semina na Kazi Maalumu ( Kusimamia mitihani, n.k)

Shida nyingine itakayoleta upungufu wa walimu japo kwa muda kidogo ni kama kwenye idara fulani ya somo fulani mwalimu mmoja ameenda kwenye semina au kufanya kazi maalumu kwa muda fulani na kwenye idara yao wako 2 au 3 je hapo si wanafunzi watakosa huduma ya kufundishwa kama inavyopaswa? Au; hapo si dhahiri shahiri kuwa walimu hao wanaobaki watakuwa na kazi kubwa sana juu ya mzigo mkubwa walokuwa nao kwa kukava vipindi vya huyo ambae hayupo?

- Kwenda Kusoma.

Hii pia itaathiri sana. Kwani kujiendeleza kielimu ni haki ya mtanzania kikatiba. Sasa chukulia kwa mfano idara ya somo fulani ilikuwa nawalimu 2 au 3 na mmoja wao ameenda kujiendeleza kielimu. Je hapo si wazi kabisa kuwa kwenye idara hiyo kutakuwa na upungufu wa mwalimu? Au wataomba tena mwalimu mmoja apandushwe tena toka shule ya msingi kuja kuziba pengo hilo!
Lasivyo Serikali inaweza kuwa inatatua tatizo hili kumbe inattengeneza tatizo lingine hapo baadae!


My take:

Mosi; Serikali haikupaswa kuwashusha walimu hao wa sanaa kwenda shule za misingi bali ingejaribu kuwapunguza toka kituo kimoja cha kazi ( shule ya sekondari) chenye walimu wengi kwenda kituo kingine cha kazi( shule ya sekondari) chenye upungufu wa walimu kwani ni ukweli usiopingika kuwa shule za vijijini na za ndani ndani sana hazina walimu wakutosha. Hata hao walimu wa sanaa hawapo kabisa na ni shida tu. Walimu wengi wamejazana katika mashule ya mijini.

Pili; Serikali ingeajiri walimu wa kutosha wa masomo ya Science na hisabati kwenye shule za Sekondari na Msingi ili kutatua hiyo changamoto ya uhaba wao.
 
Kwa uandishi huu kama wewe ni MWL wa sekondari ni halali yako kupelekwa shule ya Msingi. Ni kweli wamezidi na wanalipwa mishahara wakati mzigo wao wa ufundishaji ni mdogo huko sekondari. Naunga mkono waraka kwa maendeleo ya kunusuru wadogo zetu wenye uhaba wa walimu. Kutojua sikolojia ya mtoto mdogo hilo ni dogo kwa mwalimu yeyote kwani semina zitatolewa wakati wa likizo kupitia vyuo vya ualimu kote nchini na wakufunzi wa elimu msingi. Serikali yetu haina pesa za ajira mpya.
 
Kwa uandishi huu kama wewe ni MWL wa sekondari ni halali yako kupelekwa shule ya Msingi. Ni kweli wamezidi na wanalipwa mishahara wakati mzigo wao wa ufundishaji ni mdogo huko sekondari. Naunga mkono waraka kwa maendeleo ya kunusuru wadogo zetu wenye uhaba wa walimu. Kutojua sikolojia ya mtoto mdogo hilo ni dogo kwa mwalimu yeyote kwani semina zitatolewa wakati wa likizo kupitia vyuo vya ualimu kote nchini na wakufunzi wa elimu msingi. Serikali yetu haina pesa za ajira mpya.

Nakuunga mkono kuhusu uandishi mbovu wa hiyo Mwalimu na hakika hakustahili kurudishwa shule ya msingi Bali chekechea akaimbe na vijana wetu wadogo

Zoezi zima la uhamishaji wa walimu wa shule za sekondari kufundisha shule za msingi ni wazo baya zaidi kutolewa na viongozi ambao wamewahi kuwa walimu na matokeo/ athari zake zitaonekana baada ya muda tujiandae kuwa na academic dwarf na nchi kuendelea kuwa shithole

Mwalimu wa sekondari amesomea mbinu za kufundisha vijana wa rika hilo sasa unampeleka kufutdisha watoto ataweza?

Psychology ya watoto hayo wa primary ni tofauti na psychology ya watoto wasekondari ataweza?

Natambua kunawezekana kukawa na seminars elekezi lakini zitakua zima moto je zitatibu maradhi haya ya elimu tuliyonayo?
 
Kwa uandishi huu kama wewe ni MWL wa sekondari ni halali yako kupelekwa shule ya Msingi. Ni kweli wamezidi na wanalipwa mishahara wakati mzigo wao wa ufundishaji ni mdogo huko sekondari. Naunga mkono waraka kwa maendeleo ya kunusuru wadogo zetu wenye uhaba wa walimu. Kutojua sikolojia ya mtoto mdogo hilo ni dogo kwa mwalimu yeyote kwani semina zitatolewa wakati wa likizo kupitia vyuo vya ualimu kote nchini na wakufunzi wa elimu msingi. Serikali yetu haina pesa za ajira mpya.

Uyu hafai kufundisha shule ya msingi.
 
Wakati Shule za Sekondari za Kata hazina walimu tunapeleka Shule za Msingi,Awamu hii naona kuna kama kadizaini kakurudisha nyuma ELIMU yetu ili tutawaliwe na Majirani huko baadaye
shule za sekondari walimu wa sanaa ni wengi wamezidi walimu wa sayansi ndio wanahitajika hao wacha warudi kufundisha shule za msingi kwanza wengi wao wamefeli form four
 
Sijaona point ya msingi hapo. Kuwa mwalimu alijifunza kufundisha wnfnz. Wa sec school ndio ashindwe kufundisha Pr. School.

Je wanajeshi wetu wanaopata mafunzo nchini lakini wanaenda kupigana Vita Sudan, DRC, Lebanon na Sudan nao wasemeje???
Ulitaka nao waseme wamezoea kukimbizana kwenye mapori ya Tanzania na hivo hawawezi kujificha kwenye Misitu ya Kongo?

Cha msingi serikali iendelee kulinda Maslah ya walimu hao. Ikiwa ni pamoja na kupata stahiki zao zote na pia bila kusahau inclination ya madaraja na mishara bila kubagua kada.

Nawashauri walimu waione hii nafasi kama exposure kwao na sio demotion kama mtoa mada alivyo wasilisha
 
Back
Top Bottom