Sintofahamu ya wanafunzi waliofaulu kidato cha 4 mwaka Jana.

Lugombo Nsesi

Senior Member
Jun 16, 2016
126
149
Wanajamii naombeni maoni yenu na hili suala. Tangu yatangazwe matokeo mwezi wa tatu mpaka sasa wanafunzi waliofaulu hawajapangiwa shule za kusoma. Kikawaida shule zinafunguliwa mwezi ujao mwanzoni, wazazi watajiandaa lini kuwapeleka watoto hayo Shuleni?
Ikumbukwe kwamba kidato cha 5 hawapo katika mpango wa elimu buree..
Kunashida gani wizara ya elimu....??
Mhusika ni nani hapo, wizara ya elimu au baraza la mitihani???
It is serious jamani toeni mawazo nipate kujua hilo.
NAWASILISHA!!!
 
Baraza la mitihani halihusiki maana kama matokeo lilishatoa. Ni jukumu la wizara husika ya Mama Ndali. Yawezekana masomo ya mwaka huu yamesitishwa. labda waliofanya mitihani ya kidato cha nne mwaka jana wote walikuwa vilaaazaa
 
Nakumbuka mwaka jana muda wa kujiandaa kitu kama haujuzidi wiki tatu. Yaani kuliwa na wiki chini ya 4 kati ya kutangazwa kwa shule wakizopangiwa na siku ya kufungua shule.
Hawa jamaa hawajali kabisa wananchi sijui kwa vile watoto wao wanasoma nje na hata wakati wa kwenda shule hupanda ndege.
 
Kama mwanao kafaulu lakini unasubiria mpaka apangiwe shule ndiyo uanze kujiandaa una matatizo kichwani.

Toka upate matokeo mpaka sasa una subiria nini kujipanga?

Hakuna sitofahamu hapo subirieni taarifa tu.
 
Zipo shule wanafunzi wa form five wanakaribia kumaliza muhula wa kwanza, wewe subiri ofa ya bure.
 
Wasio na mda na serikali wstoto wao saizi wanaelekea maliza topics za f V ... Wwe endelea subiri..
 
Unajua viongozi wengi wanajua watu wengi wana pesa kwamba hata ukimkurupusha ana pesa kitu ambacho si kweli.
 
Kama mwanao kafaulu lakini unasubiria mpaka apangiwe shule ndiyo uanze kujiandaa una matatizo kichwani.

Toka upate matokeo mpaka sasa una subiria nini kujipanga?

Hakuna sitofahamu hapo subirieni taarifa tu.
Atakuwa ana subiri elimu bure, lakini atambue elimu bure mwisho ni kidato cha nne, kidato cha tano hadi sita unalipa ada, lakini pia ufahamu tuition ni lazima, najua walimu hakuna hasa wanaosoma sayansi.
 
Back
Top Bottom